Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

MOD, ondoa huu uchafu hapa plz!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Yule 'liwalo na liwe' ni kiongozi wa chama cha TLP nchini sio????????????

Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa tukio la kutekwa na kupigwa vibaya kwa Dr ULIMBOKA limefanywa na baadhi ya vyama vya upinzani ikiwa ni njia ya kuwapandikizia wananchi chuki zaidi dhidi ya serikali iliyopo madarakani.
Akiongea kwa kuijiamini sana mpelelezi huyo amesema wameshaanza kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo lakini awali picha ya tukio zima linawafanya waamini Serikali haijahusika kwa namna yeyote kwa hili.
Mengi tutayasikia na kuyashuudia Tanzania ni zaidi ya uifikiriavyo.

Get well soon Dr ULIMBOKA na haki itatafutwa hata kwa upanga.
Keep it up.
 
Huyu Mbwa mpelelezi??? Toka lini mtuhumiwa ajichunguze alete majibu ambayo ni positive!!! Wanatafuta wakumwegeshea Zigo Lao!!!
 
hizi ccm bado ina dhani watanzania wa leo ni sawa na wa mwaka 70
 
Serikali iko nyuma saaana. Yaani ni sawa na kusema watanzania huku mtaani wamepiga hatua 1,000 lakini serikali bado iko kwenye hatua 10! Huu mchezo wa 'cheusi-chekundu' ulishachuja, umeitwa, hauna maana tena kwa kizazi cha leo cha DOTCOM.

Na kwa bahati mbaya serikali wanaliangalia hili tatizo la madaktari in isolation. Huu muono mfupi sana. Mgogoro wa madaktari ni kilelel cha feelings za watanzania wa leo katika fani mbalimbali, na kama serikali itaendelea kuwa kipofu watajikuta wanazima hapa lakini hatua 2 mbele moto ni mbaya zaidi.

Ni lazima wajiuluze, tumefikaje hapa? Madaktari wameanza kudai haki leo? Na matatizo haya yako kwa madaktari tu? Inakuwaje serikali 'maskini' ijitengee Tsh 3 trillion kuhudumia mawaziri 55? lakini itenge Tsh 700 kwa Halmashauri? Inakuwaje serikali imiliki magari yenye thamani ya Tsh 5 trillion lakini iache wagonjwa wakilala chini, tena bila ya dawa? Ni cha muhimu, kununua shangingi au kununua 'x-ray machine? Kulipa posho ya kukaa (seating allowance) au kumlipa mtu anayeokoa maisha?
 
Ndio mbinu zenu kuua atake kuua JK mzigo atupiwe BLANDINA NYONI hatudanganyiki...atakaye tawala kwa mtutu nae atamalizwa kwa mtutu refer GADDAFI incidence.
 
usalama wa taifa wote Wana mivyeti feki walivyo vipata Bulgaria, yugoslavia, Russia na ukrain Pambaf zao Kama ni wataalamu na wamo humu ndani waseme hii comment imetokea wapi narudia tena Pambaf zao
 
Naipa serikali masaa 6, wasipotuambia ni akina nani wamefanya huu unyama, basi nitaamini asilimia 100 kwamba serikali yenyewe ndio imehusika.
 
serikali ndio inamakosa hapo kwani hata kipofu anaona na kwanini wasiwatekelezee madai yao?fedha ndio hazipo?wakati huo wao wanajilipa mishahara mikubwa na hawana elimu zaidi ya hao madaktari.

Mr Z mm sina takwimu za mishahara ya Madaktari wala watumishi wengine wa Serekali, ila kitu kimoja naweza kukiwekea uhakika kuwa kwa Standard narudia kwa Standard ya Tanzania/Tanganyika Madktari wanalipwa vizuri kuliko watumishi wa Sekta Nyingine. Mbali na ongezeko la kipato , pia wanadai Mazingira bora ya kufanyia kazi, na huo ni uwanja mpana ambao kama Mishahara hauwagusi madaktari tu. hivyo hauwezi kutekelezeka kwa hadithi za Kusadikika.
Narudia tusimame kwenye mada ,tusipambwe na huzuni wala tusiwe washabiki, Tuangalie ukweli uliopo Mezani.
Kilichomkuta Dr ni cha kusikitisha naungana nawe kukilani kitendo hicho. Madaktari wetu ni watu Muhimu sana Lakini WASIJIONE wao ni Muhimu kiasi cha kucheza na MAISHA ya wengine hilo halikubaliki hata katika hizo nchi zenye Demokrasia Iliyokomaa. Kwa hiyo wasijidangaye, huruma na uvumilivu wa Wananchi wenzao una kipimo na kikomo.
Kama Akili ya Darasani imeshindwa kuwasaidi...............Watumie Akili ya kuzaliwa! Waingereza wanasema ukipewa Futi usichukuwe Yadi...............!!
 
