Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

yaelekea great thinkers tumesahau kuwa mapinduzi hayaji ila kwa mtutu so ukiona hivyo ujue mapinduzi yako mlangoni. Binafsi namuona DR Ulmboka kama mtu aliyejitoa kwa ajili ya wengine.
 
WaTANGANYIKA hamjayazoea mambo ya aina hii !! Mnahitajia uamsho ili kusimama kidete na kutorudi nyuma. Ni majuzi tu mliwazomea WaZanzibari na kuwaita magaidi au materoristi na kuisifu serikali hihii mnayoibeza ,WaZanzibari wapo juu ya mstari wa Katiba kudai madai yao kisheria ,mlipoambiwa waliohujumu makanisa sio kutoka uamsho hamkusikia la mkuu leo guu ndio hilo limevunjika ,mnafikiri wenzenu waZanzibari wataungana na nyinyi kivipi ?? Wakati wanapopewa kibano huwa mnashangilia na kuleta hoja za ajabu ajabu ,akina Mwanakijiji mko wapi katika hili mbona hamsemi ??? Ni Serikali ya Muungano huo ndio unaofanya vitendo hivyo au sio.

UPANDE WA PILI WA SHILINGI

Sasa kwa upande mwingine naweza kusema inawezekana kabisa serikali haihusiki na janga hilo , tusifuate ushabiki au jazba ,katika hali ya kisiasa iliyopo leo Tanzania ,jambo lolote linaweza kutokea.

Wapinzani wanajua fika kuna mgogoro kati ya serikali na Madaktari mbali ya taasisi zingine,huu wa madaktari ni mkubwa na unaowavutia wananchi wengi sana. Technically kuitia serikali kwenye kitanzi ni kuwafanyia ushenzi viongozi wa mgomo huo kama alivyofanyiwa Ulimboka na upinzani kuwarushia Serikali kuwa ndio waliotekeleza ili kuwazima madaktari ,tayari serikali itakuwa imeshatiwa doa na pengine kuzidi kwa vurugu.

Serikali nayo inaweza kusema kuna Chama pinzani kimetekeleza uovu huu na uchunguzi unafanywa kubaini ni nani mhusika mkuu , kilichobaki ni huyo jamaa kutoka salama inaweza ikasaidia ,mnakumbuka kesi ya kifo cha Chacha ,dereva alipona ile kesi sijui imeishia wapi kwani ni kati ya serikali na CDM ndio mmoja wao alihusika,lakini hadi leo kimya.

Kisiasa ili kuiangusha serikali au upinzani kupata nguvu ni kutafuta njia yeyote ile ,sasa hii inaweza kuwa njia moja kuipotezea mvuto serikali kutoka kwa wananchi.


Sidhani kama serikali inaweza kuwa mhusika mkuu katika hili na kama imefanya basi walioshauri hawaitakii mema serikali iliyopo madarakani.
 
Kumbe uhai wa Dr Ulimboka ni muhimu kuliko wengine?!Tumwombee apone haraka!
 
kweli serikali yetu imejionyesha dhahiri kuwa haipo kwa ajili ya kuwasidia waTZ, bali kuwatesa. pole Daktari Ulimboka
 

Umenena mkuu...sio watu wanakurupuka tu wanaleta ishu za CCM na CHADEMA katika hali tete kama hiii....
 

Ina maana wewe ungekuwa ni miongoni mwa wafanya maamuzi ungefanya maamuzi ya kijinga kama hayo?!

Kuwatisha madaktari mbona jambo dogo sana mkuu wangu!! Hivi unataka kuniambia hufahamu ni kwanini madaktari walikuwa wanaenda kusaini lakini hawafanyi kazi?!

Ina maana hapo inahitaji mtu awe na digrii kufahamu kwamba pamoja na kugoma kwao lakini wanaogopa kupoteza ajira na ndio maana walikuwa wanasaini ili waonekane wamekuja kazini?!

