Kiongozi wa umma kumiliki vitu vya anasa huku kundi la unaowatawala wakipitia dhiki haijengi taswira nzuri

Kiongozi wa umma kumiliki vitu vya anasa huku kundi la unaowatawala wakipitia dhiki haijengi taswira nzuri

Hakuna hali inayokera na kuleta uhuzuni kwa kundi kubwa la watawaliwa kama kuona kiongozi wao akiishi maisha ya anasa huku wao wakizidi kutumbukia katika lindi la umasikini.

Tanzania kuna watu wengi sana wanaishi katika dhiki isiyo ya mfano, kama wewe ni mtafutaji wa mtaani au pembezoni mwa mji utakubaliana nami.

Vijana wengi sasa maisha wanayoishi yanakatisha tamaa maana yamejaa ufukara usio na mfano hapa usitegemee taasisi ya ndoa itakuwa na uhai, so usishangaee kuzidi kuyumba kwa taasisi ya ndoa na kuzidi kuimarika zaidi kwa biashara ya ngono.

Inapojitokeza kiongozi mkubwa wa nchi akiishi maisha ya anasa na kufuja mali kusiko na mfano inajenga taswira isiyo faa na inahuzunisha sana.

Kiongozi wa nchi anaye weka tu mkononi kitu chenye thamani ya milioni 100+ hii ni level ya juu sana ya ufujaji na kuishi maisha ya anasa yasiyo na mfano.

Saa tu millioni 100+ hizi pesa ni nyingi sana ambazo Watanzania wengi inaweza fika hata asilimia 80 wanakufa hawajawahi hata kuigusa wala kuiona sasa kiongozi mkubwa wa umma ambae ni picha ya anao watawala anaweka tu mkononi mil 100+ inasikitisha sana.

Kiongozi wa umma ambae haoni aibu kumpa mstaafu mzee gari la mamia ya mamilioni ya fedha kama zawadi ya birthday.

Kiongozi wa umma ambae haoni aibu kugawa pewa hovyo kwa timu za mpira wa miguu huku wananchi wake wakiishi maisha ya dhiki yasiyo na mfano.

Kiongozi anagawa pesa kama njungu za kuwajengea nyumba za kusali wakristo na waislam za mamilioni ya pesa.

Kiongozi wa umma ambae haoni tatizo kuzidi kutapanya hovyo pesa na kuishi maisha ya anasa anafikirisha sana namna anavyo watazama watu wake anao watawala.

Tanzania kuna umasikini napo sema umasikini namaanisha umasikini kweli kama ni mtu wa ofisini tu huwezi kuelewa level ya umasikini waliyo nayo Watanzania wengi inasikitisha sana.

Inasikitisha sana tena sana kuona kiongozi mkubwa wa umma anaiweka mkononi saa ya zaidi ya shilling million 100 na inanisikitisha zaidi pale ambapo kuna kundi la watu wanaona jambo hili ni sawa tu kufanywa.
Jamani Jamani Jamani!
Uchawi siyo Lazima ufuge Nyoka!

Ngoja nikwambie

Kwanza Rais wetu ni Mwanamke!

Kuvaa vizuri ni Sifa kwetu Sisi wananchi wake tuliomchagua!

Saa ya Milioni Mia mbona ni kitu kidogo sana!

Mbona hamuongelei Kamati za Harusi zinachangisha Tsh 150M kwa ajili ya kuozesha tu Binti wakati ndani ya wanafamilia kuna watu wanashindwa kumudu Mlo wa Siku moja?

Tuongee vitu vyenye kujenga bhana tusiongelee ati saa ys 100M!
By the way kwani hiyo saa ni ghali sasa?

Nenda kwenye gallery za saa ujue thamani ya saa

Arnold Shawzneeger hivi majuzi amevaa saa ya almost 1bn.

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Kwa kifupi tu na uone jinsi Mbowe alivyodhulimiwa na kupoteza mabilioni kwa kuwa kiongozi wa upinzani, sitaji zile chains of hotels, haka ni ka-hotel kadogo tu ka huko migombani kwa Mbowe:
Hoteli ya Aishi inayomilikiwa na Freeman Mbowe iliyopo Machame wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

aishi-hotel-mbowe-arusha
Uamuzi huu wa serikali ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro umekuja siku moja tangu Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa alipotangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbowe kwa madai kuwa lipo katika eneo la chanzo cha maji cha Mto Weruweru.
Hiyo Lodge tu ya kawaida hata wilayani watu wanazo acheni uongo uongo!
 
