Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Hili halita kwenda likaisha hivi hivi. Mijizi mikubwa hii
 
Waliomteka ni watu wenye hasira za kufiwa na ndugu zao na kukosa huduma mahospitalini kwa ajili ya huyu mnafik pamoja na wenzake.
 
wana JF, je inawezekana kuanzisha michango hapa kwa ajili ya matibabu ya huyu dr Ulimboka na ikiwezaka nje ya nchi. kama masanja aliweza kufanikisha michango kwa ajili ya Sajuki, kwa nini JF yenye wanachama zaidi ya 80,000 washindwe?
Kila member wa JF achangie kiasi kidogo cha 1000/ tu. Nani anaweza kuratibu hii kitu?????????????//
 
Umesikia kauli ya Pinda liwalo na liwe? umejaribu kuifafanua ili kuelewa kwa kina?

Taarifa iliyonifikia hivi punde ni kuwa jemedari Dr. Ulimboka ametekwa majira ya saa sita usiku na watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka kusikojulikana! Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la 'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa akiwasiliana naye na kujiita afisa wa serikali na kudai kuwa alitaka aonane naye face to face kwa ajili ya reconciliation.
hiyo statement ndio ushahidi wako? Je nikisema kuwa CHADEMA baada ya kusikia maneno ya PM wametumia vijana wao kufanya hili tukio. Mtu anaweza kujipachika jina lelote na cheo chochote.
 
Wadau,
Habari ndiyo hiyo.

"Jamani this is iserious nimepigiwa simu sasa hivi na watu wa legal and human rights center wameniambia wametoka kumchukua Dr Ulimboka kule Mabwepande amepigwa vibaya sana na ni emergency wanampeleka MOI sasa hivi please tunaomba mtume habari hii kila mahali please!
Ni habari ya uhakika sana nimeomngea na Patience Mlowe wa Legal and Human Rights center"".
By Dr. Riwa


Sasa atahudumiwa na nani wakati madaktari wamegoma?
 
nikimaliza mhimbili nasepa zangu zimbabwe sifanyi kazi katika hospitari za serikali ni ujinga mkubwa
 
wana JF, je inawezekana kuanzisha michango hapa kwa ajili ya matibabu ya huyu dr Ulimboka na ikiwezaka nje ya nchi. kama masanja aliweza kufanikisha michango kwa ajili ya Sajuki, kwa nini JF yenye wanachama zaidi ya 80,000 washindwe?
Kila member wa JF achangie kiasi kidogo cha 1000/ tu. Nani anaweza kuratibu hii kitu?????????????//
Naunga mkono hoja...
 
Naamini njia zao zingine ziligonga mwamba na wameamua kubadilisha tu njia za ubabe, wameona sumu inadunda wameanza kuwadunda sasa. Ila kwa nini Dr. Ulimbooka alikubali kutoka usiku ule wote na alikuwa anajiamini nini? Kwa kweli naye hakufikiria vyema, Japo si mda wake sasa kulaumu ila watu wengine wajifunze wasije kukubali kukutana na mtu yeyote usiku hata kama iweje. Kwa sasa ngoja tuone madaktari watachukua hatua gani kulingana na hili tukio la kusikitisha sana

I hope this story is not true.

Mkuu usimlaumu Ulimboka, what if hii ni kawaida ya yeye kukutana na vingozi wa serikali chini ya usimamizi wa secret agents?. Kama ni kweli yamemkuta yaliyomkuta Ulimboka basi this is the war for the Govt to lose. Kazi ya usalama wa Taifa ni nini hasa?. Mi najua kuwa watu ambao huwa na influence kubwa sana katika nchi huwa wanalindwa bila wao kujijua kwa masilahi ya nchi, maana anything happens to them will trigger unrest.

Hii vita ni vita ambayo serikali imechagua wakati ikiwa haina jeshi na silaha za kuishinda.
 
[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD]Serikali inawajibika kutueleza: Dkt. Ulimboka kutekwa, kupigwa na kuumizwa - Zitto Kabwe

27/06/2012
1 Comment


Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI

‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad, I agree with you this is outright outrageous'

Nimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.

Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.

Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa 'agente provocateure' kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.

Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.





[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Source: wavuti - wavuti
Huyu nae naanza kumuona ni mpumbavu tu, je yeye anauhakika gani kama ndio serikali imehusika, hizi statement mchwara ndio zina kuja kuwaponza hawa wanasiasa mchwara.
 
Habari zinazoletwa na magwanda humu ndani huwa za kutatanisha, mara "atekwa", mara yuko "polisi", mara kaokotwa "mabwepande" yuko taabani.

Hivi huwa hamjui kusema kweli?

