Pre GE2025 Kinyang'anyiro cha Urais 2025 kwa tiketi ya CCM: Dkt Mwinyi kuwania Urais wa Muungano?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
M
Mwigulu yuko bize kumhonga pesa Kigogo ampambe kumbe ndio anazidisha watu mashaka.

Eti Mwigulu ni Mr clean, kweli Kigogo ni tapeli la karne.
 
Mi nilisikia Mwinyi alipaswa kuchukua urais bara baada ya JM kumaliza muda wake sasa jamaa ndio hivyo akapendwa zaidi, lakini nahisi mpango bado upo kwani kila siku jamaa ni mgeni rasmi kwenye matukio kibao huku bara
 
Ni muda wa kupumzisha chama chakavu 2025 . Ni kirusi kwa watanzania.
 
Tupewe Tanganyika yetu kwa katiba hatutaki kuongozwa na wazanzibar
Mkuu Sir luta , civic education kuhusu uraia wa JMT bado inahitajika sana!, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili za Tanzania bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Uraia wa JMT ni uraia mmoja tuu, Watanzania wote wakiwemo Wanzanzibari wana haki sawa za kiraia ndani ya JMT!, hakuna Mtanzania bara wala Mzanzibari, kuna mtu mmoja tuu, Mtanzania!. Kauli ya hatutaki kuongozwa na Mzanzibari ni kauli ya kibaguzi!. Baada ya hatutaki kuongozwa na Mzanzibari ikipita itakuja hatutaki kuongozwa na Msukuma, then Mhaya, then Mchagga, ukiisha tenda dhambi ya ubaguzi, inaendelea kukutafuna...
P
 


Leo ni 2023, mambo ya u rais ni 2025, mwandishi mwenye upeo mkubwa wa kiwango chako, anaacha Habari zan uchunguzi kibao...

Paschal katafute ajira hata Kidimbwi..
 
Hayo mawazo yako hatuwezi kuongeza na wazanzibar consecutively haipo pia waisilamu consecutively ww muota ndoto na uchawa wa kutaka vyeo unakusumbua
 
Hii nchi ni kubwa sana na Ina watu wengi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki .
Hii nchi Ina rasilimali nyingi kuliko nchi zote Za Afrika Mashariki. Hii nchi Ina Amani kuliko nchi zote za Afrika Mashariki. Hii inchi ilipata uhuru kwa Amani kuliko nchi zote Za Afrika Mashariki. Hii nchi ni nchi Pekee iliyojengwa na waasisi wake katika Misingi ya Umoja,Ujamaa , mshikamano na utu kuliko nchi zingine nyingi barani Afrika.Hii nchi ni nchi yenye Muungano Wa nchi Mbili na nchi moja kupoteza uhuru wake Kwa manufaa ya Muungano huo.
Hii ni nchi Pekee Kwa Sasa yenye mfumo Wa Kijeshi ndani ya mfumo Wa Kidemokrasia. Watawala wanaoongoza kijeshi lakini Kwa mgongo Wa Demokrasia hivyo kutoa mwanya mkubwa Kwa watawala mamluki Wa Mafisadi ,mabwanyenye na Wakoloni mambo leo kuihujumu nchi Kwa Kasi kubwa sana Huku wakitumia power ya Katika yenye mfumo Wa Kijeshi kuwagandamiza Wananchi Haki ya kuwachagua Wazalendo Wa ukweli kupitia mfumo bandia Wa Kidemokrasia.

Tunataka kuona Mwaka 2025 anachaguliwa Rais mwenye uchungu na Wananchi Wa Tanzania bara na watanzania wote Kwa ujumla . Watanzania bara tumefundishwa Uzalendo Wa kutobaguana Wala kuona Dini zetu ni Bora kuliko Taifa .
Hawa Jamáa nimeshawasoma sana . Kamwe hawajalelewa kwenye mazingira ya kuwaona Watanzania Bara au Watanganyika kama Watu Sawa na wao Katika Imani na Katika Mila na Hata desturi . Wale watu wanaubinfsi unaotokana na malezi na kuwaona watanganyika kama watu wasio na Dini Wala Imani Wala utamaduni mzuri. Wanachanganya utaifa matamanio ya nafsi zao . Wanaongizwa zaidí na nafsi na malezi Yao kuliko Katiba na Sheria za nchi.

Mwinyi , Majaliwa ,Jafo, na Mama wote ni Wa Imani moja lakini SIO wote wanye nafsi zilizo na upendo Wa dhati Kwa Watanzania Kwa ujumla wao yaani Tanganyika na Zanzibar.
Bila kupepesa Uso Kwa uwazi na ukweli na Kwa ajili ya Kesho Bora ya Taifa la Tanzania Nzima na watu Milioni 61 na rasilimali nyingi Kasimu Majaliwa ni Mzalendo na Hana ubaguzi Hata chembe iwe kidini ,kikabila na Hata kitamaduni na pia kisiasa .
Lakini pia Jafo ni Bora mara kumi ya wale watu wasiojali Kesho ya watu Milioni 61 Kwa manufaa ya watu Wachache .
Tunaliua Taifa la baadae Kwa manufaa ya Wachache wasiojali na Wenye mioyo isiyowafurahia Watanzania wote Kwa usawa Wa Imani na tamaduni zao.

Majaliwa na Jafo wachukue Fomu 2025 anyeona anafaa zaidí Naye achukue washindanishwe ndani na nje ya Chama.
Tunataka siasa Bora Kama zile za Marekani.
Watu wanachukua fomu ndani ya chama na kuzunguia nchi Nzima Kuomba uungwaji mkono Huku wakishindanishwa kwenye midahalo mbalimbali.
Haya mambo ya kupitisha majina kimya kimya ni kuruhusu nchi kuwa chini ya kikundi kidogo cha watu Wa familia Moja au Mbili . Na matokeo yake baadae patakua panaibuka matukio ya makundi kuuana Ili linako kundi moja lenye nguvu ya kuweka raisi Wa maslahi yake tuu.
Kama tungekua na Katiba Bora basi hayo mambo ya CCM na kakundi kake kuwalazimsha watu wao kingekua linakikosti chama peke yake lakini Kwa Sasa kosa la CCM linalogharimu Taifa na matokeo yake nchi inakosa dirá na kujikuta tunaletewa watu wale wale walioshindwa au waliofanya makosa makubwa ya kulihujumu Taifa ambapo kimsingi walitakiwa wawe Gerezani . Badala yake wanatumia nguvu ya pesa walizohujumu nchi kuweka mitandao ya kifisadi kuendelea kulindana na kurithishana utawala chini ya mgongo Wa CCM .

CCM ni Lazima isimamie Katiba yake kuwahoji wanaowaletea wagombea kuwa je,Bado wanasimamia Imani ya chama. Imani ya usawa, rushwa ni adui Wa haki, Ujamaa ,Kupinga Unyonyaji n.k. !!

Nchi Mbili haifai Kutawaliwa na Marais Wa wili kutoka nchi moja . Huo ni uvamizi Wa nchi ya Pili.
 
wajiengue tu hakuna Mkubwa nje ya Taasisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…