Katika pitapita zangu, nimedokezwa kuwa mfululizo huu wa migomo na maandamano ni kufanikisha mpango wa ki haini wa kutaka kuiangusha serikali iliyoko madarakani. Tulianza kushuhudia maandamano na kuambiwa kama nchi haitatawalika, nadhani ilitakiwa iwe kama yale ya arab spring. Lakini Mungu bariki mbinu hii ikabuma.
Ikaja mgomo wa wafanyakazi, nao ukabuma. Ukaja mgomo wa madaktari kupitia interns...huu ulisumbua kiasi mpaka ukang'oa vigogo kule wizarani lakini ukapita. Sasa mgomo huu mwingine kwa kisingizio kile kile cha hali bora za madaktari. Cha kushangaza wanaoshabikia zaidi migomo yote hii ni wale walioanzisha maandamano.
Nashawishika kuamini jamaa yangu aliyenin'gata sikio kuwa mpango huu unalenga kutaka kuifanya nchi isitawalike, nimedokezwa kuwa waalimu nao wameshawishiwa kugoma.
Sasa kama nadharia hii ni kweli, basi masikini dr. Uli jamaa zako wenyewe ndio wamekutia jiti. Na jamii iaminishwe kama ni jeshi la polisi and so serilkali ili umma woote uanze kuichukia serikali na kuiangusha. Dr. Uli adui yuko chumbani kwako, usimtafute mchawi.
I was just thinking very loud, sitaki nkuamini hata kidogo kam serikali kupitia jeshi la polisi could be dare to do this.