Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Nimesikia eti Zembwela wa EA radio anasema huu ni uzushi tu...ni mtu mwingine aliyekuwa anadhaniwa ni usalama wa taifa ndiyo amepigwa na madaktari na yupo chini ya ulinzi wa askari wa muhimbili...katahadharisha na uvumi unaoenea kwenye mitandao ya kijamii...
 
Wakafunge na zile hospital zao za PRIVATE. Na kule PART TIME wasiende.

Pamoja na kwamba mnadai haki zenu jaribuni kuwafikiria na wengine hasa walalahoi ambao hawajui hata wafanye nini, waende wapi au wale nini leo! Mnadai haki kwa kupoteza roho zisizo na hatia???!!! Msiifanye migumu mioyo yenu, mwangalieni Mungu anayetoa uhai, jua na mvua bure kwa wote.

wakuwafikiria walala hoi ni serikali yao,sio madokta.
 
Hata kama wakipokelewa halafu hospitali zenyewe hata dripu au panadol mpaka ukanunue nje,wakati kuna watu
wameweka dola 300bil. Uswiss hutumii akili ukaona mantiki ya madaktari.Wewe ndio KILAZA MKUBWA......

Kwa hiyo watu wameiba dola 300bil ... nyinyi hasira zenu mnahamishia kwa mwananchi wa tandale ? wewe kichwa chako kitakuwa kimeja mikasi ya pale muhimbili
 
nasikitika Jk kuanza kuitawala nchi kwa style ya Idd Amin. Mungu rehemu upumbavu huu!
.
 
"Tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, kwa uzembe wa Bunge, na kwa sababu ya upuuzi wa CCM" Tuma kwa watu 10 kama unamsuport Mh. Mnyika bungeni.
 
yaani naumoa kupita maelezo,mungu wangu.....msaidie ulimboka apone aseme kilichomkuta
 
Madaktari msikubali huu upuuzi wa CCM uendee, hata mkirudi kazini akikisheni mtoto, ndugu au kiongozi yeyote wa CCM akiletwa hospitalini, watieni sindano ili wapooze.
 
Jamanieeeeeeeeeeee! hili swala si dogo. Watu walifikiri na kuliangalia kwa undani zaidi.

Hivi kuna uthibitisho gani kama waliomteka ni watu wa serikali???? Je, haiwezekani mwananchi yeyote mwenye uchungu wa kufiwa na ndugu yake kutokana na migomo ya madaktari akafanya utekeji huo kwa lengo la kulipiza kisasi? Kwani hao madaktari wenyewe wanaogoma wanapendana??? hawawezi kuwa na visasi vyao na kutumia muda huu kuchanganya ushahidi??

Tuweni makini katika hili.
 
Nimesikia eti Zembwela wa EA radio anasema huu ni uzushi tu...ni mtu mwingine aliyekuwa anadhaniwa ni usalama wa taifa ndiyo amepigwa na madaktari na yupo chini ya ulinzi wa askari wa muhimbili...katahadharisha na uvumi unaoenea kwenye mitandao ya kijamii...

Zembwela nae anaongea nn,pumbaf....ni ulimboka,comfermed
 
Jamani mi ndo naingia jamii forum kwa mara ya kwanza na ninasikitika sana kwa hali hii ya mgomo wa madaktari. swali kubwa kichwani mnifungue macho, Dr. anayeanza kazi analipwa shs ngapi? naomba msaada wenu ili nami nichangie objectively.

gross salary ni 957,700/=
wakikata Paye, NHIF, Pension fund inakuwa 705,900/=
TUGHE/TALGWU na loanboard wakichukua michango yao, inabaki kama 630,000/=.
Haya endelea kuchangia.
 
machozi yamenidondoka.. pole sana comrade, na jumuia ya madaktari Tz!
 
wewe mtoa maada,yule sio kiongozi wa mgomo.yule ni kiongozi wz umoja wao.
madaktari ndio waloamua kugoma hakuna mtu aliyewaongoza wagome.

Wote hao ni walewale tu. Usilete misamiati mingine hapa. Haitusaidii!
 
Tunaelekea wapi watanzania.
Busala inatakiwa sana katika swala hili,la sivo taifa litatumbukia pabaya.

God save Tanzania.


