Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana



hujitambui
 
Jamani mi ndo naingia jamii forum kwa mara ya kwanza na ninasikitika sana kwa hali hii ya mgomo wa madaktari. swali kubwa kichwani mnifungue macho, Dr. anayeanza kazi analipwa shs ngapi? naomba msaada wenu ili nami nichangie objectively.
 

...ni kweli jamani,shemeji yangu yupo hapa muhimbili,ulimboka ameshambuliwa vibaya
 
Kwa nini tusiamin kwamba serikali ya ccm inahusika moja kwa moja na move hii ya kutekwa kwa dr Ulimboka
Njia hii ya kutatua migogoro ni ya kifedhuli na haikubaliki sasa nawashauri madaktari kama dr Ulimboka atakufa wao wasiendelee na mgomo bali waache kazi kabisa kwa hata wao hawatakuwa katika mikono salama kwani washajenga uadui na serikali
 
Zanta hili swala liache kama lilivyo.....nimeshwambia ndugu yangu we soma na kufatilia mjadala usijifanye unajua kila kitu....
Sasa kama tuache kama lilivyo kwa nini wewe unalazimisha hoja? kila mtu ana haki ya kuliangalia hili jambo kwa jinsi anayoona ila wewe unataka kulazimisha tuamini kua polisi wanahusika.! kama huna ushahidi na wewe kaa kimya angalia tu wengine wakichangia
 
Kwa mtindo huu nadhani ni wasaa wa kujiandaa kisaikolojia,kimwili na kwa sala maana lolote linaweza kutokea katika nchi hii.inasikitisha kuona matendo haya against mtetea haki na mpigania haki.
Mungu haja lala
 
ss dr ulimboka atatibiwa vp wkt wapo ktk mgomo?au wao kwa wao haina shida. . . .

atatibiwa vizuri sana,tena ikiwezekana madaktari wote wakafanyie mgomo MOI,dr uli anahitajika akiwa hai aseme kilichotokea
 
Mkuu mbona unakuja mjini bila kupiga hodi?
 
Wakati suala hili linahusu maisha ya watu wapumbavu wengine waroho madaraka wanawaza jinsi watakavyo yapata. Mpo tayari kutumia maiti kufika ikulu, ila kumbukeni hakuna aliyepata madaraka kwa damu ya watu aliyeondoka salama.

CCM inalinda madaraka yake kwa kumwaga damu ya Dr. Ulimoka halafu wewe unakurupuka kufikiri kinyumenyume! Unatakiwa usome thread kwanza kabla ya kuchangia, usilete tabia za magamba! Hu uwanja wa GREAT THINKERS!
 
Serikali ya pinda toeni pesa kwa madaktari wanusuru maisha ya watz.Vasco da gama hana habari na mgomo huu na wala huwa hamshtui coz yeye n kula bata tu safarini.Rais gan huyu?.Eti serikal sikivu!! Kwa lipi?.
 
Haya mambo ya kutekana na kupigwa na kutelekezwa uwa yanatokea Colombia, Mexico, Cambodia, sasa yamefika mpaka Tanzania ni hatari sana tunapoelekea...Umafia umefika Tanzania.

Sasa Tafakari kwa makini na uchukue hatua.
 
Jamani tusihamasishe chuki na uvunjifu wa amani bali:
  1. upole
  2. upendo
  3. kusameana
  4. kuvumiliana

ni muhimu kutoa solution ya amani kuliko uvunjifu wa amani

tuache kuchukiana. Tupendane jamani tunaenda wapi?

Acheni maneno ya uchochezi, watakao umia ni wengi zaidi
 
Hapo tulipofika ni penalty shoot fanya mchezo na gvt
 
Ndio hapo nawashangaa watu wanleta hisia kwenye ishu sensitive namana hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…