MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Siku mkipata akili mtaelewa.Unafikiri Trump kuutaka urais ni kwamba hana ukwasi?.
Sent from my TECNO CK7n using JamiiForums mobile app
😂😂😂😂😂😂😂😂😂Huyu kiongozi wetu ni mzigo sana,hapo ni saa tu tunayoiona huko kiunoni unaweza kuta kavaa shanga za 200mln.
Jamani Jamani Jamani!Hakuna hali inayokera na kuleta uhuzuni kwa kundi kubwa la watawaliwa kama kuona kiongozi wao akiishi maisha ya anasa huku wao wakizidi kutumbukia katika lindi la umasikini.
Tanzania kuna watu wengi sana wanaishi katika dhiki isiyo ya mfano, kama wewe ni mtafutaji wa mtaani au pembezoni mwa mji utakubaliana nami.
Vijana wengi sasa maisha wanayoishi yanakatisha tamaa maana yamejaa ufukara usio na mfano hapa usitegemee taasisi ya ndoa itakuwa na uhai, so usishangaee kuzidi kuyumba kwa taasisi ya ndoa na kuzidi kuimarika zaidi kwa biashara ya ngono.
Inapojitokeza kiongozi mkubwa wa nchi akiishi maisha ya anasa na kufuja mali kusiko na mfano inajenga taswira isiyo faa na inahuzunisha sana.
Kiongozi wa nchi anaye weka tu mkononi kitu chenye thamani ya milioni 100+ hii ni level ya juu sana ya ufujaji na kuishi maisha ya anasa yasiyo na mfano.
Saa tu millioni 100+ hizi pesa ni nyingi sana ambazo Watanzania wengi inaweza fika hata asilimia 80 wanakufa hawajawahi hata kuigusa wala kuiona sasa kiongozi mkubwa wa umma ambae ni picha ya anao watawala anaweka tu mkononi mil 100+ inasikitisha sana.
Kiongozi wa umma ambae haoni aibu kumpa mstaafu mzee gari la mamia ya mamilioni ya fedha kama zawadi ya birthday.
Kiongozi wa umma ambae haoni aibu kugawa pewa hovyo kwa timu za mpira wa miguu huku wananchi wake wakiishi maisha ya dhiki yasiyo na mfano.
Kiongozi anagawa pesa kama njungu za kuwajengea nyumba za kusali wakristo na waislam za mamilioni ya pesa.
Kiongozi wa umma ambae haoni tatizo kuzidi kutapanya hovyo pesa na kuishi maisha ya anasa anafikirisha sana namna anavyo watazama watu wake anao watawala.
Tanzania kuna umasikini napo sema umasikini namaanisha umasikini kweli kama ni mtu wa ofisini tu huwezi kuelewa level ya umasikini waliyo nayo Watanzania wengi inasikitisha sana.
Inasikitisha sana tena sana kuona kiongozi mkubwa wa umma anaiweka mkononi saa ya zaidi ya shilling million 100 na inanisikitisha zaidi pale ambapo kuna kundi la watu wanaona jambo hili ni sawa tu kufanywa.
[emoji1784][emoji1784][emoji1784][emoji706][emoji706][emoji706]kuwa na adabu basi uhuru usizidi mipaka.
↙saa inakwenda kuondoa maisha ya watu, hakuna kitu mbaya kama dhiki zako kuzifanya kama dhiki za watanzania wote!.Saa itawatoa roho 🐼
Hiyo Lodge tu ya kawaida hata wilayani watu wanazo acheni uongo uongo!Kwa kifupi tu na uone jinsi Mbowe alivyodhulimiwa na kupoteza mabilioni kwa kuwa kiongozi wa upinzani, sitaji zile chains of hotels, haka ni ka-hotel kadogo tu ka huko migombani kwa Mbowe:
Hoteli ya Aishi inayomilikiwa na Freeman Mbowe iliyopo Machame wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Uamuzi huu wa serikali ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro umekuja siku moja tangu Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa alipotangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbowe kwa madai kuwa lipo katika eneo la chanzo cha maji cha Mto Weruweru.
Ndio nimekwambia hiyo ni nyumba ka migombani huko kwao.Hiyo Lodge tu ya kawaida hata wilayani watu wanazo acheni uongo uongo!