Sasa kama kiongozi huoni aibu ya kuvaa saa mkononi ya Tsh 100+ mkononi katikati ya lindi la umasikini wa watu wako waliokosa fursa ya mlo mmoja tu kwa siku.
Itakuwa mali za huyu kiongozi za uficho achilia mbali za wazi ni za matrilioni ya shilingi.
Ni kiwango cha juu kabisa cha dalili ya mtu asiyejali na wala asie na chembe ya utu.
 
Siku wewe nyumbu ukipata akili njoo ufute hii comment yako. Hakunaga mfanyabiashara anayefanya kazi za hasara. Siasa imempa Mbowe pesa nyingi sana. Hela za msaada kutoka Ulaya kwa ajili ya chama alifungulia kampuni yake binafsi ya magazeti ambayo wanunuzi wakuu ni nyie nyumbu. Mwaka 2010 alikikodishia chama chenu magari ya kampeni na kujilipa mamilioni kupitia ruzuku baadae. Hapo sijazungumzia mishahara ya ubunge na mafao. Na bado asali anayolambishwa. Mbowe hawezi kuacha siasa kwasababu inampa utajiri, sifa na heshima kwenye jamii. Halafu elewa pesa haijawahi tosha kwa mfanyabiashara yeyote akiwemo Mbowe. Hadi leo kina Bill Gates wanazisaka pesa.
Ukiniambia anatafuta sifa na heshima naweza kukubaliana na wewe, lakini Mbowe ha-hemei siasa ili apate kula, tayari ana pesa nyingi tangu utoto wake ameachiwa utajiri mkubwa. Anatafuta mambo mengine sio chakula kama wewe na wanasiasa wa ccm wanaopiga magoti ili wapate ubunge waweze kula na kujenga nyumba.
 
Acha mkuu yaogelee kwenye umaskini.Kwa maana ni ccm damu damu.
Hivyo kwao ccm ni mzazi wao.

Mabadiriko yapo Kwa waishio mjini ambapo ni wachache,lakini hayo ya vijijini hakuna kitu mkuu.
Acha wale,maana mtaji wao ndo hayo matutusa.
 
Ukiniambia anatafuta sifa na heshima naweza kukubaliana na wewe, lakini Mbowe ha-hemei siasa ili apate kula, tayari ana pesa nyingi tangu utoto wake ameachiwa utajiri mkubwa. Anatafuta mambo mengine sio chakula kama wewe na wanasiasa wa ccm wanaopiga magoti ili wapate ubunge waweze kula na kujenga nyumba.
Wewe nyumbu akili huna kabisa. Kwa hiyo akiachiwa urithi ndo hapaswi kufanya tena kazi. Baba yake Mbowe alikuwa tajiri ila haina maana warithi wake ndo watulie tu watumie tu kilichochumwa na wazazi. Akili za kingese kama zako ndo zinachangia waafrika tushindwe kurithishana utajiri. Tajiri wa kibongo akishakufa na utajiri wake ndo umekufa. Badili fikra zako wewe nyumbu.
 
Hakuna hali inayokera na kuleta uhuzuni kwa kundi kubwa la watawaliwa kama kuona kiongozi wao akiishi maisha ya anasa huku wao wakizidi kutumbukia katika lindi la umasikini.

Tanzania kuna watu wengi sana wanaishi katika dhiki isiyo ya mfano, kama wewe ni mtafutaji wa mtaani au pembezoni mwa mji utakubaliana nami.

Vijana wengi sasa maisha wanayoishi yanakatisha tamaa maana yamejaa ufukara usio na mfano hapa usitegemee taasisi ya ndoa itakuwa na uhai, so usishangaee kuzidi kuyumba kwa taasisi ya ndoa na kuzidi kuimarika zaidi kwa biashara ya ngono.

Inapojitokeza kiongozi mkubwa wa nchi akiishi maisha ya anasa na kufuja mali kusiko na mfano inajenga taswira isiyo faa na inahuzunisha sana.

Kiongozi wa nchi anaye weka tu mkononi kitu chenye thamani ya milioni 100+ hii ni level ya juu sana ya ufujaji na kuishi maisha ya anasa yasiyo na mfano.

