Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Jamani this is VERY SERIOUS NEWS nimepigiwa simu sasa hivi na watu wa legal and human rights center wameniambia wametoka kumchukua Dr Ulimboka kule mwabepande amepigwa vibaya sana na ni emergency wanampeleka MOI sasa hivi please tunaomba mtume habari hii kila mahali please!
Na kama kuna anayeweza kusogea eneo la MOI kwa ajili ya kutoa msaada please leave whatever you are doing tukutane pale.

Ni habari ya uhakika sana nimepigiwa simu na Patience Mlowe wa Legal and Human Rights center.
This is real bad
 
Soma thread zilizopita! habari inaongelewa tangu jana saa 6 usiku we bado unauliza maswali ambayo majibu yake yapo humuhumu kwenye hii thread!
Nimeuliza watu wote wenye silaha ni polisi?
 
Sumaye frederick waziri mkuu mstaafu aliwahi kutuonya watanzania kuwa "yeyote anayetaka madaraka kwa kutumia kalamu kuwachafua wenzake akiingia madarakani atatumia RISASI KUJISAFISHIA NJIA"
 
There's something fishy kuhusu hili tukio,time will tell.
 
Wakati suala hili linahusu maisha ya watu wapumbavu wengine waroho madaraka wanawaza jinsi watakavyo yapata. Mpo tayari kutumia maiti kufika ikulu, ila kumbukeni hakuna aliyepata madaraka kwa damu ya watu aliyeondoka salama.
 
Watanzania lakini wakadhulumiwa na NEC kwa kumtangaza dhaifu kuwa mshindi na kwa kuwa haturuhusiwi kupiga ikabidi tuwe wadogo kama piritoni hata kama angekuwa mbwa ndiyo katangazwa kuwa mshindi..
katika karatasi la kura lile sikuona mgombea akiitwa watanzania may be i miss the point here!
 
Pole sana bajabiri
Unashabikia usilolijua.
Serikali inapaswa kufuata sheria sio kujichukulia sheria kihuni kam unavyoshabikia.
SOMA katiba

SEHEMU YA TATU
HAKI NA WAJIBU MUHIMU
Haki ya Usawa
Usawa wa
binadamu
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
12.-(1) Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa.
(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na
kuthaminiwa utu wake.
Usawa mbele
ya Sheria ya
1984 Na.15 ib.6
13.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki,
bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya
sheria.
Sheria ya Na.4
ya 1992 ib.8
Sheria ya 2000
Na.3 ib.5
(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka
yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo
ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya
watu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombo
vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwa
mujibu wa sheria.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
17
(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au
mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria
yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya
Mamlaka ya Nchi.
(5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii
neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji
mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao,
kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini,
jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina
fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na
kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa
aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida
iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno
"kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikali
kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha
matatizo katika jamii.
(6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,
Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia
misingi kwamba -
(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji
kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo
kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na
haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na
pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya
kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au
chombo hicho kingenecho kinachohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai
kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka
itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa
hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya
kitendo chohote ambacho alipokitenda hakikuwa ni
kosa chini ya sheria, na pia kwamba ni marufuku kwa
adhabu kutolewa ambayo ni kubwa kuliko adhabu
iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendwa;
(d) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu,
heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zote
zinazohusu upelelezi na uendeshaji wa mambo ya
jinai na katika shughuli nyinginezo ambazo mtu
anakuwa chini ya ulinzi bila uhuru, au katika
kuhakikisha utekelezaji wa adhabu;
(e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama
au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.
 
nawapa pole wagonjwa wanaokosa huduma mahospitalini kutokana na mgomo
 
Pinda and team, wanaweza kumteka mtu ila si fikra za mapinduzi ambazo Dr. Ulimboka amezianzisha na zimeshaingia vichwani mwa watanzania.
 
attachment.php
 

Attachments

  • 301770_299621630107499_700334721_n.jpg
    301770_299621630107499_700334721_n.jpg
    68 KB · Views: 448
Ndio hali halisi. Niko hapa Muhimbili na madaktari, mageti yote ya Muhimbili yamefungwa na Wamesema LIWALO NA LIWE hakuna huduma yoyote inayotolewa, hakuna wagonjwa wala wahudumu wanaowahudumia wagonjwa KAULI YA PINDA na kitendo walichomfanyia OLIMBOKA vinaliangamiza taifa kutokana na UDHAIFU wa serikali ya Kipuuziii.

Mda mfupi uliopita jamaaa mmoja ambaye ni usalama wa taifa kapigwa alipokuwa anaripoti kwa walio mtuma kuangalia madaktari wamepokeaje hari ya Olimboka
 
Kwa nini wasiwe ndugu wa jamaa waliopoteza maisha kwa mgomo? kwa nini unasema ni polisi?

Eti? Hata mimi najiuliza hilo? Anyway kama yupo mzima najua yeye atapata matibabu bora kutoka kwa madaktari wenzake na atapona. Kwangu mimi, yeye hata ange/akipoteza maisha sio issue, issue ni pale ndugu yangu alipofariki tokana na mgomo wao wa mwanzo, bado nagugumia kwa huzuni na maumivu. Kumbe kuna wakati Mungu anaweza akalipizia hapa hapa duniani, kwani naona kama kuna Mungu anaanza kutulipizia kwa machungu yaliyotukuta wakati ule ndugu yetu amepoteza maisha.
 
Ni mgonjwa hata kabla hajatekwa kama una macho mwangalie vizuri utajua anaumwa nini? anataka kwenda na mwengi??

Gonjwa linalomsumbua linaweza kuwa limeharibu kichwa chake tukidhani anatetea wanyonge.

mbona nawe ni mgonjwa lakini hatukusemi? Umagamba unakusumbua tu wewe .
 
Ee Mungu tusaidie waja wako kwako yote yawezekana. Hii hali ni mbaya.
 
Back
Top Bottom