- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Tizama hi video kwa makini kabla ya ku-comment.
Kiongozi wa Korea kasikazini amelegeza mashariti kwa dini moja tu uko nchini kwake baada ya kushuhudia great miracle en Wisdom katika kitabu cha Qur"an tukufu, wakati anaingia madarakani 2011 Uislamu kama dini zingine zilikua marufuku nchini mwake, mwaka 2015 waislamu kwa kujificha ficha walifika 3000 tu kwasasa waislamu ni 30,000.
Adhana ya kila swala kwa kutumia vipaza sauti misikitini imeruhusiwa katika hiyo nchi kali ya kicommunist kuna hofu kubwa kwamba Uislamu ndani ya miaka 10 watagawana hiyo nchi na wa Buddha.
Kiongozi wa Korea kasikazini amelegeza mashariti kwa dini moja tu uko nchini kwake baada ya kushuhudia great miracle en Wisdom katika kitabu cha Qur"an tukufu, wakati anaingia madarakani 2011 Uislamu kama dini zingine zilikua marufuku nchini mwake, mwaka 2015 waislamu kwa kujificha ficha walifika 3000 tu kwasasa waislamu ni 30,000.
Adhana ya kila swala kwa kutumia vipaza sauti misikitini imeruhusiwa katika hiyo nchi kali ya kicommunist kuna hofu kubwa kwamba Uislamu ndani ya miaka 10 watagawana hiyo nchi na wa Buddha.
- Tunachokijua
- Kim Jong Un ni kiongozi wa Korea Kaskazini tangu 2011, alipochukua nafasi ya baba yake, Kim Jong Il. Utawala wake unazingatia itikadi ya Juche, falsafa inayosisitiza kujitegemea, ingawa kwa hali halisi inatumiwa kudumisha mfumo wa udikteta wa chama kimoja. Serikali yake inadhibiti karibu kila sekta ya maisha ya wananchi, ikiwemo dini, na kuifanya Korea Kaskazini kuwa moja ya mataifa yanayokiuka sana uhuru wa kuabudu.
Tangu Desemba 2, 2024 kumeibuka Taarifa inayodai kiongozi huyo Kim Jong Un ameamua kubadii dini na kuwa Muislam. Taarifa hii iliyoletwa na MwanaJamiiCheck inamuonesha Kim akiwa ameshika Msahafu huku kukiwa na ujumbe unaoarifu kiongozi huyo kusilimu. Uchunguzi wa JamiiCheck umebaini taarifa hiyo kutokea Mtandao wa YouTube (hapa na hapa), Mtandao wa TikTok (Tazama hapa), kwenye tovuti za watu binafsi (Tazama hapa). Aidha, JamiiCheck imebaini kuwa madai kama haya yameshawahi kujitokeza mwaka mmoja uliopita (Mwaka 2023) (Tazama hapa na hapa).
Baadhi ya Post za TikTok zinazoelezea Kim Jong Un kusilimu
Upi uhalisia wa Madai hayo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa madai ya Kim Jong Un kubadili dini na kuwa Muislamu yameenea hasa kupitia YouTube, katika akaunti za watu binafsi. (Tazama hapa na hapa)
Hata hivyo, hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa sauti au video unaothibitisha madai haya. Zaidi ya hayo, ufuatiliaji wetu katika vyanzo vya kimataifa umeonyesha kuwa hakuna ripoti rasmi au chanzo kinachoaminika kilichoripoti madai hayo.
Kwa kuzingatia historia ya Korea Kaskazini na msimamo wa serikali yake dhidi ya dini, madai haya yanaonekana kuwa ya kubuniwa. Viongozi wa taifa hilo mara nyingi hujihusisha na itikadi ya Juche, ambayo inapinga kufuata dini yoyote rasmi. Ikiwa madai haya yangekuwa ya kweli, ni dhahiri kwamba yangekuwa habari kubwa katika vyombo vya habari vya kimataifa, lakini hilo halijatokea.
Nafasi ya Uislamu na Ukristo Korea Kaskazini
Ukristo unachukuliwa kama tishio kubwa zaidi kwa serikali ya Korea Kaskazini, hasa kutokana na historia yake ya kuhusishwa na mataifa ya Magharibi. Wakristo wanaoshiriki ibada za siri hukabiliwa na mateso makali, kukamatwa, na mara nyingine kupelekwa katika kambi za kazi. (Tazama hapa na hapa)
Ingawa kuna taarifa chache kuhusu Waislamu nchini Korea Kaskazini, dini yoyote isiyoidhinishwa na serikali, ikiwemo Uislamu, inadhibitiwa vikali. Serikali huona imani za kidini kama tishio kwa itikadi rasmi na utii wa wananchi kwa kiongozi wa taifa. (Tazama hapa)