Kiongozi Mkuu wa Hamas, Ismail Haniyeh afariki baada ya kushambuliwa akiwa Iran

Kiongozi Mkuu wa Hamas, Ismail Haniyeh afariki baada ya kushambuliwa akiwa Iran

Huo ni ujumbe wa Israel kwa maadui zake wote popote pale walipo duniani, hata kama ukiwa Tandahimba huwezi kuwa salama.

Hawa Israel tukubali tukatae Mungu amewajalia akili sana kitendo kilichopelekea hata Hitler kuwachukia sana, Dunia inatakiwa ielewe kwenye mishipa ya damu ya wayahudi kunatembea damu ya Albert Einstein hivyo umakini na mikakati hatari waliyokuwa nayo sio vitu vya kubahatisha ni natural gifts.

Hivyo myahudi akitaka kukumaliza huwezi kumkwepa mahala popote, hata Aldof Eichmann mmoja wa mastermind wa Holocaust hakuamin alivyojikuta mikononi mwa Wa-Israel licha ya kukimbilia kujificha vijiji vya ndani ndani huko Argentina 1960.

Kwa yanayotekea hawa jamaa hawabahatishi, Hizi nchi za Yemen, Iran and the likes kama wanataka vita na Israel wafanye risk assessment vizuri mara nyingi watamba wana silaha zinazofika sehemu yeyote ndani ya Israel. Wanasahau kitu kimoja cha muhimu katika medani za kivita kuwa "War is all about mindsent and well organized intelligence".

Unaweza kuwa na silaha zinazofika kila mahala lakini zikawa intercepted zote.

Kitendo cha Israel mmoja kuumiza vichwa nchi karibia zote za mashariki ya kati inabidi wajue Israel ana kitu cha ziada kwenye medani za vita na ushushu ambacho labda wao hawana.
Wafia dini watakuja wakutukane wewe hawawezi kukubaliana na ulichoandika hata kama ni kweli wako na ubishi
 
Marafidhwah (mashia) wanajulikana kwa khiyana katika historia.

Salahuddin (Allah amrehemu) kabla ya kuikomboa Al Quds (Jerusalem) kutoka katika mikono ya crusaders aliwabonda kwanza mashia wa Misri. Hakwenda kuikomboa al Quds kutoka katika mikono ya crusaders huku mgongoni mwake kuna 'Ubaydiyyun (mashia walioitawala Misri).

Kina Khamenei, HezboShaytaan na Houthi sio wa kuwaamini.

Watu wanaomtukana na kumkufurisha Amiri wa Waumini 'Umar na wenzake katika maswahaba (Allah Awaridhie wote) walioikomboa Al Quds mwanzo kabisa kutoka kwa warumi na kuifungua kwa ajili ya Uislam, hawawezi kuikomboa al Quds sasa kama ambavyo hawakuweza kuikomboa ilipochukuliwa tena na crusaders na kuja kukombolewa na Waislam akina Salahuddin. Wao ni watu wakuwafanyia njama na khiyana tu Waislam.

Allah awasamehe na awarehemu ndugu zetu Waislam wote waliouawa katika vita hii. Allah awanusuru ndugu zetu wanyonge na wadhaifu.

View: https://x.com/Osint613/status/1818547931059819001?t=dM2opw0wUb0Qw5hYmCy6LQ&s=19
 
Sio kweli siku kadhaa zilizopita uchina imepokea viongozi wa Hamas Beijing na kufikia maafikiano kadhaa na fatah na viongozi wengine na wala Mossad hawajatekeleza jambo lolote la hatari maeneo ya Beijing kwa kiongozi yoyote.
 
Kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh ameuawa nchini Iran, kundi hilo limesema.

Katika taarifa iliyotolewa leo siku ya Jumatano, Hamas imesema Haniyeh aliuawa kufuatia uvamizi wa Israel kwenye makazi yake mjini Tehran.

Kwa mujibu wa kundi hilo, Haniyeh alifariki baada ya kushiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Iran Masoud Pezeshkian aliyeapishwa siku ya Jumanne.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Irani lilisema chanzo cha "tukio" hakijafahamika mara moja lakini "kinachunguzwa", shirika la habari la AFP liliripoti.

