SI KWELI Kiongozi Mkuu wa North Korea asilimu kuwa Muislam

SI KWELI Kiongozi Mkuu wa North Korea asilimu kuwa Muislam

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Tizama hi video kwa makini kabla ya ku-comment.

Kiongozi wa Korea kasikazini amelegeza mashariti kwa dini moja tu uko nchini kwake baada ya kushuhudia great miracle en Wisdom katika kitabu cha Qur"an tukufu, wakati anaingia madarakani 2011 Uislamu kama dini zingine zilikua marufuku nchini mwake, mwaka 2015 waislamu kwa kujificha ficha walifika 3000 tu kwasasa waislamu ni 30,000.

Adhana ya kila swala kwa kutumia vipaza sauti misikitini imeruhusiwa katika hiyo nchi kali ya kicommunist kuna hofu kubwa kwamba Uislamu ndani ya miaka 10 watagawana hiyo nchi na wa Buddha.

kimu.png
 
Tunachokijua
Kim Jong Un ni kiongozi wa Korea Kaskazini tangu 2011, alipochukua nafasi ya baba yake, Kim Jong Il. Utawala wake unazingatia itikadi ya Juche, falsafa inayosisitiza kujitegemea, ingawa kwa hali halisi inatumiwa kudumisha mfumo wa udikteta wa chama kimoja. Serikali yake inadhibiti karibu kila sekta ya maisha ya wananchi, ikiwemo dini, na kuifanya Korea Kaskazini kuwa moja ya mataifa yanayokiuka sana uhuru wa kuabudu.

Tangu Desemba 2, 2024 kumeibuka Taarifa inayodai kiongozi huyo Kim Jong Un ameamua kubadii dini na kuwa Muislam. Taarifa hii iliyoletwa na MwanaJamiiCheck inamuonesha Kim akiwa ameshika Msahafu huku kukiwa na ujumbe unaoarifu kiongozi huyo kusilimu. Uchunguzi wa JamiiCheck umebaini taarifa hiyo kutokea Mtandao wa YouTube (hapa na hapa), Mtandao wa TikTok (Tazama hapa), kwenye tovuti za watu binafsi (Tazama hapa). Aidha, JamiiCheck imebaini kuwa madai kama haya yameshawahi kujitokeza mwaka mmoja uliopita (Mwaka 2023) (Tazama hapa na hapa).

1733642513679-png.3171923

Baadhi ya Post za TikTok zinazoelezea Kim Jong Un kusilimu

Upi uhalisia wa Madai hayo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa madai ya Kim Jong Un kubadili dini na kuwa Muislamu yameenea hasa kupitia YouTube, katika akaunti za watu binafsi. (Tazama hapa na hapa)

Hata hivyo, hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa sauti au video unaothibitisha madai haya. Zaidi ya hayo, ufuatiliaji wetu katika vyanzo vya kimataifa umeonyesha kuwa hakuna ripoti rasmi au chanzo kinachoaminika kilichoripoti madai hayo.

Kwa kuzingatia historia ya Korea Kaskazini na msimamo wa serikali yake dhidi ya dini, madai haya yanaonekana kuwa ya kubuniwa. Viongozi wa taifa hilo mara nyingi hujihusisha na itikadi ya Juche, ambayo inapinga kufuata dini yoyote rasmi. Ikiwa madai haya yangekuwa ya kweli, ni dhahiri kwamba yangekuwa habari kubwa katika vyombo vya habari vya kimataifa, lakini hilo halijatokea.

Nafasi ya Uislamu na Ukristo Korea Kaskazini
Ukristo unachukuliwa kama tishio kubwa zaidi kwa serikali ya Korea Kaskazini, hasa kutokana na historia yake ya kuhusishwa na mataifa ya Magharibi. Wakristo wanaoshiriki ibada za siri hukabiliwa na mateso makali, kukamatwa, na mara nyingine kupelekwa katika kambi za kazi. (Tazama hapa na hapa)

