IKUNGURU IJIRU CHUKU
JF-Expert Member
- Feb 27, 2021
- 484
- 545
Nyama na mchicha zote ni mboga, tofauti yao ni utamu na gharama! Nyama iko juu ya mchicha!
Cha kushangaza vyote vikioza nyama inanuka na kutia kinyaa sana kuliko mchicha.
Maana yake ni kwamba vitu vyenye thamani vikioza vinanuka kuliko vitu visivyokuwa na thamani, kosa la kiongozi linanuka kuliko kosa la anayeongozwa hata kama wote wamefanya kosa moja!
Tunapokuwa viongozi tuwe makini katika kusema, kuvaa, kutembea, kula, kutenda na kuishi.
Ukiwa kiongozi hata ukapenga kamasi kwa mikono ni nongwa. Hata kunywea maji kwenye lichupa kubwa la maji bila glass ni nongwa!
Ndiyo maana kuna miongozo ya viongozi, kama huijui uliza usionekane kituko. Unaalikwa ikulu unaenda umevaa tai ya zambarau, unaenda kufanya mapenzi na nani?
Unakutana na kiongozi unatoa mkono kumsalimia, utapigwa! Subiri yeye ndio aanze. Hii inaitwa handshaking protocal!