Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 42
Mkuu JokaKuu, tatizo kubwa liko kwenye system ya uongozi wa nchi. System ambayo haina controls za kutosha kuhakikisha kuwa kuna uwajibikaji, na nidhamu ya kutosha.Bongolander,
..nadhani kuishi nje peke yake siyo kigezo kikuu cha kumpa mgombea uongozi.
..nadhani tunapaswa kuwa makini zaidi ktk kuchagua viongozi kuliko ku-base kwenye upinzani wa walioishi nje vs walioshi nyumbani.
..mgombea anapaswa kuwa na sifa za ziada juu ya kufanya kazi na kusoma nje ya nchi.
..kuna tatizo kubwa sana hapa Tanzania na limeshindikana kutatuliwa hata kwa kurudisha nchini wataalamu wetu waliofanya kazi nje. tatizo hilo ni utamaduni wa rushwa, wizi, na ubadhirifu. watu kama Dr.Balali walifanya kazi kwa uadilifu mkubwa ktk mashirika ya kimataifa, mara waliporudi Tanzania wamejitumbukiza ktk rushwa na ubadhirifu wa kutisha.
..sasa pamoja na kulaumu kwamba wataalamu wetu wanaorudi toka nje wametuangusha, labda tuangalie ni mazingira gani ya ndani ya Tanzania yanasababisha tunaangushwa[tunaibiwa,tunahujumiwa] na kila mhusika anayepewa madaraka.
..vijana, wanawake, wazee,...kila anayepata uongozi Tanzania ya leo haichukui muda mrefu anatumbukia ktk mambo ya ufisadi. tuna tatizo kubwa sana Tanzania na kwa kweli linahitaji umakini na uzalendo wa hali ya juu kulitatua.
Kama kiongozi wa juu wa serikali akiwa anavumilia makosa ya watendaji wa chini, ni dhahiri kuwa hata wale wenye nia njema na wenye uwezo kiutendaji watachoka kuwa watiifu na wachapakazi kwa malengo yanayotarajiwa na wengi.
Ni kwasababu hii, ndio maana ninafuraha kubwa kuona na kusikia kuwa Dr. Slaa amejitokeza na kupendekezwa na chama chake kuwa mgombea uRais. Furaha yangu inasababishwa na mambo kadhaa.
1. Ni nafasi ya kubadili mfumo mbovu wa kuvumiliana kwa manufaa machanga ya kisiasa
2. Ni nafasi nzuri na adimu ya kupata mtu mpya mwenye mawazo mapya kutoka katika chama kipya
3. Na kubwa zaidi, ni kwa kuwa ni vizuri kuubadili uongozi wa nchi baada ya kila dalili kuonyesha kuwa huko tunakokwenda hakuna nuru kwa kuwa mshika mshumaa ameuzima na hana kiberiti cha kuuwasha tena.