Pre GE2025 Kinyang'anyiro cha Urais 2025 kwa tiketi ya CCM: Dkt Mwinyi kuwania Urais wa Muungano?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa hiyo hii nchi Raia wengine hawana haki yaani , watoto wa viongozi tu ndio wanatakiwa kupokezana uongozi !

Tena watoto wenyewe hawana uzalendo wowote ule , Wengine walikataa hata kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa kiburi tu , kwa vile Baba zao ni viongozi .

Poor Tanzania !
 
Kwa akili yako unafikiri Mwinyi ndio anaamua kumpinga Samia?

Magufuli mwenyewe hakutaka Samia awe makamu wake ila wenye maamuzi wakalazimisha

..walimlazimisha Magufuli kwasababu alikuwa hajapata Uraisi.

..mtu akiwa raisi wa Tanzania na Amiri jeshi mkuu hakuna yeyote ndani ya mipaka yetu anayeweza kum-challenge na kumpangia nini afanye.

..Raisi wa Tanzania ni sawa na mungu-mtu, chochote anachokitaka kkinatekelezwa. Kwa katiba na mifumo tuliyonayo tunasubiri huruma ya Mama kuhusu kitakachotokea 2025.

..Vilevile msifikiri kwamba Magufuli alikufa na kuzikwa pamoja na genge lake la watesaji. Wale jamaa wapo benchi na Mama akiamua anaweza kuwatumia.
 
Hili bandiko sio bure, nadhani limekuja kimkakati zaidi, JF ni jukwaa Pana Sana, wanaoingia humu hawasemeki, hawachangii wala kuanzisha Uzi wowote, Ila wana nguvu kubwa, sasa kwa huu ujio wa mleta taarifa nadhani hao wakaa kimya wamekuja kivingine.
NINAONAVYO MIMI : MAMA KAINGIA CHAKA KUMRUDISHA BASHITE, bila Shaka hili linaweza kumtafuna, tusubiri tuone.
Inawezekana pia kwamba uchafuzi ndani ya Chama utawafaidisha wale wanaotaka kurudi UARABUNI, wakiwa nje ya Muungano. rais wa jamhuri ya Muungano siku zote awe wa MUUNGANO kweli, na sio mchana tu. Hata usiku pia.
 
Miongoni mwa siri zilizofichuliwa leo kuhusu Mkataba wa kuiuzia kampuni ya Waarabu Bandari za Tanzania, imo habari kwamba Bandari zitakazohusika ni zile za Tanganyika Pekee, za Zanzibar hazitahusika.

Ikumbukwe kwamba Bandari ni miongoni mwa mambo ya Muungano, ikiwa kama jambo hili lina faida kwanini tunaitenga Zanzibar. Je, Wazanzibar hawataki faida?

Tafakuri inatafakarisha sana;-

1. Kwanini mkataba umevuja kwa hatua za awali?
2. Je kuna mwananchi wa kawaida au hao walioingia mkataba ambaye ameuvujisha?
3. Baada ya tafakuri ya (2.) Umadhani nani kavujisha?
4. Je ni kweli kila jambo hutokea kwa makusudi maalum?
5. Unadhani ni makusudio gani waliyonayo wavujisha mkataba?

Ndiyo maana hata lile bomu la DP World taarifa ilipenyezwa na mtu wa ndani ya system kwenda CHADEMA ili kumwambia Mama safari yake ni mwisho 2025.
Nakushauri kuzisoma hizo quotation zote na kwa urefu wake.

Wako, Nkaburu.
 
Angalizo kwa Wanabodi na Mode

Hii no C&P kutoka kwa mwana JF fulani.
Kwasababu mwandishi ni member wetu humu na humu hajaileta, naomba ikitokea ameileta humu, then futa hili bandiko langu.

Nime C&P kwasababu mimi ni miongoni mwa watu wa mwanzo mwanzo kuandika humu kuwa mgombea urais wa CCM kwa uchaguzi wa 2025 could be Dr. Hussein Mwinyi, kupitia bandiko hili Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Hivyo hoja kama hii inapotolewa na mwajeiefu mwenzetu, mwandamizi kama huyu, hivyo nimejikuta ni muhimu kuisambaza.

Paskali.

Barua ya...

Kwa kiasi kikubwa, siasa za Tanzania zimejikita zaidi kwenye chaguzi, hususan uchaguzi mkuu. Kwamba vyama vya siasa hutumia muda mwingi kujiandaa na chaguzi kiasi kwamba kuna dhana kwamba haviwatumikii wananchi vya kutosha kutokana na hilo.

