Huyo Magu ndio kituvo cha huu uovu unaoendelea leo hii.
Acheni kujidhalilisha kwamba vichwa vyenu havina muunganiko na macho.
1. Umesahau namna gani Magu alivyoipangua hii kesi kwa kuwa alipowaambia wampelekee ushahidi wakawa hawana na wamekuja kukiibua baada ya yeye kulala?
2. Kama Magu ndiye ibilisi wako, sasa hayupo, ni Magu huyo aliyekataa kuibariki hii kesi ndiye anayewapa amuri mahakama wafanye wanayofanya?
3. Kama hawa waliopo kwako ni malaika, na wameweza kubadili mambo mengi ya Magu likiwemo la mikataba ya wachina, n.k, kwa nini hili kama wanajua ni ovu, wanaliendeleza kama shutuma zako kwa marehemu ni za kweli?
4. Acheni kujiondoa ufahamu hadi watu wawadharau kwamba hamwezi kufanya mambo kwa ufahamu.
5. Wakati anauawa Mwangosi kwa kupigwa bomu makusudi tena mchana kweupe pale Nyororo, na kisha waandishi wa habari kuanza kufukuzwa kwenye mashamba ya mahindi wakitakiwa wanyang'anywe kamera zao ili picha zile zisitoke, na baadaye wakasema "CHaDEMA wamemuua mwandishi wa habari kwa kumpiga bomu", na baadaye picha zikarushwa chapu chapu zikionyesha anauawa kwa bomu na askari wa polisi wakiwa wamemzunguka wanampiga na rungu kama nyoka, mwangosi anag'ang'ania miguu ya RPC, ambeya hata hivo hakuweza kumwokoa na mtutu wa bomu, utumbo wake ukatawanywa hadharani, na kesi ilivyoendeshwa kkisanii kila mtu akiona, na hukumu iliyotoka , ili kuwa ni enzi ya Magufuli?
6. Wakati Dr. Ulimboka anatekwa na watu wasiojulikana, wakamg'oa meno na kucha bila ganzi kisha kumtumpa Mabwepande, wakidhani kafa, ilikuwa ni siku za Magufuli?
7. Wakati watu wasiojulikana walilpokuwa wanazingira nyumba za viongozi wa CUF zanzibar, wakiwa na magari yanayojulikana, wanawachukua kwa nguvu, na kuwapoteza, ama kuwatupa wakidhani wameshakufa, ilikuwa ni enzi ya Magufuli?
8. Ikiwa Magufuli, ameanza utawala kayakuta haya mambo yakifanyika tena kwa viburi na dharau, ameasisi vipi?
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Lawama kwa waliokufa ambazo si za kweli zinawaletea laana na kuwaweka mbali na Mungu mwenye Kweli na Uweza wote. Kama huna hakika ya jambo, au huna sababu ya kusema, nyamaza. Kumchafua mtu kwa kumsingizia uwongo kunawatengenezea mambo magumu sana safarin mwenu. Wananchi watawadharau kwamba hamna uelewa na ama ni wadanganyifu mnaendeshwa kwa mihemuko na chuki na hivoy vivyo hivyo hamwezi kutenda haki. Ama uelewa wenu hautoshi.
Tafadhari sana lindeni hekima ya Mbowe.