Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana


Kimbinu huyo angedakwa kimya kimya then ateswe hadi ataje wenzake maana hapo polisi wameshamuokoa na hilo soo! Huyo alikuwa si wa kuachia polisi kabisa,very big mistake. JINO KWA JINO TUU!
 


Sasa atahudumiwa na nani wakati madaktari wamegoma?
 
unaweza kulazimisha Ng'ombe kwenda mtoni ,lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji.
 
Nadhani hawa watu waliomfanyia hivi walifikiri ameshakufa ndio maana wakamwacha. Wakijua kwamba bado yuko hai kuna uwezekano mkubwa watarudi ili kumalizia asije akawataja atakapopona. Kuna uhitaji mkubwa sana wa kuhakikisha anapatiwa ulinzi wa uhakika. Haya ndio yaliyosabisha kiongozi wa serikali ya wanafunzi miaka ya hapo nyuma, Harun Kimaro, atoroke nchi na kukimbilia Zimbabwe baada ya kupata taarifa uhai wake ulikuwa hatarini toka watu wa vyombo vya "usalama" vya serikali.
 
Mungu yuko nae, wala hafi ila sasa ndo wamemwaga petrol kwa moto, ndo watawajua vizuri.
 
mwenziwe akinyolewa wewe tia maji....... bado mkoba wa walimu sasa...... ajiandae. mimi simo natafakari wapi nikatibiwe, huvi huyo ulimbo alipata matibabu wakuuu. madaktari ni watu muhimu sana kama wanajeshi vitani kugoma ni ni ishara ya kukosa uzalendo just imagine wanajeshi wangegoma enzi za idd amin............leo wahaya ingekuwa historia. naumia mtanzania wa kawaida
 
Hii haina tofauti na ugaidi, kama serikali yetu inahusika na jambo hili basi hizo ni dalili mbaya sana.
Hatuwezi kuwarudisha kazini Madaktari kwa mbinu hizi,tunataka Madaktari warudi kufanya kazi kwa mioyo yenye dhamira ya dhati na upendo kwa wagonjwa. Kuwalazimisha kwa staili hii ndio tutakapo pasuliwa kichwa badala ya goti.
 
Angekamatwa ingejulikana ni kwa sababu zipi na amepelekwa wapi, unasema amekamatwa kwa mahojiano zaidi,unajua amekamatwa na nani na anahojiwa kuhusiana na nini?

Hakuna reconciliation ya usiku wa manane, hii ni serikali ya Dhaifu na ndo maana vyombo vya habari vimerpigwa biti kutangaza janga hili....
 
Dah! Pole sana Dr Ulimboka! I pray that whoever is responsible for this, is arrested and punished accordingly!
 
serekali wala haihusiki na hilo tukio, hili jambo limesha kuwa la kisiasa na njia moja nzuri ya kuichafua serikali ni kufanya vitendo kama hivi, hii itakuwa ni CHADEMA.

Nahisi umepoteza network
 
usilete nadharia hapa wewe, ya nini kuingia gharama za kumdhuru Dr Ulimboka badala ya kwenda hospitali binafsi? si lazima utibiwe hospitali za umma na hasa unapojua kuna tatizo la mgomo

Me nnadhani hapa tunajadili hili kwa kuzingatia hali halisi za Watanzania walio wengi masikini,inawezekana mwenzetu hali yako ni nzuri kifedha(tajiri) sasa sidhani Kama unaweza kuyawakilisha mawazo ya hali usiyoishi Kama sio kuipitia udogoni.Hivi unafikiri Watanzania wote wanao uwezo wa kwenda katika hizo hospitali binafsi?Hebu kuwa mzalendo ndugu yangu(wajali wenzio kabla ya kujijali wewe tu).
 
Duh mbaya sana kwa kosa lipi????
Why polisi wanasema juu ya hili??
Pole sana dokta mungu atakuponya kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…