Lakini lengo kuu la chama chochote cha siasa ni kushika dola. Na katika nchi za kidemokrasia, kushika dola kunawezekana kwa njia moja tu, yaani uchaguzi mkuu. Kwa mantiki hiyo, ni sahihi kwa vyama vya siasa kujipanga vema kwa ajili ya chaguzi.

Na kwa chama tawala, kisipofanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya chaguzi zijazo, nafasi yake kama chama kinachoshika dola inakuwa hatarini.

Ni katika mazingira hayo ndio maana kumekuwa na maongezi mengi kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 japo bado miaka miwili hivi kabla ya uchaguzi huo. Na japo kuna chaguzi za serikali za mitaa mwakani, maongezi mengi ni kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Taarifa za kiintelijensia zinaeleza kwamba kuna jitihada zinafanyika huko Zanzibar kumwezesha Dkt Hussein Mwinyi kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano mwaka 2025.

Si tayari CCM “ina mgombea wake” 2025?
Naam. kwa mujibu wa utaratibu usio rasmi huko CCM, rais aliyepo madarakani anakuwa automatically mgombea pekee wa urais mwaka katika uchaguzi utakaomuingiza awamu ya pili ya urais wake.

Ilikuwa hivyo kwa Mkapa mwaka 2000, Jk 2010 na Magufuli 2020. Na inatarajiwa iwe hivyo kwa Mama Samia 2025.

Hadi wakati makala hii inaandikwa haijafahamika rasmi kwanini kuna mpango huo amba sio tu utapelekea “kuukoroga utaratibu huo usio rasmi wa Rais aliyepo madarakani kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo ili akamilishe ngwe zote mbili” bali pia utakuwa upinzani baina ya wanasiasa wawili kutoka Zanzibar.

Maandalizi yameanza
Taarifa zinaeleza kwamba tangu Zanzibar ijiunge na Tanganyika mwaka 1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna kipindi ambapo upande huo wa Muungano umepokea fedha nyingi kutoka serikali ya Muungano kama kipindi hiki cha utawala wa Mama Samia.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa sehemu ya fedha hizo zimekuwa zikitumiwa na wanamkakati wa mpango huo wa kumwezesha Dkt Mwinyi kuwa mgombea mwaka 2025.

Licha ya ukweli kuwa maandalizi ya uchaguzi wowote hule huhitaji fedha za kutosha, yaaminika kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 utatawaliwa na matumizi makubwa ya fedha hasa kutokana na ukweli kwamba wanasiasa wengi wamepoteza mvuto machoni mwa wananchi na njia pekee ya “kupendeka” ni kumwaga fedha.

Mama Samia anawarahisishia kazi wapinzani wake ikiwa ni pamoja na mwanasiasa huyo wa Zanzibar
Kuna matukio mawili makubwa ambayo yanatarajiwa “kumsumbua” Mama Samia kati ya sasa na uchaguzi mwaka 2025. La kwanza ni suala la mkataba wa bandari ambalo japo “kwa nje ya CCM” linaonekana kama lilikuwa lina mwafaka miongoni mwa wana-CCM, ukweli ni kwamba sio tu lilizua mgawanyiko wakati wa mjadala bali pia limeacha makovu ambayo yanaweza “kukwanguliwa” pindi kampeni za urais zitaposhika kasi.

La pili ni hili la “Mama Samia kujichoma msumari mwenyewe” kwa kumteua Bashite kuwa katika mwenezi wa chama hicho, huku akifahamu fika kuwa kada huyo anachukiwa na wengi ndani na nje ya chama hicho.

Japo Mama Samia anatarajia kuwa Bashite atamsaidia kukabiliana na “wapinzani wake”, nguvu za kada huyo huko nyuma zilitegemea zaidi staili ya uongozi wa kibabe wa marehemu Magufuli, ambayo ni tofauti na satili ya uongozi wa Mama Samia, unless aamue kubadilika.

Hitimisho
Kuna msemo kuwa kwenye siasa, wiki moja ni sawa na uhai mzima (lifetime). Na kwa hakika, kati ya sasa Novemba 2023 hadi Oktoba 2025 ni takriban miaka miwili, na mengi yanaweza kutokea aidha kuimarisha dhamira ya mwanasiasa yeyote mwenye ndoto za kumpiku Mama Samia au urais wa Mama Samia ukaimarika zaidi kiasi kwamba yeyote mwenye ndoto za kum-challenge atakuwa anapoteza muda wake.

