Kiongozi wa dini usihubiri amani ya kisiasa bali hubiri amani ya Mungu

umeshindwa kuelewa sentensi ndogo kabisa.
Basi elewa hivi.
Unaweza kuwa na amani ya kisiasa alafu usiwe na amani ya Mungu. Amani ya Mungu inakuwa moyoni. Amani ya Kisiasa inaleta tu utulivu ndani ya nchi lakini sio mioyoni mwa watu,
 
Hakuna kitu kinachoitwa AMANI YA KISIASA. AMANI NI AMANI TU. Lakini AMANI hiyo hutegemea mazingira ambayo mwanadamu yupo.

Shule inaweza kuwa na amani kwa sababu wanafunzi na walimu wao wana amani, na amani hiyo inakuwa ni tunda la yale yanayofanyika kwenye mazingira yao ya shule - inaweza kuwa ni usawa katika huduma, kusikilizwa na kushirikishwa, n.k.

Dini au dhehebu linaweza kuwa na amani kutokana na amani waliyo nayo waumini. Amani hiyo itakuwa ni tunda la namna wanavyotendewa kama vile viongozi wao wa kiimani kuwatendea haki, serikali kuwapa haki yao ya kuabudu, n.k.

Mwananchi, anaweza kuwa na amani katika moyo wake kutokana na anavyopata haki zake zote kama vile fursa za kiuchumi, haki zake za kuabudu, haki za kisiasa, haki zake za kijamii, n.k. Mwanadamu huyu akipata haki zake zote au hata kwa kiwango kikubwa, anakuwa na amani moyoni mwake, amani inayokuwemo mioyoni mwa raia husababisha amani ya Taifa.

Tunaposema nchi yetu ina amani ina maana wananchi wana amani katika mioyo yao. Ile amani ya wananchi katika mioyo yao huchangia utulivu katika Taifa. Amani ni matokeo ya kuridhika na yale yanayokuzunguka. Kama umetenda uovu au kutendewa uovu, huwezi kuwa na amani.

Kwa mtizamo wa kiimani, kama umetenda dhambi, huwezi kuwa na amani. Lakini dhambi ni nini? Dhambi ni matendo yote yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu. Na matendo hayo yapo katika makundi matatu:

1) Maneno - tunanena nini? Kama unatoa kauli za uwongo, ufitini, ubaguzi, matusi, bila ya kujali ni kwa mtazamo wa kisiasa au kijamii, umetenda dhambi.

2) Matendo - ubaguzi, wizi, mapigano, kuwanyima watu haki za aina yoyote wanazostahili, ni dhambi. Na hii inategemea na nafasi yako katika jamii. Kama wewe ni kiongozi lakini unawabagua watu kwa misingi ya aina yoyote ile, hiyo ni dhambi.

3) Kushindwa kutimiza wajibu - wajibu wetu wa kwanza kumpenda Mungu na binadamu wenzetu. Kama ndugu yako anaonewa, anauawa, anateswa, na wewe upo tu umekenua meno au kutofanya chochote kuzuia matendo ya namna hiyo, ni dhambi. Kama wewe unakubali kushiriki kudhulumu ushindi wa mtu au kura zake, ni dhambi, na kiongozi wa dini ni lazima akemee, tena kwa ukali. Maana kazi mojawapo ya kiongozi wa dini ni kuwapa watu amani, na huwezi kulifanikisha hilo kama hakuna haki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ufafanuzi mzuri ndugu ubarikiwe
 
Naomba rejea hapa.
 
Ukitii sheria za nchi na uongozi husika unapata amani ya kusiasa ila ukitii sheria za mungu unapata amani ya Mungu, mfano ukimsifu nakumtii jiwe unakua na amani hapa nchini ila amani ya Mungu bado
Kuna namna yoyote unaweza kutenganisha amani ya siasa na amani ya dini?
 
[emoji110] naunga mkono hoja, hata kibiblia mbona wameonyesha manabii na watumishi wengi wakikemea mambo ya siasa kwa sababu maovu ya siasa nayo ni chukizo mbele za Mungu kama yalivy mambo mengine kama uzinzi
 
Usiwe unarukia kujibu,huna maarifa ya kutosha kujibu hapa.
kivipi tena ningekua sina maarifa ningeandika huo uzii. Hebu jaribu kufuatilia nyuzi zangu ujipime kama waweza kujilinganisha na mimi
 
Imebaki raha ya sabato kwa watu kwa wale washikao amri ya Mungu na imani ya Yesu
 
kivipi tena ningekua sina maarifa ningeandika huo uzii. Hebu jaribu kufuatilia nyuzi zangu ujipime kama waweza kujilinganisha na mimi
Hili moja tu linatosha kujua kuwa hutumii maarifa wala ufahamu kujibu ila unalojua Ni kudandia hoja pole sana hata maandiko yanasema mnaangamia kwa kukosa maarifa, kama hivi
 
Vipi akimsi
Vipi akimsifia Magufuli?
 
Binafsi huwa nakerwa sana na hawa wanaojiita 'viongozi wa dini' kutokujua wanachotakiwa kuhubri!
hamtakiwi kuhubiri AMANI hata kidogo, hubirini HAKI.
Hakuna amani popote kama hakuna haki! msikimbie wajibu wenu kuweni kama mashujaa akina Bagoza na Sheikh Ponda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…