Kiongozi wa upinzani wa Israel ataka kuuzuliwa Netanyahu

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
6,846
Reaction score
10,288
Kinara wa upinzani wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema wakati umefika wa kuiangusha serikali ya utawala huo inayoongozwa na Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu.

Yair Lapid amesema hayo na kuongeza kuwa, utawala wa Netanyahu unapasa kuangushwa kwa namna unavyoendeshwa ndivyo sivyo vita vya Gaza.
Lapid amesema wiki kadhaa zimepita, lakini Netanyahu na serikali yake wameshindwa kuwarejesha nyumbani kwa familia zao mateka wa Kizayuni walioko katika Ukanda wa Gaza.
Ametoa mwito kwa upinzani ndani ya utawala huo haramu kuungana kwa shabaha ya kulianguisha baraza la mawaziri la vita linaloongozwa na Netanyahu.
Hivi karibuni, Benny Gantz na Gadi Eisenkot, wajumbe wawili wa ngazi za juu wa baraza la mawaziri la vita la utawala wa Kizayuni walitangaza rasmi kujitoa kwenye baraza hilo. Aidha Hili Tropper ambaye ni mtu wa karibu na Gantz pia ametangaza rasmi kujitoa kwenye muungano unaounda serikali ya Netanyahu.
1718562889628.jpeg
Yair Lapid
Haya yanajiri siku chache baada ya msemaji wa jeshi katili la utawala haramu wa Israel, Daniel Hagari kuiambia kanali ya 12 ya televisheni ya Kizayuni kwamba haliwezi kuwarejesha nyumbani mateka kupitia operesheni ya kijeshi.
Katika siku za hivi karibuni, walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakiandamana kupinga na kulalamikia sera za Benjamin Netanyahu na kushindwa kwake kufikiwa mapatano ya kuachiwa huru mateka wa utawala wa kizayuni wanaoshikiliwa Ukanda wa Gaza.
 
View attachment 3018960Yair Lapid

Wafia dini mnatamani netanyahuu aondoke wala haondoki ni kipigo kwenda mbele kwa magaidi
 
Kwenye changamoto ndo unapata rafiki wa kweli na rafiki mnafiki, nchi iko kwenye vita badala ya kuwaza kutafuta mateka na amani yeye wao wanatafuta vyeo vya kisiasa. Mpaka uvamizi unatokea wao kama mawaziri wa vita walikuwa wapi?
 
Walishamwambia aache vita wakomboe mateka BIBI hataki.kILA WANACHOMSHAURI HATAKI !
 
Mnafikiri uongozi ni kushauriwa na mke na wahuni. Nchi inaongizwa kwa mipango, ambayo ni mjumuiko wa watu
 
Back
Top Bottom