Kiufupi huo mjadala wa Doumbia utakuwa hauna mwisho mpaka siku anaondoka Simba kwa sababu zifuatazo:-
1. Ndio mshambuliaji wa kati wa kigeni wa mchovu kuliko wote aliyeletwa na Simba tokea Simba ianzishwe mwaka 1936. Na mbaya zaidi huyo mshambuliaji ameletwa wakati Simba inatimiza miaka 90 huku teknolojia ikiwa ikiwa ipo juu kiasi unaweza kumfuatilia mchezaji kwa urahisi sana na kujua uwezo wake. Na hata lingekuwa suala la usafiri kwenda kumuona mubashara kujua uwezo wake bado usafiri wa ndege sasa hivi upo advanced sana kulinganisha na miaka 90 iliyopita
2. Ndio mchezaji wa kwanza wa kigeni mwenye bahati ya kuvumiliwa na viongozi mashabiki, wapenzi na hata benchi la ufundi. Mpaka sasa ameshacheza mechi zaidi ya kumi akiwa na bao moja (Kagame Cup) na kugongesha mwamba mara mbili tu lakini kila mechi lazima apewe dakika uwanjani. Mpinzani wake kwenye nafasi anayocheza Mgunda kacheza tu mechi moja akatoa assist 1 na pre assist moja lakini mechi iliyofuata Mgunda akasugua benchi dakika zote 90 lakini Doumbya bado akapewa dakika chache za kucheza ili kutimiza lille lengo lazima acheze kila mechi.
3. Ni mchezaji anayeanguka mara kwa mara uwanjani bila sababu za msingi.
4. Ni mchezaji ambaye kwake kuzuia pasi zisifike kwa wachezaji wenzake au mpira usiingie kwenye goli la timu pinzani ni kawaida sana kwake.
5. Ni mshambuliaji wa kati wa mwisho lakini ukimuangalia wakati mchezo unaendelea uwanjani unaweza kudhani ni kiungo mshambuakiaji. Muda mwingi uwanjani huwa anacheza off position. Anawakimbia mabeki wakati wa timu pinzani kama anawaogopa vile na analikimbia boksi wakati ndio sehemu yake ya kazi aliyoajiriwa na Simba kuwa akae hapo kwa sababu kazi yake ni kufunga tu lakini yeye anajiongezea majukumu yasiyo ya msingi kwake.
6. Ni mmojawapo wa washambulijaji warefu zaidi katika ligi yetu na kila mtu angetemea kuwa angekuwa anafunga magoli mengi ya vichwa hasa ukizingatia Simba ina mawinga na mabeki wanaopiga krosi nyingi sana lakini amekuwa bure kabisa. Kuna wakati hata mabeki wafupi huwa wanaruka zaidi yake kuokoa mipra ambayo ungetemea yeye ndio angeifikia kwanza
7. Ni mshambuliaji mwenye umbo kubwa ambaye ilitegemewa awe anawalalia mabeki wa timu pinzani kuwatoa kwenye mstari ili afunge lakini yeye ndio hulaliwa na kutolewa kwenye mstari kirahisi na mabeki wa timu pinzani.
8. Ni mshambuliaji wa kati ambaye hawezi kufanya pressing ya maan kwa mabeki wa timu pinzani hivyo husababisha mabeki wa timu pinzani kufanya build up bila wasiwasi.
9. Ni mchezaji aliekuja kuvunja rekodi ya kukosa magoli ya wazi iliyowekwa na Yikpe.
10. Ndio mchezaji pekee pale Simba ambaye hakuna upande wa uongozi kati ya mwekezaji MO, wanachama chini ya Mangungu au Jayrutty unaotoka hadharani kujisifia kuwa wao ndio waliomleta.
Ni mtizamo.