Ndio hali halisi. Niko hapa Muhimbili na madaktari, mageti yote ya Muhimbili yamefungwa na Wamesema LIWALO NA LIWE hakuna huduma yoyote inayotolewa, hakuna wagonjwa wala wahudumu wanaowahudumia wagonjwa KAULI YA PINDA na kitendo walichomfanyia OLIMBOKA vinaliangamiza taifa kutokana na UDHAIFU wa serikali ya Kipuuziii.

Mda mfupi uliopita jamaaa mmoja ambaye ni usalama wa taifa kapigwa alipokuwa anaripoti kwa walio mtuma kuangalia madaktari wamepokeaje hari ya Olimboka
 
Nimesikia eti Zembwela wa EA radio anasema huu ni uzushi tu...ni mtu mwingine aliyekuwa anadhaniwa ni usalama wa taifa ndiyo amepigwa na madaktari na yupo chini ya ulinzi wa askari wa muhimbili...katahadharisha na uvumi unaoenea kwenye mitandao ya kijamii...
Tutasikia mengi sana leo
 
SIDHANI KAMA HABARI HII NI YA KWELI! KAMA NI KWELI BASI

1-WATAKUA MADAKTARI WENZAKE WANACHEZA MCHEZO MCHAFU ILI WASIKILIZWE AU NCHI ISTAWALIKE

2- WATAKUA WANAHARAKATI WANATADUTA NJIA YA KUPATA PESA ZA WAZUNGU

3- WAFUASI WA CHAMA CHA SIASA WALIOMTEKA DC IGUNGA

siasa ina mambo mengi. anaweza kupakwa matope usoni na shati lake kumwagiwa damu ili aonekane kapigwa. anaweza hata kupelekwa icu na madaktari wenzake ili kuchochea mgomo na kuhamasisha wananchi. kuna watu wanataja bastola, sijui tunisia...... mbona mnaota ndoto za mchana. siyo raia wote wanaunga mkono mgomo wa madaktari. zaidi ya 85% wanaulaani
 
Lazima Pinda amewatuma wasalama wake wafanye kitu hicho kwa Ulimboka, kwanza kwa sababu yeye mwenyewe kasema liwalo na liwe, pili alimsema vibaya kiuadui mgomo wa kwanza akidai hamtambui, tatu yeye mwenyewe ni msalama wa Taifa anajulikana sana na hivyo ni kiongozi makini wa usalama wa taifa anayeweza kuwatumia apendavyo.

Nakumbuka kuna kiongozi mmoja wa UDSM miaka ya nyuma aliwahitekwa kama hivihivi akajikuta yuko mbele ya PM wa wakati ule Warioba akimuuliza "Kijana, do you know what a government is and its power?" Hayo maswali ni baada ya vichapo.

Kwa maana hiyo ni serikali tu inayoweza kufanya hadithi kama hiyo. Majambazi hawafanyagi hayo, wapate nini kwanza kwa ulimboka, wangemuua kabisa kama ni majambazi wa nje wa serikali. Hao waliofanya lazima ni majambazi walioko ndani ya serikali wanaotekeleza maagizo ya majambazi wao wakuu. PERIOD!
 
Jamani mi ndo naingia jamii forum kwa mara ya kwanza na ninasikitika sana kwa hali hii ya mgomo wa madaktari. swali kubwa kichwani mnifungue macho, Dr. anayeanza kazi analipwa shs ngapi? naomba msaada wenu ili nami nichangie objectively.

Udaktari ni kazi ya wito sio ya mshahara. Nilitegemea utauliza Dr anayenza kazi anaruhusiwa kutumia CT au MRI scans, au kuna gloves za kutosha kuwakinga madaktari na maambukizi?? Sasa wewe unaanza kuuliza mshahara!! Ndo nyie mtakuwa mnafurahia wagonjwa wafe ili uvute ila laki moja aliyotoa Pinda ya Post Mortam.
Ushauri wa bure nenda kasomee uhasibu ndio utakuwa unashinda na hela kila siku. Udaktari ni wito, hata madaktari waliogoma dai lao la kwanza ni kuboreshewa mazingira ya kazi na dai lao la mwisho ni nyongeza ya mshahara
 
Back
Top Bottom