Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kweli inasikitisha hiki kitendo walichomfanyia.

Kwa kusema kutotumia majina ndio mtu huwezi julikana hiyo sio kweli, admin wa JF au niseme forum yoyote wana access ya juu kwa mtu anaye jiregister katika forums.

wanaweza mengi, kujua IP address uliyojiungia, wapi unalog in toka, kulink username yako na e-mail (wengi hutumia majina), ni kuwa ukijiunga u basi umewapa ruhusu ya kukujua weye. wengi ukigoogle e-mail zao utakuta majina etc, au hata kwenye facebook kama wapo public utapata kuona profile zao etc. hii kitu inatumika na wengi hata kwenye maofisi kumjua mtu etc

hata mtu uwe Musoma utume ujumbe unajifanya upo Mbeya wakitaka angalia wanajua ukweli.

Cha umuhimu ni kuamini kuwa hawa admin na owners wa forum hawata angukia kupokea pesa za kuongwa ili kutoa data za watu. wanaweza block ip address ya mtu, kwa hiyo mtu inajulikana ni hadi wapi wanaweza fika.

Ndio maana ni muhimu sana owners wa forums kutoa access kwenye sensitive data kwa watu wanaowaamini, humu kuna mods I guess sidhani kama wanawajua wote kiundani as na ma spy wanaweza kuwa wamo. kitu cha michango ya pesa nyingi isifanye wakadhani kuwa hao ndio watakatifu.

mtu anaweza kutumia pesa kupata anachotaka hata kama itawachukua miezi, miaka bali wajilinde na mambo or maisha yao.

ukitaka leta nyaraka na unajua utakuwa huru bila kufatwa au kuwa na wasi basi ni...
kutumia connection ya internet isilink na home kwako, kazini au unapokuwepo mara nyingi, zile za kununua kwa mwezi, fungua e-mail account tofauti, ingia kwenye forum ujisajili thne rusha mambo.

tabu humu wengi wana fikira ndogo wakiona mtu kajiunga siku hiyo au siku chache zimepita wanadhani mambo yanayoletwa ni mchezo hawajui ujanja wa kutumia mitandao.

haya I hope wenye mambo watarusha wakitaka kusaidia nchi yetu.

Mkuu, ma-spy wamo kibao! Jaribu kuangalia kwenye personal profile yako utaona idadi ya waliotembelea ukurasa wako inaongezeka lakini last visitors ni walewale (ID ni zile zile). i have been watching mine and there are constant IDs that are never miss!
 
Pamoja na masikitiko yangu makubwa kwa lilchotokea kwa Dr Ulimboka ningepanda kabla sijachangia vema nijue chanzo gani kilichowafikisha hawa ndg zangu LHRC mabwepande. Kwa sasa niseme tuu -- kama serikali kwa kutumia usalama wa taifa au wengineo ndiyo inayohusika basi conclusively haistahili hata kidogo kuendelea kuwepo madarakani.


Hali kama hii haina tofauti na iliyowahi kutokea kwa akina Thom Mboya na Ouko huko kenya miaka kadhaa iliyopita. Hawa kama watu wengi mnavyoweza kukukmbua ni watu walioweza kusimamia haki hadharani bila kuogoapa lolote na wakiwa wamekamata madaraka makubwa ndani ya serikali ya Kenya. Hali kama hii iki achwa ikakomaa katika nchi yetu hata ufisadi ambao umekuwa uki itikisa nchi hii utokomaa kwa kiwango ambacho hatutaweza kuhimili amani tena.

Yaliyowahi kutokea kwa Kubeneye, Mwakyembe na Njama za kumtegeshea madawa Abdiel Mengi na sasa Daktari wetu kiongozi Ulimboka tukikaa kimya yataendela bila kukoma kwa kuwatumia wale ambao walitarajiwa wawe mfano wa kulinda amani ndio wanaotumika kuangamiza amani kwa maslahi ya CCM. Kwa uhakika hata sisi tuliyomo humu ndani ya CCM hatuko tayari tena kuona uzandiki wa kiasi hiki unataendeka.

Nitakoposikia kutoka kwa LHRC nitachangia yaliyoko moyoni.


TUSHIKAMANE BILA KUJALI VYAMA MPAKA KIELEWEKE
 
maumivu ya kichwa huanza taratibu,
ukiona moshi una fuka jua pana moto unawaka,
chonde chonde heri nusu shali kuliko shali kamili,
tulivumilia kule arusha, mkatuona wajinga,
tulivumilia tarime mkatuona wajinga,
kule bulyamhulu mliwafukia kaka zetu na baba zetu tukanyamaza mlituona wajinga,
haya za mwenio zikinyolewa zako tia maji,
tunisia,misri, libya,siria, ina maana hajajifunza?
 
SIDHANI KAMA HABARI HII NI YA KWELI! KAMA NI KWELI BASI

1-WATAKUA MADAKTARI WENZAKE WANACHEZA MCHEZO MCHAFU ILI WASIKILIZWE AU NCHI ISTAWALIKE

2- WATAKUA WANAHARAKATI WANATADUTA NJIA YA KUPATA PESA ZA WAZUNGU

3- WAFUASI WA CHAMA CHA SIASA WALIOMTEKA DC IGUNGA

siasa ina mambo mengi. anaweza kupakwa matope usoni na shati lake kumwagiwa damu ili aonekane kapigwa. anaweza hata kupelekwa icu na madaktari wenzake ili kuchochea mgomo na kuhamasisha wananchi. kuna watu wanataja bastola, sijui tunisia...... mbona mnaota ndoto za mchana. siyo raia wote wanaunga mkono mgomo wa madaktari. zaidi ya 85% wanaulaani

Una roho ngumu kweli Kusoma hujui hata picha huoni!? ni vema ukakaa kimya usitutafutie ban za lazima.
 
Bado zamu yako kwenda kutupwa Mabwepande

Sitoshangaa kwa hilo, kama uliwaua wale wafanyabiashara wa Mahenge, na leo mkataka kumuua Ulimboka huko huko Mabwe Pande.

Fanyeni mtakavyo kwani nyie ndio miungu ya Duniani, sisi ni sawa na sisimizi ambao mnaweza kutukanyaga mpendavyo.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
kazi wanayo Huwezi kushindana na Mungu hata siku moja lazima serkali ijue hilo.
 
Ndio maneno yao ya siku zote..ila sisi tumeshamjua mbaya wetu.
 
Mama yangu mama yangu.
Nilikuwa sijaingia humu....yaani mwili wote umekufa ganzi, machozi yanamwagika yenyewe. hakuna ninachoweza kufanya kutoka sasa.
Dah! dunia ina watu wabaya sana.
 
Mimi binafsi nilitegemea atasema hayo hayo hata kabla hajazungumza. Inasikitisha sana!
 
Duh, sasa imegeuka kwamba halikuwa Leaders club na sio nyumbani! Kweli hata Simbachawene hakufumaniwa!!!?
 
Back
Top Bottom