Ingawa kuna taarifa chache kuhusu Waislamu nchini Korea Kaskazini, dini yoyote isiyoidhinishwa na serikali, ikiwemo Uislamu, inadhibitiwa vikali. Serikali huona imani za kidini kama tishio kwa itikadi rasmi na utii wa wananchi kwa kiongozi wa taifa. (Tazama hapa)
Masikini mnahangaika sana kueneza dini yenu kwa mabavu na propaganda ila kwa bahati mbaya dunia ya leo vinazaliwa vizazi ambavyo vinajua kuhoji na vinatumia akili kuliko hisia, ndio maana mnaona watu wengi siku hizi wanaanza kuachana na hizi dini na huko tunakoelea dini zinazidi kufubaa kwahiyo hata ikitokea uislam ukaenea dunia nzima, hautakuwa ule wa itikadi kali kama sasa hivi wengi watakuwa waislam kwa majina tu ila hawata practice uislam ipasavyo hivyo hautakuwa na impact yoyote

Wakristo mkishaikatia tamaa dini yenu utasikia "hizi dini this, hizi dini that" kujipa moyo. Sisi tunamshukuru Allah kwa neema ya Uislam. Na Uislam ndio mfumo wa maisha ulio juu ya mifumo yote ya maisha, sio ukristo, sio uyahudi, sio uhindu, sio ubudha, sio u "atheism", sio jainism, sio Confucianism, sio Taoism, sio u feminist, sio ukomunisti, sio demokrasia wala mifumo mengine ya maisha. Uislam uko juu ya mifumo yote mengine ya maisha.

Wala hakuna haja ya propaganda ili kuueneza Uislam. Uislam ndio haki.

Namuomba Allah anifishe katika Uislam.
 
Mkuu nchi za kikuristo ni zipi hizo? au unamanisha za kishogaa?
We ni choko? Naona unapenda kuzungumzia habari za machoko hata kwenye mada zisizowahusu! Umetajiwa nchi za Kikristo zinazotawala Dunia, nawe taja za Kiislam kama zipo na zinatawala kwatika nyanja zipi?
Mijinga kama wewe ndo inayopokea tamaduni za watu kwa mgongo wa dini na kuzivaa zaidi hata ya hao waliozileta. Hapo ukute umesugua komwe mpaka limeota sugu (wenyewe mnaita sijda) ila waliokuletea dini (Waarabu) hawana huo upuuzi, wanaswali kwenye mazingira mazuri yasiyo athiri maungo yao.
 
Kwani wewe unatumia kigezo gani , kubagua wengine kwenye ukuristo, wakwangu sio kama wa kwako mramba msalamba na anae abudu sanamu, mimi namtambua Yesu kama nabii wa Mungu kama nabbi wengine, naamini kitabu chake alicho pewa Injili, na heshimu mama ake kama mwanamke mtakatifu ambae hajawahi kuzini kabisa nk.
Nilichokiandika nakijua,hakuna Mkristo mwenye maandishi uliyoandika hapa zaidi sana hakuna Mkristo duniani anayeamini ujinga ulioandika hapo juu.
 
Nilichokiandika nakijua,hakuna Mkristo mwenye maandishi uliyoandika hapa zaidi sana hakuna Mkristo duniani anayeamini ujinga ulioandika hapo juu.
Kwani kuna tofauti gani baina ya Usilamu na ukuristo ulio huru?.........naomba nikupe somo leo watu wote duniani walikua waislamu isipo kua baadhi viongozi wao walichakachua vitabu vyao nakuingiza mambo yao wengine walikata Mtume wa Mungu wa mwisho nakumtukana ndo hao tunao waita wa kuristo wa siku hizi makuffaru.
 
Hii dini inafanya propaganda za kijinga za kuieneza kama wafanyavyo watu wanaouza bidhaa zilizopitwa na wakati au zisizo na ubora
 
Kwani kuna tofauti gani baina ya Usilamu na ukuristo ulio huru?.........naomba nikupe somo leo watu wote duniani walikua waislamu isipo kua baadhi viongozi wao walichakachua vitabu vyao nakuingiza mambo yao wengine walikata Mtume wa Mungu wa mwisho nakumtukana ndo hao tunao waita wa kuristo wa siku hizi makuffaru.
Bwahahah wewe nikuache!!!

Naona unatafuta appetite ya biriani la buku 3 kwangu.
 
