Kiongozi aliyehujumu na kuua kiwanda cha TIPER ni wa ovyo kuwahi kutokea Tanzania

Mnapoambiwa tunataka katiba mpya kwanini mnakataa?
 
W
Kama hujui undani wa kufa TIPPER nyamaza fanya utafiti.Kwanza mtambo wa Tipper haukuweza kutosheleza mahitaji ya nchi toka ifuguliwe hadi kifo chake cha aibu.It was smallest refinery in the world but also was too old.
Tipper ilikufa kwa hiyo mikataba mibovu,alipotoka Kambarage ma Taliani wakatumia upungufu ulio kwenye mikataba wakachuma pesa nyingi tu,tukikopa kama nchi kukarabati mitambo ya miaka 40,na hiyo pesa inaishia kwao wala haikuja kukarabati TIPPER alioiacha Nyerere.
Benki ya dunia kwa ubora wake akagundua janja ya nyani akajiondoa kufadhili au kukopesha TIPPER. nao mafia Italy walijiondoa wakauza hisa zake kwa kuwa walikuwa ndio wachumia tumbo.Ndio ukawa mwisho TIPPER.
Mtaliani anasimamiwa na nchi au watu makini sio waomba scholarship ya mwanae au kufadhili harusi ya mwanae.
 
Ach uongo, serikali haikutaifisha hicho kiwanda. Nakumbuka wakati ule iliamuliwa kiwanda kifungwe na kigeuzwe kuwa storage facility ya mafuta yaliyosafishwa. Hoja za kifisadi zilitolewa wakati ule kuwa Msumbiji na Afrika Kusini kuna refinery kubwa ambazo zitahudumia mpaka huku kwetu, kulikuwa na malumbano makali wazalendo wakipinga na wahujumu ndani ya serikali na washirika wao nje ya serikali wakishabikia Tipper ifungwe isisafishe mafuta. Hadi wakati kinafungwa kiwanda hicho kilikuwa mali ya ubia kati ya Italia na Tanzania.

Uamuzi wa kukifunga haukuwa wa busara bali uligubikwa na ufisadi na sindicate iliyolenga kuifanya Tanzaniaiwe tegemezi wa mafuta yaliyosafishwa nje ya nchi.
 
Hivi unaelewa ulichoandika ? Hisa za Serikali kampuni ya Agip walizipataje? Hadi wakawa na wakurugenzi wateuliwa na Serikali kuingia bodi ya Agip?
 
Hivi unaelewa ulichoandika ? Hisa za Serikali kampuni ya Agip walizipataje? Hadi wakawa na wakurugenzi wateuliwa na Serikali kuingia bodi ya Agip?
Sijaelewa ulichoandika,

Tipper ilikua kiwanda cha ya ubia kati ya Tanzania na Italia (Tanzania and Italy Petroleum Refinery Ltd) Agip ilikuwa ni i kampuni ya Italia iliyokuwa ikifanya biashara ya mafuta Tanzania ingawa serikali ya Tanzania ilikuwa na hisa mule. Hivi ni vitu viwili kwa uelewa wangu wa wakati ule.
 
Naunga mkono hoja.
Tusimung'unye maneno, Rais Mwinyi ndiye aliyeuza kiwanda cha TIPER.
 
Sisi wabongo ni wababaishaji mno hakuna chochote tunachoweza kuendesha kwa ufanisi. Angalia vitu vingi tu tulivyonavyo lakini uendeshaji wake ni ubabaishaji mtupu; serikali, viwanda, bandari, utalii, chadema, nk
 
TIPER ile ya refinery imekufa na kuzikwa kabisa maana mitambo yte imeshauzwa kama sikilepa...wazeni kujenga matank ya serikali...yaani storage ya serikali
 
Serikali inaweza ikiamua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…