TANZIA Kiongozi wa TLS Kagera, Seth Niyikiza akutwa amekufa nyumbani kwake

TANZIA Kiongozi wa TLS Kagera, Seth Niyikiza akutwa amekufa nyumbani kwake

MUNGU awape nguvu kipindi hiki kigumu ndugu na jamaa wa marehemu
 
Alafu kweli ukishindwa mtihani wa kukaa na mtu ambae hamna undugu kabisa(mke) huwezi shinda mtihani ya kukaa na ndugu..
1 .huaminiki kwa ndugu wenyewe hata wageni hupati kwa sababu huna mke.

2. Huoni haja ya kukaa na ndugu unaona wanakukera unajikuta unakaa kibachela.

3.Unaona gharama za uendeshaji ni kubwa kuhudumia watu ambao sio damu yako.

4.Kwa umri huo kufa peke yako ndani ni mashaka hata lifestyle yake inaonesha alikuwa mkaksi balaa.


Ila team kataa ndoa buana...Anyway Mungu ampumzishe salama.
 
POle sana Mwamba.

Mtu mzima kuishi peke yako Asubuhi hadi jioni, week hadi mwezi mpaka mwaka.

Unajua ukiwa kijana unajiona una nguvu, una pesa, life is easy but ́y frienf When you reach 50, my frienf you will regret
Wakifika 50 na hawana wake nao wanapataga changamoto kipata wenza..wanaogopwa na wanawake
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Mkoa wa Kagera, Seth Niyikiza amefariki dunia akiwa kajifungia ndani mwake.

Akithibitisha tukio hilo leo Jumatano Februari 26, 2025 Kamanda wa Polisi mkoani humo, Brasius Chatanda amesema mwili wa wakili huyo ulibainika baada ya mteja wake kwenda nyumbani kwake kufuatilia kwa nini haudhurii kesi yake mahakamani.

"Alilala, hakuonekana mpaka mteja wake amekuja mahakamani hamuoni... ndio akaamua kwenda nyumbani kufika akafanikiwa kusukuma geti, kuingia eneo la ndani akakuta kuna inzi...yaani kuna ‘movement’ ya inzi nyingi kwenye dirisha hali ambayo ilimshtua ikabidi awashirikishe majirani," amesema.

Amesema baada ya majirani kuona hali hiyo wakaamua kuvunja mlango na kumkuta amefariki na mwili umeharibika.

Kwa mujibu wa kaka yake, Laurent Seth mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera mjini Bukoba, wakisubiri kufanyiwa uchunguzi ili kujua chanzo cha kifo chake.
Tujifunze kiswahili fasaha sio kufa binadamu hafi. Sema Amefariki
wanaokufa ni wanyama kama mbuzi kondoo nk
 
Back
Top Bottom