Kipa na Beki Kagera Sugar wasimamishwa kwa tuhuma ya kuhujumu dhidi Yanga SC

Kipa na Beki Kagera Sugar wasimamishwa kwa tuhuma ya kuhujumu dhidi Yanga SC

Don't hate the player, Hate the game...Don't be mad

Yanga waleee kuelekea nafasi yao
 
Hivi idadi ya magoli ya kufungwa timu kwa mechi huwa ni mangapi?Inawezekana kuna idadi kamili na ukishinda zaidi ya hayo utakuwa umehonga/hongwa.
 
Hao Takukuru upangaji wa matokeo ligi daraja la kwanza umewashinda huku ndo wataweza?
 
kwa mwendo huu mpira wetu unasafari ndefu wewe timu imezidiwa kila idara unakuja kufukuza wachezaji wawili.

hayo ndo matatizo ya makocha wetu kuona kwamba wanauwezo wa kupambana na timu kubwa bila kuzingatia mbinu za soka mwishowe ndo haya

nakukumbuka ile timu ya masau Bwire walipigwa goli 7(kama sikosei) na Yanga Jamaa baadaye anahojiwa anakwambia anashangaa Yanga walikua wanacheza nn uwanjani ati walikua wanarukaruka tu uwanjani,wewe umepigwa goli saba unasema ati wenzako walikua wanarukaruka kiwanjani baada ya kusema tumezidiwa mchezo tutajipanga vizuri kwa mechi ijayo..

Nlikua nampenda Julio na makocha wengine wa Ulaya neno I respect,Wakicheza na timu kubwa wataanza kwa kusema Naheshimu mpinzani wangu ni timu kubwa ila tutajitaidi kupambana kadri ya uwezo wetu

kikwetu sasa hata siku Kauzu fc/Faru jeusi akitokea anacheza na timu kubwa either Yanga/Simba/Azam/Mtibwa...nk utasikia kocha wao anajigamba kweli akija kufungwa naye atakwambia refa kapendelea au wachezaji wameuza game

Angekua mtu wa kufukuzwa Fabian Bartez akiwa Man utd angekua wa kwanza kufukuzwa manake alikua anafungwa hata magoli ya Doba

Tuache Mambo ya Kutafuta Mbuzi wa Kafara badala yake timu zetu zijiandae vizuri

Yale yale mambo ya taifa stars vs Algeria huku 2-2 tukajua wenzetu wale hata kwao tutawafunga matokeo yake tukala 7 kwao kocha aliona mapunguzu na kuyafanyia kazi na wala hakulaamu mchezaji yeyote
 
Yule kocha wa stand mzungu aliyeondoka kasema mengi sana kuhusu mambo hayo,

Hapa ukweli ni kuwa,
Simba, yanga, azam, zote zinatumia rushwa kutafuta ushindi na hawa Ndio wameuwa mpira,

TFF Ndio imeoza kama walipanga matokeo ya Ligi daraja la Kwanza sioni ajabu kwa haya kufanyika
 
Povu linakutoka mekula maharage ya wap ww ngoja tumwite ngwajima aje akuombee uyaharishe hayo maharage. Kila yanga akishinda amehonga mashabk wa simba km man u fujo tupu
 
We mbona umecheza mchezo 11 home 1 away umetoa rushwa Tff usha ona wap dunian lakn mashabk wa timu zngne Hawaongei ona aibu hata weweee looo aibu yako
 
Wakuu kama mnavyokumbuka timu ya Kagera Sugar ilifungwa na Yanga ya Dar jumla ya Goli 6 kwa 2. Na kama mnavyokumbuka Yanga imekuwa ikishutumiwa kununua ama timu nzima au baadhi ya wahezaji ili kurahisha mazingira ya ushindi wa kimbunga.
Taarifa zinazosomwa Azam TV zinasema kuwa Wachezaji wawili wa Kagera Sugar, Husein Sharifu 'Casillas Munyama' na Erick Kyaruzi wamesimamishwa na kuondolewa kambini.Wanatuhumiwa kupewa mlungura na Yanga katika kipigo cha 6-2.

