Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Salamu wakuu,
Siku za karibuni kumekuwa na kundi kubwa la watu wanaopiga matarumbeta kunadi viongozi kwa munajili wa Jinsia. Watu hao wanasahau kabisa kwamba ubora wa kiongozi hautokani na Jinsia yake, Dini yake, Uzanzibari wake, Utanganyika wake, Sura yake nk. Bali ubora wa Kiongozi unatokana na uwezo wake na nia yake ya dhati ya kuwainua watanzania katika ngazi zote kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, Kiuchumi na Kijamii.
Bila kujali Jinsia ya kiongozi, Kama anayeonekana ana uwezo zaidi ni Mwanaume, anapaswa kupewa, Kama anayeonekana ana uwezo zaidi ni Mwanamke basi naye apewe.Lakini masuala ya Gender balance na kulazimisha watu wasio na uwezo kuongoza na kushika idara nyeti za taifa ni hatari sana, Na sote tumelishuhudia hilo kwa miaka minne iliyopita.
Wako viongozi wa Jinsia ya kike waliopambana ma kuonyesha uwezo wa uongozi kuzidi Jinsia ya kiume na wakaweza kupewa nyadhifa mbalimbali Tanzania na hata Duniani, Mfano walikuwepo kina Dr. Asharose Migiro, Dr. Mary Nagu, Prof. Tibaijuka nk. Viongozi hawa hawakubebwa kwa jinsia zao, Uzanzibari/utanganyika wao wala dini zao, bali waliingia kwenye Kinyang'anyiro na wenzao wa jinsia ME na wakashinda!
Hitimisho;
Viongozi hususan wa idara nyeti za umma, wapewe nyadhifa hizo kwa kuonyesha competency na uwezo usiopingika si kwa kuonyesha UZANZIBARI, JINSIA au DINI zao.