Ni Uchambuzi mzuri lakini naomba nipingane na wewe kwenye umalizio wako au niseme ungeongeza point ya Serikali yenyewe kuhusika moja kwa moja kuyafanya hayo.
Huwezi kuitoa serikali kwa kigezo eti ni utoto kufanya hivyo. Tumeshuhudia serikali ikifanya mambo mengi sana ya kitoto kabisa au mengine hata mtoto hawezi kuyafanya, sihitaji kuyasema kwani yanafahamika sana.
Kwa hiyo hatuwezi kuitoa kuhusika, ni moja kati ya makundi ya watuhumiwa uliowataja katika kisa hiki
Mkuu wangu coby,
Ni kweli katika tasnia za ukachero si busara hata kidogo kupuuza uwezekano wa aina yoyote katika jambo kama hili. Hata hivyo, labda tu nifanye usahihisho ili kuweka rekodi sawa. Suala la serikali kufanya jambo kama hilo si tu kwamba ni la kitoto bali ni jambo la hatari kuliko hatari yenyewe. Hivyo basi, pamoja na ukweli kwamba serikali inaweza kufanya jambo la kitoto lakini sizani kama inaweza kufanya jambo la hatari kama hilo ambalo madhara yake kwa taswira ya serikali ni makubwa mno. Ni serikali chache sana, ambazo hususani ni za kidikteta wa wazi ndio wanaweza kufanya jambo kama hilo.
Labda niongeze possibility nyingine katika mambo kama haya. Hata wananchi wa kawaida wanaweza kufanya alichofanyiwa Ulimboka. Just imagine, mtu amepeleka ndugu kipenzi halafu akafa kwa kukosa huduma huku yeye akiamini kwamba pamoja na kwamba madaktari wana madai lakini sio busara kwao kuacha watu wanakufa. Mtu au watu wenye mawazo kama hayo wanaweza kumtendea mbaya Ulimboka kama njia ya kulipiza kisasi.
Na wengine wanaweza kutaka kutoa ujumbe kwa Ulimboka na wenzake waone uchungu wa kuuguliwa....! Wahenga wanasema, ukitaka kujua kifo kachungulie kaburi!