Masikini mnahangaika sana kueneza dini yenu kwa mabavu na propaganda ila kwa bahati mbaya dunia ya leo vinazaliwa vizazi ambavyo vinajua kuhoji na vinatumia akili kuliko hisia, ndio maana mnaona watu wengi siku hizi wanaanza kuachana na hizi dini na huko tunakoelea dini zinazidi kufubaa kwahiyo hata ikitokea uislam ukaenea dunia nzima, hautakuwa ule wa itikadi kali kama sasa hivi wengi watakuwa waislam kwa majina tu ila hawata practice uislam ipasavyo hivyo hautakuwa na impact yoyote
Inashangaza
 
Kwani waislamu sio watanzania kwamini wakimbilia nchi nyingine wakati ni jukumu lao kuakikisha kwamba nchi yao Tanzania pia inakua ya kiislamu kwa 100% nani asio taka pepo ya Allah.
Kwenda zako huko kaa na imani yenu ya kibabe
 
Tizama hi video kwa makini kabla ya ku-comment.

Kiongozi wa Korea kasikazini amelegeza mashariti kwa dini moja tu uko nchini kwake baada ya kushuhudia great miracle en Wisdom katika kitabu cha Qur"an tukufu, wakati anaingia madarakani 2011 Uislamu kama dini zingine zilikua marufuku nchini mwake, mwaka 2015 waislamu kwa kujificha ficha walifika 3000 tu kwasasa waislamu ni 30,000.

Adhana ya kila swala kwa kutumia vipaza sauti misikitini imeruhusiwa katika hiyo nchi kali ya kicommunist kuna hofu kubwa kwamba Uislamu ndani ya miaka 10 watagawana hiyo nchi na wa Buddha.

Bullshit.
 
Hata ikiwa ni kweli amekuwa Muislamu siamini kama anaweza kuishi katika misingi ya dini hasa katika kuhakikisha haki imetamalaki ndani ya nchi yake pia nasikia ni mlevi sana kitu ambacho dini hairuhusu.
 
Huyo anatapatapa tu maana siku zake zinahesabika. Mungu anaenda kuingilia kati utawala wa Korea Kaskazini na Uamsho mkubwa utatokea na Wakorea kumjua Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wao. Hivyo hivyo kwa nchi za kiislamu. Mungu hana upendeleo. Watu waliodanganywa kwa muda mrefu na Ukomunist na Uislamu wanakwenda kuona Nuru Kuu!
 
Hata ikiwa ni kweli amekuwa Muislamu siamini kama anaweza kuishi katika misingi ya dini hasa katika kuhakikisha haki imetamalaki ndani ya nchi yake pia nasikia ni mlevi sana kitu ambacho dini hairuhusu.
Imani ya Dini hubadili tabia za watu anaweza kuacha hizo tabia zote na akawa muumini mzuri sanaa.
 
View attachment 3169529

Wakuu katika pitapita kwenye mitandao ya kijamii nimekutana na hii taarifa inayodai kuwa Kiongozi Mkuu wa North Korea, Kim Jong Un amesilimu na kuwa Muislam. Ni jambo zuri sana kwake, na naamini hii itapelekea wakorea wengi kuhamia dini hiyo.

SubhanAllah, MashaAllah, Alhamdolillah
Mkuu be careful na hasa picha maana video hiyo ni muunganiko wa picha si video ambayo unaona kashika Quran, siku hizi ni rahisi generate picha.
Mfano hii ni picha niliyoigenerate kwa sekunde 15 kwa kutumia AI ningeweza kuiphotoshop kwa kutumia picha yake mwenyewe ila nilitaka tu kukuonyesha mfano. Covax
img-xI1rmBKgHaIq5BvBsrR7T.jpeg
 
Tizama hi video kwa makini kabla ya ku-comment.

Kiongozi wa Korea kasikazini amelegeza mashariti kwa dini moja tu uko nchini kwake baada ya kushuhudia great miracle en Wisdom katika kitabu cha Qur"an tukufu, wakati anaingia madarakani 2011 Uislamu kama dini zingine zilikua marufuku nchini mwake, mwaka 2015 waislamu kwa kujificha ficha walifika 3000 tu kwasasa waislamu ni 30,000.

Adhana ya kila swala kwa kutumia vipaza sauti misikitini imeruhusiwa katika hiyo nchi kali ya kicommunist kuna hofu kubwa kwamba Uislamu ndani ya miaka 10 watagawana hiyo nchi na wa Buddha.

Habari mbaya sana kwa kobazi na kanzu. Takbirrrr
 
Back
Top Bottom