Saa tu millioni 100+ hizi pesa ni nyingi sana ambazo Watanzania wengi inaweza fika hata asilimia 80 wanakufa hawajawahi hata kuigusa wala kuiona sasa kiongozi mkubwa wa umma ambae ni picha ya anao watawala anaweka tu mkononi mil 100+ inasikitisha sana.

Kiongozi wa umma ambae haoni aibu kumpa mstaafu mzee gari la mamia ya mamilioni ya fedha kama zawadi ya birthday.

Kiongozi wa umma ambae haoni aibu kugawa pewa hovyo kwa timu za mpira wa miguu huku wananchi wake wakiishi maisha ya dhiki yasiyo na mfano.

Kiongozi anagawa pesa kama njungu za kuwajengea nyumba za kusali wakristo na waislam za mamilioni ya pesa.

Kiongozi wa umma ambae haoni tatizo kuzidi kutapanya hovyo pesa na kuishi maisha ya anasa anafikirisha sana namna anavyo watazama watu wake anao watawala.

Tanzania kuna umasikini napo sema umasikini namaanisha umasikini kweli kama ni mtu wa ofisini tu huwezi kuelewa level ya umasikini waliyo nayo Watanzania wengi inasikitisha sana.

Inasikitisha sana tena sana kuona kiongozi mkubwa wa umma anaiweka mkononi saa ya zaidi ya shilling million 100 na inanisikitisha zaidi pale ambapo kuna kundi la watu wanaona jambo hili ni sawa tu kufanywa.
Hii ni laana ya CCM. Ujinga wao ndiyo umefanya mpaka watu wa aina hii wapewe urais.
 
Naunga Mkono hoja Ukiwa kiongozi Hata Kama unapesa,, jifiche Kidogo Maana walioko Nyuma Wengi Hata Kula Ni Shida.
Mkuu,

Kwa hiyo wewe tatizo lako si kiongozi kufuja pesa kwa anasa.

Akiweza kufuja pesa kwa anasa kisiri afuje tu.

Tatizo lako ni watu masikini anaowaongoza kuona kiongozi anafuja pesa kwa anasa.

Nimekuelewa vizuri hapo?
 
[QUOTE="So special, post: 49440262, member: 720861]
Tanzania kuna watu wengi sana wanaishi katika dhiki isiyo ya mfano, kama wewe ni mtafutaji wa mtaani au pembezoni mwa mji utakubaliana nami.

Tanzania kuna umasikini napo sema umasikini namaanisha umasikini kweli kama ni mtu wa ofisini tu huwezi kuelewa level ya umasikini waliyo nayo Watanzania wengi inasikitisha sana.[/QUOTE]

Nakuelewa sana mkuu.

Nimefanya kazi ya kuzunguka vijijini kwa miaka 5+.

Aisee tusichukulie poa, watanzania wengi wanaishi maisha yenye ugumu usioelezeka, si umasikini bali ufukara uliopitiliza ambao inafaa upatiwe jina jingine kabisa, naona kama jina la ufukara bado haliwatoshi kabisa! Yaani watu wanaiishi kuzimu wakiwa duniani halafu Kuna matajiri Simba na Yanga wanapewa mamilioni ya fedha yanayotokana na kodi za hao wanaolionja joto la jiwe!

Nikiona viongozi wanavyoleta utani na maisha ya watu halafu nikavuta picha za mambo niliyoyashuhudia huko vijijini huwa naumia sana.

Kuna watu wanalala sehemu ambazo huwezi kuamini kama binadamu anaweza kulala. Kuna familia zikinywa uji usio na sukari (wala chumvi) leo zinapitisha siku mbili, zikinywa na kesho ni anasa. Watu wa namna hii hata ukiwaletea stori za kujenga choo wanaona kama unawapigia makelele tu.

Inaumiza sana kiukweli.

Ndo maana nawaheshimu sana wapinzani, hata wawe na mapungufu milioni+, jitihada zao hata ziwe kiduchu kiasi gani bado zina thamani. Huwezi kuelewa vema kama hujazishuhudia tabu za watu huko ndanindani.
 
Wananchi wote ni sawa, ila wanasiasa wameongezewa kidogo mabaki ya usawa
 
Back
Top Bottom