Mwana if fulani.
C&P by Paskali
p
kwanza nikushukuru Kwa bandiko lako, naomba nitoe maoni yangu kidogo

1)ulichokieleza na hapa between the lines ni kuwa mama hatokuwa miongoni mwa wagombea wa urais 2025 na ukaja na pendekezo la mwamvuli wa Dr mwinyi, kimsingi umesaidia umma kuuandaa kwako kuwa huenda mama asiwe miongoni mwao..

2)sijajua kama mwandishi(kama nmekulewa vizuri) umepata wapi ushahidi kuwa semaji wa ccm mpya anachukiwa? (A) umezingatia Nini kwenye hoja hii
(B) umeuliza Nan na wapi kujua hlo
(C) makonda anahusianaje na kuwepo au kutokuwepo Kwa mama samia kuwa mgombea urais wa CCM?
(D) utafiti ulioufanya ulizingatia vigezo vipi?
(E) faida za utafiti huo zinainufaishaje jamii ya watz? kwamba rais alikosea au ana plan ipi?

3)badiko lako limekuja kutujulisha kuwa umekuwa mtu wa mwanzo kumwona uliemtaja kuja kuw rais je umetumwa? umeagiZwa? ni maoni? ni utafiti? hisia au maono kama unavyosema kwenye baadhi ya mabandiko yako?

nikushauri Kwa kuwa u mkongwe na kunavijana wanajifunza jiepushe kuingia kwenye kile unachokipenda tukipende wote au unachokichukia tukichukie wote, hata kama ni maoni yazingatie uhuru na mipaka ya hisia na mhemko.

B

Sent using Jamii Forums mobile app
 
p
kwanza nikushukuru Kwa bandiko lako, naomba nitoe maoni yangu kidogo

nikushauri Kwa kuwa u mkongwe na kunavijana wanajifunza jiepushe kuingia kwenye kile unachokipenda tukipende wote au unachokichukia tukichukie wote, hata kama ni maoni yazingatie uhuru na mipaka ya hisia na mhemko.

B
Mkuu Boniphace Bembele Ng'wita , kwanza asante.
Pili, bandiko hili limeanza kwa angalizo, ulilisoma hilo angalizo?, ulilielewa?.
Kwa faida yako na ya wengine
Angalizo kwa Wanabodi na Mode

Bandiko hili ni C&P kutoka kwa mwana JF fulani.
Kwasababu mwandishi ni member wetu humu na humu hajaileta, naomba ikitokea ameileta humu, then futa hili bandiko langu.

Nime C&P kwasababu mimi ni miongoni mwa watu wa mwanzo mwanzo kuandika humu kuwa mgombea urais wa CCM kwa uchaguzi wa 2025 could be Dr. Hussein Mwinyi, kupitia bandiko hili

Mwana if fulani.
C&P by Paskali

P
 
Angalizo kwa Wanabodi na Mode

Bandiko hili ni C&P kutoka kwa mwana JF fulani.
Kwasababu mwandishi ni member wetu humu na humu hajaileta, naomba ikitokea ameileta humu, then futa hili bandiko langu.

Nime C&P kwasababu mimi ni miongoni mwa watu wa mwanzo mwanzo kuandika humu kuwa mgombea urais wa CCM kwa uchaguzi wa 2025 could be Dr. Hussein Mwinyi, kupitia bandiko hili Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Hivyo hoja kama hii inapotolewa na mwajeiefu mwenzetu, mwandamizi kama huyu, hivyo nimejikuta ni muhimu kuisambaza.

Paskali.

(Mwanzo wa kunukuu Barua ya...)

Kwa kiasi kikubwa, siasa za Tanzania zimejikita zaidi kwenye chaguzi, hususan uchaguzi mkuu. Kwamba vyama vya siasa hutumia muda mwingi kujiandaa na chaguzi kiasi kwamba kuna dhana kwamba haviwatumikii wananchi vya kutosha kutokana na hilo.

Lakini lengo kuu la chama chochote cha siasa ni kushika dola. Na katika nchi za kidemokrasia, kushika dola kunawezekana kwa njia moja tu, yaani uchaguzi mkuu. Kwa mantiki hiyo, ni sahihi kwa vyama vya siasa kujipanga vema kwa ajili ya chaguzi.

