Kiongozi wa Yanga atishia kuvuruga amani na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,476
Nimesikiliza kwa umakini maelezo ya wanaoitwa viongozi wa Baraza la Wazee na wa matawi ya Yanga.

Bila kusema mengi, kuna huyu jamaa mmoja ambaye sijamfahamu jina ila nadhani ni mmoja wa viongozi wa matawi alisema maneno yafuatayo "Sisi ni klabu kubwa, na ukubwa wetu unaakisi katika kila angle ya taifa hili. Sisi ndiyo waasisi wa uhuru wa nchi hii. Sisi ndiyo waasisi na ndiyo tunalinda amani ya nchi hii. Sasa ambacho tunawaambia wahuni wa mpira, wasitujaribu. Wanakwenda kwenye uchaguzi mwezi wa nane, wasitake tuuharibu uchaguzi wao. Tunakwenda kwenye uchaguzi wa nchi mwezi wa kumi, wasitake tuuharibu uchaguzi wa nchi hii"

Labda hizi ndiyo zile nyakati tulizoambiwa zitakuja maana naona kama kila mahali kumeanza kuchangamka.
 
Kuna jicho la tatu linaniambia hawa wahuni wameingiwa na kiwewe na wanaogopa gwaride la TREBLE ya Simba ya makombe ya CAFCC, NBC na CRDB Cup.

Wameanza vitisho wanajua Simba inachoenda kufanya katika gwaride la mwisho wa msimu hakijawahi kufanyika toka nchi hii imeumbwa.

Wanawaza wataishije na kadhia hii? Wataficha wapi sura zao? Vizazi vingapi vitapita kabla hawajapata nafasi ya kulipa mafanikio hayo ya Simba?

Wanajenga hofu ili mashabiki wa Simba wanywee. Wanataka hata Simba ikishinda makombe wasiwe na furaha. Wanataka drama zao zifunike kila kitu. Hawataki Simba ipite na gwaride pale Jangwani. Hizi ni sinema zetu za kina Mkojani kama alivyosema kiongozi mkuu wa mpira Tanzania.
 
We uliona wapi nyumba ambayo mkuu wa kaya ni mwanamke kukawa na utulivu?
 
Tanpol kazi kwenu....
Wanafanya michezo ya kitoto sana halafu wanachekewa tu. Hapa inabidi kuanza kuwadaka viongozi wote wanaotoa kauli kama hizi na kufungia kujishughulisha na soka viongozi wote wanaoimba kuwa hawachezi maana wameamua kutofuata sheria na taratibu za michezo na kujikita kwenye kuleta taharuki na sintofahamu.

Kama umeshtukia, Hersi kajiweka mbali na hili sakata.
 
Hakuna mashabiki wadwanzi kama wa Simba. Mnafurahi kwa kuwa kila kitu kipo upnade wenu si ndio?
Ule uhuni mliofanya tarehe 8 March mnaona mko sawa. Kibaya zaidi mkapata na kichaka cha kujifichia.
Na kwa taarifa yenu boramngekuja ile tarehe 8 mngeweza kufanya mapinduzi hata kushinda pia maana Yanga ingeingia kwa kujiona yeye ni mkubwa. Ila mechi yoyote mtakayocheza sasa na Ynaga mjiandae wa kumtupia lawama.
Sasa hivi sio kwamba hatuchezi ni HATUCHEZI NG'OOOO
 
Kucheza mtacheza tu ,zungukeni kama waokota makopo mwisho Arajiga atapuliza kipenga na Mpanzu mtamkaba tu 😂
 
Wanafanya michezo ya kitoto sana halafu wanachekewa tu. Hapa inabidi kuanza kuwadaka viongozi wote wanaotoa kauli kama hizi na kufungia kujishughulisha na soka viongozi wote wanaoimba kuwa hawachezi maana wameamua kutofuata sheria na taratibu za michezo na kujikita kwenye kuleta taharuki na sintofahamu.

Kama umeshtukia, Hersi kajiweka mbali na hili sakata.
Mbona uongozi wa juu wa Yanga haujaonge lolote. ?? inamaana wamebariki
 
Vitisho kama hivyo hua vinawezekana kama hao vyura idadi Yao ni 75% ya raia wote.
Wakati Hali halisi ni kama hivi
Tufanye hivi
Vyura ni 35%
Simba ni 35%
Wasio vyura wala Simba ni. 30%
Jumla ya raia 100%

Sasa hao Vyura 35% wanawezaje kutusumbua sisi Simba 35% +30% wasio vyura wala Simba ambao jumla yetu ni 65%?
Hawa vyura wachache hawawezi kutuondolea amani sisi Watanzania makini,Kwa hapa sisi Simba hatutahitaji hata Polisi wakawazuie.
Na hata waipopiga kura tutapiga sisi Simba na wasio Simba au vyura.
 
Nimesikiliza kwa umakini maelezo ya wanaoitwa viongozi wa Baraza la Wazee na wa matawi ya Yanga.

Bila kusema mengi, kuna huyu jamaa mmoja ambaye sijamfahamu jina ila nadhani ni mmoja wa viongozi wa matawi alisema maneno yafuatayo "Sisi ni klabu kubwa, na ukubwa wetu unaakisi katika kila angle ya taifa hili. Sisi ndiyo waasisi wa uhuru wa nchi hii. Sisi ndiyo waasisi na ndiyo tunalinda amani ya nchi hii. Sasa ambacho tunawaambia wahuni wa mpira, wasitujaribu. Wanakwenda kwenye uchaguzi mwezi wa nane, wasitake tuuharibu uchaguzi wao. Tunakwenda kwenye uchaguzi wa nchi mwezi wa kumi, wasitake tuuharibu uchaguzi wa nchi hii"
View attachment 3330330

Labda hizi ndiyo zile nyakati tulizoambiwa zitakuja maana naona kama kila mahali kumeanza kuchangamka.
Bora pachangamke tuondokane na wajinga
 
Back
Top Bottom