Isitoshe, kama kweli hili la mwisho la kuwa kala kichapo mpaka kawa taabani limefanyika, basi hapo itakuwa kuna watu wenye uchungu wameupokea ushauri wangu nilioutoa jana humuhumu JF, huu hapa:

Mimi nadhani wananchi tunatakiwa kuchukua hatua ya kumchapa na kumzika raisi Kikwete yeye na familia yake akifuatiwa pinda yeye na familia yake waliofilisi nchi hii kwa kuuza kila kitu kilicho juu na chini ya ardhi yetu, lakini sio madaktari wanaotugombea sisi wananchi kupata huduma bora
 
hiyo statement ndio ushahidi wako? Je nikisema kuwa CHADEMA baada ya kusikia maneno ya PM wametumia vijana wao kufanya hili tukio. Mtu anaweza kujipachika jina lelote na cheo chochote.


Naona unataka kuleta ubishi usiokuwa na kichwa wala miguu...Wewe amini unavyotaka kuamini wewe, na Watanzania wenye akili timamu ya nini kinachoendelea nchini wataamini vile wanavyotaka kuamini wao.
 
Angekamatwa ingejulikana ni kwa sababu zipi na amepelekwa wapi, unasema amekamatwa kwa mahojiano zaidi,unajua amekamatwa na nani na anahojiwa kuhusiana na nini?


Sitasema lolote hadi Serikali itoe tamko juu ya jambo maana kwanza siamini haya mazingaombwe .
 
huko fb,kuna picha tayari zinazomuonyesha dr ilimboka baada ya kupigwa!kwa kweli hali ni mbaya
 
Inawezekana kabisa kuwa ni njama/mbinu/mkakati wa wapinzani ili kuchochea hasira ya wananchi dhidi ya serikali yao. Sidhani km serikali wanaweza kufanya upuuzi/kosa hilo.
 
Sidhani kama kuna haja ya kusubiri uchunguzi wa polisi. Kwa mtu yeyote anayejua namba ya simu ya Dr Ulimboka, aiweke hapa jukwaani. Kuna watu ndani wa Tigo/Voda/Airtel/Zantel, wazichukue wacheck kwenye system kuona mara ya mwisho aliwasiliana na nani...
My foolish brain... sidhani kama hao wahuni watakuwa wameacha record yeyote kwenye system ya namba ya Dr... watakuwa wameshazifuta huko Voda...
But at least we have the name... Abeid, Abeid, Abeid...

no, no, no... Huyu mtuma thread (langei) amejuaje huyu jamaa aliwasiliana na Abeid?... wakati alikuwa hawezi kuongea wakati anaokotwa? Langei hebu isaidie JF kwenye uchunguzi...
 
Kama ni kweli hii habari basi lazima nitamke wazi kwamba serikali haiwezi kufanya jambo la kipuuzi kama hilo wakati madhara ya upuuzi kama huo yapo wazi. Kwa vyovyote vile, hiyo inaweza kuwa ni ama hujuma dhidi ya serikali, au hujuma dhidi ya kiongozi wa nchi au mchezo wa kitoto uliofanywa na madaktari wenyewe, au wabaya wa Ulimboka mwenyewe.

MCHEZO WA KITOTO WA MADAKTARI:
Kikundi kidogo cha madaktari wenyewe wanaweza ku-engineer mpango wa kipuuzi kama huo ili kutafuta huruma ya wananchi.
Michezo ya kitoto kama hii inafanywa sana na huwa inaaminiwa na wale wasio na uwezo wa kuchanganua mambo.

HUJUMA DHIDI YA SERIKALI:
Watu wenye maslahi tofauti dhidi ya serikali wanaweza kufanya upuuzi kama huo ili kujenga picha kwamba serikali iliyopo ni ya kidhalimu inayoweza kufanya lolote dhidi ya raia wake wanaotetea maslahi yao. Watu wanaoweza kufanya haya ni wale wenye maslahi ya kisiasa...ni Political Sabotage.

HUJUMA DHIDI YA RAIS:
Ulingo wa siasa ni ulingo uliojaa uadui baina ya mtu na mtu. Katika hilo, mtu au kikundi cha watu wanaweza kufanya upuuzi kama huo ili kumuumbua kiongozi mkuu wa nchi.

MAADUI BINAFSI WA Dr. ULIMBOKA MWENYEWE: Hawa wanaweza kutumia opportunity ya Dr. Ulimboka kuwa ndani ya mgogoro ili ionekane kwamba waliomdhuru ni watu wa serikalini.

MOJA kati ya hizo inaweza kuwa ndio sababu sahihi lakini there's no way kwamba serikali inaweza kufanya utoto kama huo. Ki

Try to think out of the box also. Remember Matiku from UDSM???

When you have to analyse issues you have to do it critically, meaning that you have to look at both possibilities. So far your possibilities are one sided bro!!!
 
Pole ndg Dr.Uli,Hakika Mungu atakulipia na damu yako iliyomwagika imejaza ujasiri watanzania wengine wengi.Aluta Continua.
 
Back
Top Bottom