TAKUKURU fanyika kazi hii timu inatia aibu Taifa.
c.c Makoye Matale na sembo
1. Yanga imekuwa ikishutumiwa....= Inadhaniwa kwamba Yanga ..... = Inawezekana kwamba Yanga ina....
Je, kudhani ama kuwezekana ndiyo kufanyika? Mfano: Inawezekana/inadhaniwa/ kwamba mtoa mada ametumwa na wapinzani wa Yanga kuikashifu ni sawa na kuwa mtoa mada ametumwa na wapinzani wa Yanga?
2. Taarifa zinazosomwa na Azam TV zinasema kuwa = Azam TV inatangaza kuwa = Kwa mujibu wa Azam TV
Je, kila kinachotangazwa na Azam TV ni sahihi na makini? Mbona Azam TV hiyohiyo inasifia chapa (brand) moja ya bidhaa kuwa ndiyo bora kuliko zote, wakati huohuo ikitangaza chapa nyengine ya bidhaa hiyohiyo kuwa nayo bora kuliko zote? Na ndivyo ilivyo kwa vyombo vyote vya habari. Muhimu kwa vyombo vya habari ni kutangaza biashara ili waingize fedha, si usahihi wa tangazo lenyewe. Kadhalika ukweli kwa vyombo vya habari ni kuwa habari waliyoitangaza imesemwa na mtu waliyemnukuu, hata kama amesema uongo. Wanachopigania wao ni kuwa wa kwanza kutoa habari husika, ndio maana kihabari hizi ni zama za kushindana kwa habari motomoto (breaking news).
3. Wachezaji wawili wa Kagera Sugar wamesimamishwa na kuondolewa kambini = Wachezaji wawili wa Kagera Sugar wameonekana si muhimu kwa mechi zinazofuata = Hawatakiwi kuwa na timu kwa hivi sasa.
Je, timu yenye uhakika kwamba mchezaji ameihujumu itaishia kumwondoa kambini tu? Na je, timu isiyo na uhakika kuwa mchezaji ameihujumu itakuwa tayari kukosa huduma zake kwa kutomchezesha, au itaendelea naye hata kama hatacheza mpaka itapojiridhisha? Je, ni kweli wachezaji hao waliicheza chini ya kiwango mechi hiyo? Je, kucheza mechi chini ya kiwango pekee kunatosha kuthibitisha kwamba mchezaji amehujumu? Je, haiwezekani mchezaji kuhujumu timu kwa kucheza chini ya kiwango na bado timu yake ikashinda? Mbona Tanzania hatusikii kesi kama hizo? Je wachezaji wawili wanatosha kiufungisha timu mabao 6-2?
Nionavyo: (1) Kagera Sugar inatafuta kisingizio cha kufungwa 6-2 uwanjani kwao, Casillas na Kyaruzi ndio kondoo wa kafara (2) Kisaikolojia, ni vyema Kagera Sugar wajiamini kwamba hawatafungwa tena sita. Casillas na Kyaruzi ndio 'placebo', yaani zile dawa zisizo na uwezo wowote wa kutibu lakini bado ni tiba kwa anayeziamini (3) Hakuna tokeo kubwa lolote lisilofuatiwa na nadharia ya njama (conspiracy theory). Kagera kufungwa sita kwao ni tukio kubwa. Kwamba Casillas na Kyaruzi wamehongwa ni conspiracy theory mojawapo. Yanga kufunga mabao mengi kwenye Ligi wakati wenzake wakisumbukia angalau kamoja ni habari kubwa. Kwamba wanahonga ni conspiracy theory mojawapo. (4) Usiposema, utaulizwa. Kuliko kusakamwa na 'kulikoni' mfululizo za waandishi, ni vyema uongozi na benchi la ufundi la Kagera Sugar wakajibu sasa na moja kwa moja. Casillas na Kyaruzi ndiyo jibu la haraka, ndiyo ngao endelevu dhidi ya 'kulikoni' hizo.
Angalau Azam walimpeleka TAKUKURU Aggrey Morris walipomtuhumu kuhongwa na Simba. Kagera Sugar wameokolewa na juhudi binafsi za mtoa mada kuwapeleka Casillas na Kyaruzi TAKUKURU. Hongera mtoa mada!
 