Na kwa chama tawala, kisipofanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya chaguzi zijazo, nafasi yake kama chama kinachoshika dola inakuwa hatarini.

Ni katika mazingira hayo ndio maana kumekuwa na maongezi mengi kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 japo bado miaka miwili hivi kabla ya uchaguzi huo. Na japo kuna chaguzi za serikali za mitaa mwakani, maongezi mengi ni kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Taarifa za kiintelijensia zinaeleza kwamba kuna jitihada zinafanyika huko Zanzibar kumwezesha Dkt Hussein Mwinyi kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano mwaka 2025.

Si tayari CCM “ina mgombea wake” 2025?
Naam. kwa mujibu wa utaratibu usio rasmi huko CCM, rais aliyepo madarakani anakuwa automatically mgombea pekee wa urais mwaka katika uchaguzi utakaomuingiza awamu ya pili ya urais wake.

Ilikuwa hivyo kwa Mkapa mwaka 2000, Jk 2010 na Magufuli 2020. Na inatarajiwa iwe hivyo kwa Mama Samia 2025.

Hadi wakati makala hii inaandikwa haijafahamika rasmi kwanini kuna mpango huo amba sio tu utapelekea “kuukoroga utaratibu huo usio rasmi wa Rais aliyepo madarakani kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo ili akamilishe ngwe zote mbili” bali pia utakuwa upinzani baina ya wanasiasa wawili kutoka Zanzibar.

Maandalizi yameanza
Taarifa zinaeleza kwamba tangu Zanzibar ijiunge na Tanganyika mwaka 1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna kipindi ambapo upande huo wa Muungano umepokea fedha nyingi kutoka serikali ya Muungano kama kipindi hiki cha utawala wa Mama Samia.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa sehemu ya fedha hizo zimekuwa zikitumiwa na wanamkakati wa mpango huo wa kumwezesha Dkt Mwinyi kuwa mgombea mwaka 2025.

Licha ya ukweli kuwa maandalizi ya uchaguzi wowote hule huhitaji fedha za kutosha, yaaminika kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 utatawaliwa na matumizi makubwa ya fedha hasa kutokana na ukweli kwamba wanasiasa wengi wamepoteza mvuto machoni mwa wananchi na njia pekee ya “kupendeka” ni kumwaga fedha.

Mama Samia anawarahisishia kazi wapinzani wake ikiwa ni pamoja na mwanasiasa huyo wa Zanzibar
Kuna matukio mawili makubwa ambayo yanatarajiwa “kumsumbua” Mama Samia kati ya sasa na uchaguzi mwaka 2025. La kwanza ni suala la mkataba wa bandari ambalo japo “kwa nje ya CCM” linaonekana kama lilikuwa lina mwafaka miongoni mwa wana-CCM, ukweli ni kwamba sio tu lilizua mgawanyiko wakati wa mjadala bali pia limeacha makovu ambayo yanaweza “kukwanguliwa” pindi kampeni za urais zitaposhika kasi.

La pili ni hili la “Mama Samia kujichoma msumari mwenyewe” kwa kumteua Bashite kuwa katika mwenezi wa chama hicho, huku akifahamu fika kuwa kada huyo anachukiwa na wengi ndani na nje ya chama hicho.

Japo Mama Samia anatarajia kuwa Bashite atamsaidia kukabiliana na “wapinzani wake”, nguvu za kada huyo huko nyuma zilitegemea zaidi staili ya uongozi wa kibabe wa marehemu Magufuli, ambayo ni tofauti na satili ya uongozi wa Mama Samia, unless aamue kubadilika.

Hitimisho
Kuna msemo kuwa kwenye siasa, wiki moja ni sawa na uhai mzima (lifetime). Na kwa hakika, kati ya sasa Novemba 2023 hadi Oktoba 2025 ni takriban miaka miwili, na mengi yanaweza kutokea aidha kuimarisha dhamira ya mwanasiasa yeyote mwenye ndoto za kumpiku Mama Samia au urais wa Mama Samia ukaimarika zaidi kiasi kwamba yeyote mwenye ndoto za kum-challenge atakuwa anapoteza muda wake. (mwisho wa kunukuu)

Mwana if fulani.
C&P by Paskali
Huenda ikawa ni good move kwa CCM
 
Back
Top Bottom