TANZIA Kiongozi wa TLS Kagera, Seth Niyikiza akutwa amekufa nyumbani kwake

TANZIA Kiongozi wa TLS Kagera, Seth Niyikiza akutwa amekufa nyumbani kwake

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Mkoa wa Kagera, Seth Niyikiza amefariki dunia akiwa kajifungia ndani mwake.

Akithibitisha tukio hilo leo Jumatano Februari 26, 2025 Kamanda wa Polisi mkoani humo, Brasius Chatanda amesema mwili wa wakili huyo ulibainika baada ya mteja wake kwenda nyumbani kwake kufuatilia kwa nini haudhurii kesi yake mahakamani.

"Alilala, hakuonekana mpaka mteja wake amekuja mahakamani hamuoni... ndio akaamua kwenda nyumbani kufika akafanikiwa kusukuma geti, kuingia eneo la ndani akakuta kuna inzi...yaani kuna ‘movement’ ya inzi nyingi kwenye dirisha hali ambayo ilimshtua ikabidi awashirikishe majirani," amesema.

Amesema baada ya majirani kuona hali hiyo wakaamua kuvunja mlango na kumkuta amefariki na mwili umeharibika.

Kwa mujibu wa kaka yake, Laurent Seth mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera mjini Bukoba, wakisubiri kufanyiwa uchunguzi ili kujua chanzo cha kifo chake.

Ningependa kutoa Angalizo kwa Wanasheria au Mawakili, Mawakili wanapaswa kuwa Waangalifu sana kupita kiasi katika mienendo yao yote kabisa ya maisha yao ya kila siku.
Kwa uzoefu wangu binafsi, Mawakili ni miongoni mwa Watu ambao wamekuwa wakiwindwa Sana kama ndezi ili wahujumiwe kwa kudhuriwa.
Mawakili Watetezi wa Haki za watu na Wanaharakati mbalimbali ndio ambao wapo kwenye 'Top List' ya Watu ambao ni 'Most Wanted.' Mawakili wote wa kujitegemea wanapaswa walitambue jambo hili. Watu wengine wanaofutia kwenye list hiyo ni Waandishi wa Habari.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Sheria Tanganyika (TLS) Mkoa wa Kagera, Seth Jacob Niyikiza, amefariki dunia nyumbani kwake mjini Bukoba, ambapo mwili wake ulipatikana ukiwa umeketi kitini ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi, tayari ukiwa umeanza kuharibika.

Tukio hilo lilitokea baada ya mteja wake kumtafuta mahakamani bila mafanikio, na hatimaye kuelekea nyumbani kwake mnamo Februari 25, 2025, ambako aligundua hali isiyo ya kawaida.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda, amethibitisha kifo hicho, akieleza kuwa marehemu alikuwa hajajitokeza hadharani kwa muda, hali iliyozua shaka kwa mteja aliyekuwa akimtafuta.

"Mteja alipofika nyumbani kwa marehemu, hakupata wa kumfungulia. Alipofanikiwa kusukuma geti na kuingia, aliona kundi kubwa la nzi likiwa limezingira dirisha, jambo lililomtia hofu na kumfanya kuwajulisha majirani," amesema Kamanda Chatanda.

Baada ya majirani kufika, waliamua kuvunja mlango na kukuta mwili wa marehemu ukiwa umeketi kitini na tayari umeanza kuharibika.

"Nyumba ilikuwa imefungwa kwa ndani, hivyo kwa tafsiri ya haraka, hakuna dalili za kuhusika kwa mtu mwingine katika kifo hicho. Marehemu alionekana kujifungia, na ndani hakukuwa na viashiria vyovyote vya ukatili," ameongeza Kamanda.

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo hicho licha ya kutokuwepo kwa dalili za kudhuriwa.

Kwa upande wake, kaka wa marehemu, Laurent Niyikiza, amesema mazishi yanatarajiwa kufanyika Machi 1, huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera kwa uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo halisi cha kifo chake.
Chanzo na Habari leo
 
Kama asingekuwa kataa ndoa,angeweza kupata msaada wa haraka

Mimi ni nusu kataa ndoa lakin sitakubal kukaa peke yangu
 
  • Thanks
Reactions: G4N
aliamua kukaa mwenyewe ale bata? angekua hata na kijana hapo home..maana kuna vifo vingine ni hatari..
Mfano; Sukari na Presha imepanda usiku na upo mwenyew si ni hatari sana hii
 
Ukioa haufi.
Pengine mwanamke angekumalizia na kobilo au chepe la shingo kabisa.
Nawaza tu.
Kuna mume alikuwa amepatwa na kwikwi. Mkewe akakata kipande cha tikiti na kupaka sumu kisha akampatia mumewe. Mumewe alipokula hicho kipaande cha tikiti akaenda peponi.
 
Usomi mwingi haya ndo madhara yake.usije ukashangaa kiu ya maji ndo imemuua.kitu ambacho Kama kungekuwa na mtu mwingine angemtuma amletee
 
Eeehhh, kijana wa Misenyi, alifariki kijana wake some few years ago, nadhani kuna namna kiukoo wanachapana vyombo
 
Kuna mume alikuwa amepatwa na kwikwi. Mkewe akakata kipande cha tikiti na kupaka sumu kisha akampatia mumewe. Mumewe alipokula hicho kipaande cha tikiti akaenda peponi.
Rafiki wa nyoka pale Eden hanaga jema.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Ina maana hata Kaka yake hawasalimiani?
Au labda hawakai mji mmoja
Lakini hata simu basi?
Najiuliza maswali ya bila majibu aaaghh
 
Back
Top Bottom