Usicheze na MOSSAD

=========

Ismail Haniyeh alikuwa mmoja wa viongozi wakuu wa Hamas kwa miongo miwili iliyopita, akiongoza shughuli za kisiasa za kundi hilo la kijeshi akiwa uhamishoni nchini Qatar katika miaka ya hivi karibuni.

Jumanne ya tarehe 30 Julai, 2024, Bw. Haniyeh alikuwa Iran na wanachama wengine wakuu wa "mhimili wa upinzani" wa Iran — ambao unajumuisha Hamas huko Gaza, Hezbollah nchini Lebanon na Wahouthi huko Yemen — kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa Iran.

Kama kiongozi wa kisiasa wa Hamas, alikuwa muhimu katika mazungumzo na diplomasia yenye hatari kubwa ya kundi hilo, ikiwemo mazungumzo yaliyokwama ya makubaliano ya kusitisha mapigano na Israel.

Haya ndio tunayojua: Kiongozi wa Hamas huko Gaza

Bw. Haniyeh aliteuliwa kuwa kiongozi wa Hamas huko Gaza mwaka 2006. Mwaka huo, alihudumu kwa muda mfupi kama waziri mkuu wa serikali ya umoja wa Palestina, ambayo ilivunjwa baada ya miezi ya mvutano uliyojumuisha mapigano ya silaha kati ya makundi ya Palestina.

Mwaka 2017, aliteuliwa kuwa kiongozi wa ofisi ya kisiasa ya Hamas wakati ambapo walikuwa wakijaribu kupunguza taswira yao ya umma walipokuwa wakijaribu kushawishi Wapalestina na kimataifa.

Bw. Haniyeh aliongoza Hamas kutoka Qatar na Uturuki katika miaka ya hivi karibuni. Alikuwa miongoni mwa wajumbe wa mazungumzo yanayoendelea kati ya Israel na Hamas, yaliyosimamiwa na Misri, Qatar na Marekani, kumaliza vita vya Gaza kwa kubadilishana na mateka waliotekwa kwenye shambulio lililoongozwa na Hamas dhidi ya Israel.Kupanda kwa Madaraka

Alipozaliwa
Bw. Haniyeh alizaliwa mwaka 1962 katika kambi ya wakimbizi ya Shati kaskazini mwa Jiji la Gaza, kwa wazazi wa Kipalestina ambao mwaka 1948 walihamishwa kutoka nyumbani kwao katika eneo ambalo sasa ni Israel, huko Ashkelon. Alisoma katika shule zinazoendeshwa na shirika kuu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Wapalestina, UNRWA, na kuendelea kusomea fasihi ya Kiarabu katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza.

Alikamatwa na jeshi la Israel na kuhudumia vifungo kadhaa katika magereza ya Israel miaka ya 1980 na 1990.

Kushika madaraka
Kupanda kwake madarakani huko Gaza kulisaidiwa na mshauri wake, kiongozi wa kiroho na mwanzilishi wa Hamas, Sheik Yassin, ambaye alimtumikia kama katibu binafsi. Wawili hao walikuwa malengo ya jaribio la mauaji ya Israel mwaka 2003; mwaka uliofuata, Bw. Yassin aliuawa na jeshi la Israel.

"Haupaswi kulia," Bw. Haniyeh aliwaambia umati uliojitokeza nje ya Hospitali ya Shifa huko Jiji la Gaza wakati huo. "Unapaswa kuwa imara, na unapaswa kuwa tayari kwa kulipiza kisasi."Anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu

Mwezi Mei, mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu alisema atatafuta kibali cha kumkamata Bw. Haniyeh. Mwendesha mashtaka alimshutumu yeye na viongozi wengine wa Hamas kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu kuhusiana na shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israel, ikiwemo "kuteketeza, mauaji, kuteka mateka, ubakaji na unyanyasaji wa kingono katika kizuizi."

Familia yake kuuawa na Israeli
Mwezi Juni, Hamas ilisema kuwa dada wa Bw. Haniyeh na familia yake waliuawa katika shambulio la kijeshi la Israel kwenye nyumba ya familia ya Haniyeh huko Gaza, madai ambayo jeshi halikuthibitisha. Mwezi Aprili, watoto watatu wa kiume wa Bw. Haniyeh kati ya watoto wake 13 waliuawa na vikosi vya Israel katika operesheni nyingine ya kijeshi huko Gaza.