Serikali iko nyuma saaana. Yaani ni sawa na kusema watanzania huku mtaani wamepiga hatua 1,000 lakini serikali bado iko kwenye hatua 10! Huu mchezo wa 'cheusi-chekundu' ulishachuja, umeitwa, hauna maana tena kwa kizazi cha leo cha DOTCOM.

Na kwa bahati mbaya serikali wanaliangalia hili tatizo la madaktari in isolation. Huu muono mfupi sana. Mgogoro wa madaktari ni kilelel cha feelings za watanzania wa leo katika fani mbalimbali, na kama serikali itaendelea kuwa kipofu watajikuta wanazima hapa lakini hatua 2 mbele moto ni mbaya zaidi.

Ni lazima wajiuluze, tumefikaje hapa? Madaktari wameanza kudai haki leo? Na matatizo haya yako kwa madaktari tu? Inakuwaje serikali 'maskini' ijitengee Tsh 3 trillion kuhudumia mawaziri 55? lakini itenge Tsh 700 kwa Halmashauri? Inakuwaje serikali imiliki magari yenye thamani ya Tsh 5 trillion lakini iache wagonjwa wakilala chini, tena bila ya dawa? Ni cha muhimu, kununua shangingi au kununua 'x-ray machine? Kulipa posho ya kukaa (seating allowance) au kumlipa mtu anayeokoa maisha?

Mkuu hizi 3Trilion kwa Mawaziri 55 ni Mafungu kwa Wizara zao? au.........? Ni kweli jamaa Uwiano/Balance umewashinda kabisa. Wameyafumbia macho yale yanayotaka kipaumbele!
 
Nia yao ilikuwa ni kumuuwa lakini mungu kamnusuru, na hii sio mara ya kwanza kwa watu wa namna hii kuhujumiwa na sirikali hata kina sokoine yaliwapata haya
 
hii serikali ina michezo michafu sana...ulimboka anaweza kutoa ushahidi mzuri sana akipona........

mwakyembe alituambia atakuja kusema kila kitu lakini kwa mshangao wa wengi akapotezea...
 
freedom is not a gift,we have to fight for it and suffer for it and that is what is being done by doctors,never give up doctors and for this no stone is left unturn.
 
mheshimiwa Aweda unaropoka kweli. Wewe akili yako yote inakutuma serikali imehusika! Usitizame mambo kama uko kwenye tundu la kisima. Zoom!!! Kwanini chadema isihusike ili kujenga chuki ya wananchi na serikali yao? kwanini tusiamini kuwa chadema wamepanga hivyo na kujiandaa kutoa shutuma moja kwa moja kwa serikali ili ionekane serikali imefanya hivyo? Think broadly!
 
Hawa wasauzi wakisimama wanasimama kama wao, hawategemei support kutoka vyama pinzani. Wako makini, issues zao hawazigeuzi za kisiasa ndio maana wana nguvu. Hakuna serikali yoyote duniani ina urafiki wa kweli na wafanyakazi, they are negatively related. ukisha jua hilo, cha kwanza ni kukataa mgomo wenu kuingiliwa na chama chochote cha siasa ili usipate sura ya kisiasa, vinginevyo mtapoteza malengo
 
mheshimiwa Aweda unaropoka kweli. Wewe akili yako yote inakutuma serikali imehusika! Usitizame mambo kama uko kwenye tundu la kisima. Zoom!!! Kwanini chadema isihusike ili kujenga chuki ya wananchi na serikali yao? kwanini tusiamini kuwa chadema wamepanga hivyo na kujiandaa kutoa shutuma moja kwa moja kwa serikali ili ionekane serikali imefanya hivyo? Think broadly!

watu hawataki kufikiri nahamini kama serikali ilifanya hv ingempoteza kufuta ushahd lakin iweje haachwe hai!ebu tujarib kufikiri.swali kunawatu walipambana kumuokowa au hamekutwa katupwa 2!
 
Back
Top Bottom