Ukiniambia anatafuta sifa na heshima naweza kukubaliana na wewe, lakini Mbowe ha-hemei siasa ili apate kula, tayari ana pesa nyingi tangu utoto wake ameachiwa utajiri mkubwa. Anatafuta mambo mengine sio chakula kama wewe na wanasiasa wa ccm wanaopiga magoti ili wapate ubunge waweze kula na kujenga nyumba.Siku wewe nyumbu ukipata akili njoo ufute hii comment yako. Hakunaga mfanyabiashara anayefanya kazi za hasara. Siasa imempa Mbowe pesa nyingi sana. Hela za msaada kutoka Ulaya kwa ajili ya chama alifungulia kampuni yake binafsi ya magazeti ambayo wanunuzi wakuu ni nyie nyumbu. Mwaka 2010 alikikodishia chama chenu magari ya kampeni na kujilipa mamilioni kupitia ruzuku baadae. Hapo sijazungumzia mishahara ya ubunge na mafao. Na bado asali anayolambishwa. Mbowe hawezi kuacha siasa kwasababu inampa utajiri, sifa na heshima kwenye jamii. Halafu elewa pesa haijawahi tosha kwa mfanyabiashara yeyote akiwemo Mbowe. Hadi leo kina Bill Gates wanazisaka pesa.
Wewe nyumbu akili huna kabisa. Kwa hiyo akiachiwa urithi ndo hapaswi kufanya tena kazi. Baba yake Mbowe alikuwa tajiri ila haina maana warithi wake ndo watulie tu watumie tu kilichochumwa na wazazi. Akili za kingese kama zako ndo zinachangia waafrika tushindwe kurithishana utajiri. Tajiri wa kibongo akishakufa na utajiri wake ndo umekufa. Badili fikra zako wewe nyumbu.Ukiniambia anatafuta sifa na heshima naweza kukubaliana na wewe, lakini Mbowe ha-hemei siasa ili apate kula, tayari ana pesa nyingi tangu utoto wake ameachiwa utajiri mkubwa. Anatafuta mambo mengine sio chakula kama wewe na wanasiasa wa ccm wanaopiga magoti ili wapate ubunge waweze kula na kujenga nyumba.
Hii ni laana ya CCM. Ujinga wao ndiyo umefanya mpaka watu wa aina hii wapewe urais.Hakuna hali inayokera na kuleta uhuzuni kwa kundi kubwa la watawaliwa kama kuona kiongozi wao akiishi maisha ya anasa huku wao wakizidi kutumbukia katika lindi la umasikini.
Tanzania kuna watu wengi sana wanaishi katika dhiki isiyo ya mfano, kama wewe ni mtafutaji wa mtaani au pembezoni mwa mji utakubaliana nami.
Vijana wengi sasa maisha wanayoishi yanakatisha tamaa maana yamejaa ufukara usio na mfano hapa usitegemee taasisi ya ndoa itakuwa na uhai, so usishangaee kuzidi kuyumba kwa taasisi ya ndoa na kuzidi kuimarika zaidi kwa biashara ya ngono.
Inapojitokeza kiongozi mkubwa wa nchi akiishi maisha ya anasa na kufuja mali kusiko na mfano inajenga taswira isiyo faa na inahuzunisha sana.
Kiongozi wa nchi anaye weka tu mkononi kitu chenye thamani ya milioni 100+ hii ni level ya juu sana ya ufujaji na kuishi maisha ya anasa yasiyo na mfano.
Saa tu millioni 100+ hizi pesa ni nyingi sana ambazo Watanzania wengi inaweza fika hata asilimia 80 wanakufa hawajawahi hata kuigusa wala kuiona sasa kiongozi mkubwa wa umma ambae ni picha ya anao watawala anaweka tu mkononi mil 100+ inasikitisha sana.
Kiongozi wa umma ambae haoni aibu kumpa mstaafu mzee gari la mamia ya mamilioni ya fedha kama zawadi ya birthday.
Kiongozi wa umma ambae haoni aibu kugawa pewa hovyo kwa timu za mpira wa miguu huku wananchi wake wakiishi maisha ya dhiki yasiyo na mfano.
Kiongozi anagawa pesa kama njungu za kuwajengea nyumba za kusali wakristo na waislam za mamilioni ya pesa.
Kiongozi wa umma ambae haoni tatizo kuzidi kutapanya hovyo pesa na kuishi maisha ya anasa anafikirisha sana namna anavyo watazama watu wake anao watawala.
Tanzania kuna umasikini napo sema umasikini namaanisha umasikini kweli kama ni mtu wa ofisini tu huwezi kuelewa level ya umasikini waliyo nayo Watanzania wengi inasikitisha sana.
Inasikitisha sana tena sana kuona kiongozi mkubwa wa umma anaiweka mkononi saa ya zaidi ya shilling million 100 na inanisikitisha zaidi pale ambapo kuna kundi la watu wanaona jambo hili ni sawa tu kufanywa.
Mkuu,Naunga Mkono hoja Ukiwa kiongozi Hata Kama unapesa,, jifiche Kidogo Maana walioko Nyuma Wengi Hata Kula Ni Shida.