Alikuwa mkaidi mbele ya hasara hiyo, na jambo kuu katika maisha ya Bw. Haniyeh ilikuwa: "Hatutasalimu amri" Bw. Haniyeh alisema wakati huo, akibainisha kuwa tayari alipoteza jamaa kadhaa katika vita hivyo.
Hao ndio wayahudi wanakupiga kwako wanakupiga ugegenini!!

Basi akale sasa bikra 72
 
Gazeti la serikali wamelaumu kuwa kama Israel wameweza kupiga kwenye eneo la jeshi la Iran lenye ulinzi mkali na kumuua kiongozi wa hamas ni fedheha kwa usalama wa nchi na viongozi wao...
Hakuna ndege wala rada iliyoweza kugundua kama kuna hatari ndani ya Iran
Radar na air defence missiles za Russia na Iran combined!
 
Huo ni ujumbe wa Israel kwa maadui zake wote popote pale walipo duniani, hata kama ukiwa Tandahimba huwezi kuwa salama.

Hawa Israel tukubali tukatae Mungu amewajalia akili sana kitendo kilichopelekea hata Hitler kuwachukia sana, Dunia inatakiwa ielewe kwenye mishipa ya damu ya wayahudi kunatembea damu ya Albert Einstein hivyo umakini na mikakati hatari waliyokuwa nayo sio vitu vya kubahatisha ni natural gifts.

Hivyo myahudi akitaka kukumaliza huwezi kumkwepa mahala popote, hata Aldof Eichmann mmoja wa mastermind wa Holocaust hakuamin alivyojikuta mikononi mwa Wa-Israel licha ya kukimbilia kujificha vijiji vya ndani ndani huko Argentina 1960.

Kwa yanayotekea hawa jamaa hawabahatishi, Hizi nchi za Yemen, Iran and the likes kama wanataka vita na Israel wafanye risk assessment vizuri mara nyingi watamba wana silaha zinazofika sehemu yeyote ndani ya Israel. Wanasahau kitu kimoja cha muhimu katika medani za kivita kuwa "War is all about mindsent and well organized intelligence".

Unaweza kuwa na silaha zinazofika kila mahala lakini zikawa intercepted zote.

Kitendo cha Israel mmoja kuumiza vichwa nchi karibia zote za mashariki ya kati inabidi wajue Israel ana kitu cha ziada kwenye medani za vita na ushushu ambacho labda wao hawana.
Ngoja wasaa magauni waje
 
K

Kitu Cha ziada alicho nacho ni Nchi za magharibi tu hakuna kingine
 
In addition to that hii ni msg nzito kwa Iran na washirika wake wamefanya tukio ambalo Iran imebaki uchi. Mbaya kuliko yote Huwa Israel ha confirm kwenye matukio mazito kama haya.
Hawa wanaelawana lugha hawahitaji Myahudi aconfirm publicaly.
 
kwa hyo kumbe wairan hawataki maujinga ya ayatoula ndo maana wanakubali kuwa agents wa mossad..
Mapinduzi ya Ayatolla Khomeiny ya mwaka 1978 yameiharibu Iran. Iran ilikuwa highly developed chini ya Mtawala wa wakati huo aliyeitwa Mohamed Reza Pahlavi huku Khomeiny akiwa uhamishoni Paris. Kuifanya nchi ya Kiislamu kumeirudisha nyuma sana kwa sababu ya vikwazo walivyowekewa na umoja wa mataifa

Ilikuwa nchi yenye uchumi imara, kula bata kuliko Dubai enzi hizo. Ila Ayatollah kaifanya nchi kuwa msìkiti
 
Hii ni hasira ya kushindwa vita huko ghaza kwa style hii ndo wapiganaji wa Hamas watapandisha mzuka wa kufa mtu
Yani kiongozi Namba moja wa Hamas kauawa wewe unakimbilia kudai watu wameshindwa vita. Walipiga sawasawa mnadai wanaua watoto na wanawake, walipiga kiongozi mkuu mnadai ni hasira za kushindwa vita. Hivi unaelewa maana ya kushindwa.
 
Back
Top Bottom