Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Hivi huko MOI nako si kuna mgomo au?? Yeye amepokelewa kama nani (mgonjwa wa kawaida kama wananchi wengine tulionyimwa huduma au yeye ni spesheli??)

Double standards all the way............

Pole Dr. Ulimboka ila yawezekana pia watekaji walitaka kuona je huyu Dr. Ulimboka akipata shida inayohitaji matibabu atahudumiwaje kipindi cha mgomo!? - Just speculating


It is not time for kidding guys!
 
Duh! Maskini ya Mungu!!! Hii Serikali ya wauaji...Inatisha sana. Halafu watu wanasema tutumie majina yetu ya kweli hapa JF!!! Mnaona jinsi Serikali hii inavyoweza kabisa kumaliza uhai wako kwa kuandika ukweli jinsi ambavyo imeshindwa kukidhi matumaini mbali mbali ya Watanzania...Sasa kila atakayeipinga ajue maisha yake yako hatarini anaweza kabisa kukolimbwa!!! Pole sana Ulimboka na madaktari wengine wote kwa tukio hili la kusikitisha na kutisha.
Una ushahidi gani kuwa ni serikali ndio imetenda hili jambo?
 
hapa lazima m2 ajihudhuru,si mtu tu,mtu mkubwa
 
Hizo kauli zitizamwe kwa umakini sasa maana Dr Ulimboka hupo hoi hosptali, Damu ya wenye haki itawalilia hawa walioshindwa kuongoza wameamua kutisha watu, na huu ni UDHIFU MKUBWA SANA
Hii ni hatari sana, lazima mtoto wa mkulima atueleze kauli yake "NA LIWALO NA LIWE" ilikuwa na maana gani!
 
Habari zinazoletwa na magwanda humu ndani huwa za kutatanisha, mara "atekwa", mara yuko "polisi", mara kaokotwa "mabwepande" yuko taabani.

Hivi huwa hamjui kusema kweli?

Isitoshe, kama kweli hili la mwisho la kuwa kala kichapo mpaka kawa taabani limefanyika, basi hapo itakuwa kuna watu wenye uchungu wameupokea ushauri wangu nilioutoa jana humuhumu JF, huu hapa:

Hao madaktari waliofanya mgomo ilipaswa wananchi tuchukuwe sheria mkononi tukawape kichapo kama tunavyowapa vibaka. Tukiwatandika wawili watatu wengine watarudi kazini au wataacha kabisa udaktari.

Serikali hawa ndio wakuwashughulikia ipasavyo. Sasa fungeni madai yao yote, wakatafute pa kufanya kazi. Na wote wanaogoma wasiruhusiwe kufanya kazi za udaktari hata private hospitals.
 
JK a.k.a Dhaifu, Pinda na serikali dhaifu na ya kipuuzi mkajipange kwa mapigano yasiyo na kikomo kwa msiyemuona wala kumjua
 
Natamani kuona maandishi ya Riz1, Nape na marehem Rejao plus marehem malaria sugu juu ya issue hii? Ninaanza kuona mambo yaliotokea Tunisia hapa kwa mbaaaali yaja na hapa kwetu.
 
Una ushahidi gani kuwa ni serikali ndio imetenda hili jambo?

Umesikia kauli ya Pinda liwalo na liwe? umejaribu kuifafanua ili kuelewa kwa kina?

Taarifa iliyonifikia hivi punde ni kuwa jemedari Dr. Ulimboka ametekwa majira ya saa sita usiku na watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka kusikojulikana! Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la 'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa akiwasiliana naye na kujiita afisa wa serikali na kudai kuwa alitaka aonane naye face to face kwa ajili ya reconciliation.
 
Imerudi enzi ya Mwalimu Nyerere system at work!!!Mhn be carefully marze
 
Sasa serikali ya CCM imechoka kabisa huezi kuwaforce Madr. kufanya kazi, police wa Tanzania hawana maaana kabisa kwani wanatumiwa na wanasiasa wasiokuwa na akili na ndio maaana police wanaongoza Tanzania kwa kutumia vyeti visivyo vyao kutumia majina ya watu wengine, ndio maana wanatii amri hata ambazo kwa logic ya kawaida ilitakiwa wasikubali. Dr.'s Komaenii tu acha watu wafe hata ikifika zamu yangu kwa hilo nami nife tu.
Fishbaba
Mtetezi wa wataamu.
 
Last edited by a moderator:
[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD][h=2]Serikali inawajibika kutueleza: Dkt. Ulimboka kutekwa, kupigwa na kuumizwa - Zitto Kabwe[/h]27/06/2012
1 Comment


Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI

‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad, I agree with you this is outright outrageous'

Nimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.

Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.

Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa 'agente provocateure' kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.

Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.





[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Source: wavuti - wavuti
 
Mkuu wangu coby,
Ni kweli katika tasnia za ukachero si busara hata kidogo kupuuza uwezekano wa aina yoyote katika jambo kama hili. Hata hivyo, labda tu nifanye usahihisho ili kuweka rekodi sawa. Suala la serikali kufanya jambo kama hilo si tu kwamba ni la kitoto bali ni jambo la hatari kuliko hatari yenyewe. Hivyo basi, pamoja na ukweli kwamba serikali inaweza kufanya jambo la kitoto lakini sizani kama inaweza kufanya jambo la hatari kama hilo ambalo madhara yake kwa taswira ya serikali ni makubwa mno. Ni serikali chache sana, ambazo hususani ni za kidikteta wa wazi ndio wanaweza kufanya jambo kama hilo.

Labda niongeze possibility nyingine katika mambo kama haya. Hata wananchi wa kawaida wanaweza kufanya alichofanyiwa Ulimboka. Just imagine, mtu amepeleka ndugu kipenzi halafu akafa kwa kukosa huduma huku yeye akiamini kwamba pamoja na kwamba madaktari wana madai lakini sio busara kwao kuacha watu wanakufa. Mtu au watu wenye mawazo kama hayo wanaweza kumtendea mbaya Ulimboka kama njia ya kulipiza kisasi.

Na wengine wanaweza kutaka kutoa ujumbe kwa Ulimboka na wenzake waone uchungu wa kuuguliwa....! Wahenga wanasema, ukitaka kujua kifo kachungulie kaburi!

Typical of a Socialist Party Security. They never learn, from Russia, Cuba, North Korea, China and all.

Dr. Ulimboka was supposed to be under maximum surveillance for his security as well as picking up any intel.

Please do not tell me TISS never thought of that.

Unajua kabisa huyu mtu akidhurika kutatokea mgogoro mkubwa zaidi, na humpi any security. TISS hawajui hilo? Kuwa akiumizwa na kitu au mtu yoyote watu watainyooshea serikali vidole na mgomo kuwa mkubwa zaidi.

Sasa kwa nini asipewe ulinzi. Wakitokea wakenya wakamdhuru ili tu kuhatarisha amani ya nchi, nani wa kulamiwa? Hao TISS wanafanya kazi gani.

I blame them and suspect they are involved maana haiingii akilini kusema huyu mtu hakuhitaji ulinzi.
 
Sasa hii ni kazi mpya!!!!!! imeanzishwa na hawa jamaaa Sirikalis! Jino kwa jino!!!!? kama tuko somalia!!?? :mod:
 
Emancipate yourselves from mental slavery;
None but ourselves can free our minds.
Have no fear for atomic energy,

'Cause none of them can stop the time.

How long shall they kill our prophets,
While we stand aside and look? Ooh!
Some say it's just a part of it:
We've got to fullfil the book.
 
Back
Top Bottom