Kuwaatisha ni rahisi tu.....ukiwatimua wale, baada ya mda wote wangerudi kufanya kazi na wala hawakuwa na sababu ya kumteka Ulimboka na kujenga picha ya kijinga kama hiyo!
 
zifungwe tu, tena ingefaa hata za private zifungwe kumuunga mkona dr. Ulimboka
 
kwamba Dr.Ulimboka ametoa mhanga siamini.!
 
Wanacho jaribu kufanya ni kuona kama madaktari watarudi kumtibu mwenzao
na kwa kufanya hivyo lazima watatibu wagonjwa wengine pia.....

Lakini je,hili litasaidia kuondoa tatizo?
 
umeulalia wewe.
 
Nadhani huu ni muda mwafaka kwa watanzania kuanza kufikiria kwa upana mwelekeo wa nchi yetu.

Kwa mtazamo wangu doctors hawana makosa tatizo liko na hii serikali, unajua huwezi sema serikali haina pesa lakini wakati huo huo wao(politicians) wanajiongezea mishahara. Yeyote anayewalaumu doctors afikirie na upande wa pili, hali ya hospitali zetu iko vipi?

Wewe ni mkulima halafu hata jembe, kwanja, reki huna na bado unategemewa uzalishe kwa ufanisi; linawezekana vp hili.

Watz tubadilishe mitazamo hospitali ni zetu siyo za madakitari, tunaokwenda kutibiwa ni sisi; mtazamo wangu ni kuwa katika hili la mgomo wa madakitari tuoneshe mshikamano wetu tuwaunge mkono kudai haki ya matibabu bora.

Nakuonea huruma sana Tanzania manake siioni Tz baada ya Kikwete!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nauliza hivyo kwa sababu nasikia analipwa 2m je ni kweli?

karibu sana mkuu,si kweli, wanalipwa kama uliyojibiwa hapo juu.na dai lao kubwa ni kuboreshewa mazingira ya kazi,majengo yaongezwe,vitanda vya wagonjwa,madawa yawepo,kuna wakati unataka just paracetamol unaambiwa ni out of stock!inauma sana wao wanatibiwa india
 
Rejea hotuba ya kikwete alipokuwa anaongea na wazee wa Dar kuhusu mgomo ulokuwa umeitishwa na TUCTA. Alisema nini kuhusu Mgaya?

Nikumbumbushe mkuu,yamkini yanaweza kutusaidia katika kipindi hiki cha msala wa Dr.Ulimboka.
 

Kuna kila dalili serikali itakuwa imehusika moja kwa moja, na imefanya hivyo kwa kufikiria yafuatayo:

Kuetegemea Uwezo wa Kudanganya
Kwa kufikiria kuwa wananchi hawawezi kufikiria serikali inaweza kufanya hivyo kwa kipindi hiki. Kwa kudhania kuwa utetezi wao utakuwa kama huo uliotolewa hapo juu ya kuwa serikali haiwezi kufanya ujinga kama huo kwa kipindi hiki

Kutumia Uzoefu wao wa Huko Nyuma
Serikali imewahi kufanya vitendo kama hivyo siku za nyuma kulipowahi kuwa na migomo ya Wanafunzi. Waliwahi kumteka Raisi wa wanafunzi wa chuo kikuu UDSM Bwana Bazigiza na katibu wake, na kumpa mateso kwa siku 21 wakaja kumwachia siku ya graduation baada ya wanafunzi wengine kutangaza wasingeshiriki kwenye sherehe hizo mpaka Rais wao aonekane. Hawana wasiwasi kuwa wananchi wanaweza kufanya chochote dhidi ya matendo kama hayo kwa sababu hawajawahi kufanya hivyo hata mara moja

Dharau ya Serikali Dhidi ya Nguvu ya Wananchi
Tumeshuhudia hivi karibuni, japo bila ya uthibitisho wa moja kwa moja, ikishiriki kuua wananchi mbalimbali ikiwemo viongozi wa vyama vya upinzani, wananchi wa kawaida wanaounga mkono vyama vya upinzani. Na wamekuwa wakifanya hivyo wakijua kabisa kuwa kila mtu ataiweka serikali/CCM mtuhumiwa wa kwanza lakini hawana hofu kwa kujua kuwa wananchiwa Tanzania ni waoga sana na hawawezi kufanya chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…