Kiongozi wa kiroho kujihusisha na biashara au siasa

john achila mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
142
Reaction score
281
Kiongozi wa kiroho kujihusisha na biashara au siasa
Nianze kwa kuuliza swali: je ni sahihi kwa kiongozi wa kiroho, kwa mfano mchungaji, kuwa mfanya biashara, au kugombea nafasi za kiserikali au za siasa? Kabla ya kuangalia kiongozi wa dini, hebu tuangalie kwanza kwa mtu aliyeamini. Je mtu aliyeamini, kugombea nafasi za kiutawala ni kosa?

Kugombea nafasi ya kiutawala, biblia haijaeleza moja kwa moja kuwa ni kosa au si kosa, inategemea nia ya huyo mtu. Ikiwa ataenda kule ili kutetea haki za mwanadamu, huku akitembea katika misingi ya imani, hakuna kosa kwa yeye kufanya hivyo.

Isipokuwa, tukumbuke Mathayo 6:24, anasema: Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. Hapo, Yesu mwenyewe alikuwa anazungumzia muingiliano wa kazi (conflict of interest).

Kwenye maandiko, kuna kumbukumbu ya watu wa Mungu waliokuwa na vyeo katika nafasi kiserikali, lakini waliweza kuhifadhi misingi ya imani zao. Mfano mmoja ni Yusufu mwana ya Yakobo, ambaye alikuwa Waziri Mkuu Misri.

Pia, Danieli alikuwa na imani kali ya Mungu, lakini alihudumu kwenye makao ya Mfalme Nebukadneza, na baadaye tena kwenye makao ya Mfalme Belshaza aliyekuwa akitawala Babiloni.

Hivyo, Yusufu na Danieli walikuwa na vyeo serikalini, lakini waliweza kutembea na Mungu, na hatimaye wakapendwa sana.

Mfano mwingine katika historia ni wa mkristo mmoja maarufu aliyeitwa William Wilberforce. Alizaliwa mwaka 1759. Alipokuwa mtu mzima aligombea ubunge huko Ulaya, akapata. Lengo lake lilikuwa ni kuomba sheria ya biashara ya watumwa ifutwe Ulaya. Japokuwa shitaka lake lilipingwa na kupuuzwa kwa miaka mingi, lakini aliendelea kulipigania bila kuchoka hadi mwisho wake sheria ilikuja kupitishwa. Hivyo, kutokana na yeye, biashara ya utumwa ilifutwa kule Ulaya katika karne ya 18.

Hivyo, ikiwa mkristo atajiunga kwa madhumuni ya utetezi kama huo, siyo kosa.

Lakini, kwa kiongozi wa kiroho, hadi aitwe kiongozi
, maana yake wapo watu chini anaowachunga, ambao Bwana amempa awaangalie, na siku ya mwisho atatolea hesabu kwa ajili yao.
Ikiwa ni hivyo, mtu kama huyu kujihusisha na nafasi serikalini, au ya siasa, au kuwa mfanya-biashara ni makosa.

Ikumbukwe kuwa Bwana Yesu alitoa mipaka juu ya utumishi wake. Akasema mtu hawezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Aidha atampenda huyu na kumchukia yule.
Hiyo ipo kwenye Mathayo 6:24: Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

Tuangalie mfano wa Mtume Paulo. Huyu alikuwa fundi wa kushona mahema.
Kiongozi au mchungaji wa kidini (ikiwa ni lazima) anaweza akawa na shughuli yake ndogo ya pembeni ya kumsaidia kupata kipato, ili tu aweze kujitimizia mahitaji yake ya msingi. Hawa ndio mfano wa alivyofanya mtume Paulo, alipokwenda kushona mahema (Matendo 18:3). Lakini siyo kwa lengo la kuwa mfanya biashara wa mahema na wakati huo huo utume. Paulo alifanya vile ili kumudu tu mahitaji yake ya msingi, tukizingatia pia kuwa Paulo alikuwa anasafiri sana.

Ni tofauti na inavyochukuliwa na watu leo, kuwa “alishikilia mambo yote”. Tukumbuke kuwa Mtume Paulo alimwambia Timotheo maneno haya: Timotheo 2:4: Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari".
Bila shaka tunaona kuwa hakuna mlango wa kujihusisha na mambo mengine.

Katika kipindi kile baada ya Bwana Yesu kufufuka, Petro alijaribu kurudia kazi yake ya uvuvi. Alipohangaika usiku kucha na kukosa, asubuhi yake alipokutana na Yesu, swali la kwanza aliloulizwa na Yesu ni Je! Petro unanipenda? Swali hilo aliulizwa mara tatu. Akajibu ndiyo. Yesu akamwambia, basi lisha kondoo zangu. Yesu alikuwa na maana kuwa Petro atoe akili zake kwenye uvuvi, afanye kazi ya utume alioitiwa. Baada ya hapo hatuoni mahali popote Petro, akivua huku anafanya utume (Yohana 21). Na hata kama ilitokea basi haikuwa kwa lengo la kuwa mfanya-biashara, bali kupata riziki ya siku.

Ukishakuwa kiongozi wa kiroho, tambua kuwa wewe hujatengenezwa kwa utumishi wa mambo mengine, bali kumtumikia Mungu tu. Kazi uliyonayo ni kubwa zaidi ya zote ulimwenguni, na bado ina watenda kazi wachache, Bwana Yesu alisema.

Hii ni kazi inayoweza kukufanya uwe na mambo ya kufanya wakati wote. Hivyo, hupaswi kuwa mkuu wa mkoa, wakati huo huo ni mchungaji, au kuwa mbunge au waziri, wakati huo huo ni askofu. Utakwama mahali fulani, katika upande mmoja wapo.

Pia, ni muhimu kufahamu kuwa huduma ya Kristo haipaswi kuhusishwa na utafutaji fedha ndani yake, bali ni kazi ya wito ambayo malipo yake hasa yapo mbinguni.

Bwana akikubariki, au asipokubariki, hilo halikufanyi uache huduma na kuwekeza akili yako kwingineko. Kumbuka tu kuwa Bwana aliahidi hatakuacha, wala kukupungukia kabisa.

Hivyo, kazi ya huduma ya kiroho ni kazi inayojitegemea yenyewe. Ni kazi kubwa zaidi ya zote ulimwenguni, na bado inawatenda kazi wachache. Ni kazi ya uwakilishi wa Mungu duniani.

Kama ni lazima sana kwa kiongozi wa kidini kujihusisha na biashara, iwe ni kwa lengo la kupata fedha kidogo za kujikimu tu, lakini siyo kuwa mfanya biashara kamili. Maadili ya kazi ya kiroho hayakubali.

Aidha, kama kiongozi wa kiroho (kidini) anataka kujihusisha na kazi za serikali au siasa, bado kanuni na maadili ni yale yale; hayakubali.

Isipokuwa, endapo kujihusisha kwake kwenye siasa kuna lengo mahsusi la huduma ya kiroho, kwa mfano, kutetea haki ya watoto, au haki za binadamu, hiyo inaweza kuwa sahihi
, kwani Yesu mwenywe katika Marko 10:14-15, alisema:
14 Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. 15 Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa.

Kwa ujumla, Neno lililosemwa kwenye kitabu cha Mathayo 6:24, ndilo la msingi: Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali kwa wakati mmoja. Kunakuwa na muingiliano wa kazi (yaani conflict of interest)

Ni vizuri kiongozi wa kiroho ajikite katika kuimarisha huduma za kiroho, kwani mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache (Luka 10:2).
 
Muhamad alikua kiongozi wa dini, vita, mfanyabiashara
 
Back
Top Bottom