Golikipa wa kwanza alifungwa goli 3, wakabadilisha mwingine naye akapigwa 3.... sasa hapo wote walihongwa? kama ndivyo wangesimamishwa magolikipa wote wawili kwani wote walipigwa 3.
Kuna goli analaumiwa kipa kwa uzembe wake pia kuna goli analaumiwa beki au mabeki tofautisha na ujiongeze kiakiri
 
Naona watu humu mnalaumu simba kwa kutemwa wachezaji wa kagera,kagera wamechukua hatua kwa watu wao.simba tunahusika vipi? Huyo beki na kipa wake tulijaribu kuhoji hapa tukapigwa matusi ya kutosha.Yanga kashinda mechi nyingi kwanini watu wahoji juu ya kagera na hao wanaotegeana kuokota mpira.
 
Tusibishe kama vile hili jambo si kweli na wakat tunafaham kabisa limekuwepo sana tu. Mara nying makocha na wachezaj huhusika. Na matokeo yake tunayapata vizuri tunapocheza na timu za nje. Huwa tunajikuta kila siku tunakufa kiume. Na kuwa best losers kwenye makund yetu mwishon ku lose kabisa.
 
Naona watu humu mnalaumu simba kwa kutemwa wachezaji wa kagera,kagera wamechukua hatua kwa watu wao.simba tunahusika vipi? Huyo beki na kipa wake tulijaribu kuhoji hapa tukapigwa matusi ya kutosha.Yanga kashinda mechi nyingi kwanini watu wahoji juu ya kagera na hao wanaotegeana kuokota mpira.

Sio mechi ya Kagera tu hata mechi ya Toto wamchangani mnadai Yanga amenunua hata Simba alivyofungwa na Yanga msimu uliopita mlisema Yanga amenunua mechi
 
Hawa Yanga wamezoea kamchezo haka kula mlungura michezoni,, utaona kila Wakicheza na Simba ni lazima Simba wacheze pungufu baada ya refa kupewa mlungura na hawa Yanga,,
Mechi ikiwa ngumu kwao basi ujue timu pinzani haitamaliza ikiwa kamili ni lazima wacheze pungufu au Yanga ni lazima wapewe penarti.

Ndiyo maana hawakufua dafu mbele ya Tp mazembe,,Mo bejaiya,,madiema kote huko walichezea kichapo tu.
 
Mbona kelele nyingi hivi nyie wa hapa hapa mmekuwa kimya takribani miaka 3 na heshima juu nikawaona watu kweli .Sasa kuongoza ligi kwa point 5 mnaanza kusimbua watu hii ligi bado changa sana kila msimu tunapenda mtangulie kwanza .Haina haja yanga kusajili wachezaji wa bei kubwa kama kuna uwezekano wa kununua mechi kwa bei nafuu upo.Fikiria kwanza .Simba wanarudisha nyuma soka la Tanzania kwa imani mbovu.take my world .
 
Golikipa wa kwanza alifungwa goli 3, wakabadilisha mwingine naye akapigwa 3.... sasa hapo wote walihongwa? kama ndivyo wangesimamishwa magolikipa wote wawili kwani wote walipigwa 3.


Kwa maoni yangu hizi propaganda za baadhi ya wapenzi na mashabiki wa Simba dhidi ya YANGA wakati mwingine ni za 'kitoto' sana.... Hata ile mechi kati ya YANGA na SIMBA ile kamati sijui Bodi ya Ligi (yenye mashabiki tisa wa Simba) nayo ilifanya maamuzi ya 'kipuuzi' kwa kutengua kadi nyekundu ya Mkude....Mchezaji anamtukana ovyo refa uwanjani halafu bado unatengua kadi????? Duh....
 
Wakuu kama mnavyokumbuka timu ya Kagera Sugar ilifungwa na Yanga ya Dar jumla ya Goli 6 kwa 2. Na kama mnavyokumbuka Yanga imekuwa ikishutumiwa kununua ama timu nzima au baadhi ya wachezaji ili kurahisha mazingira ya ushindi wa kimbunga.
======================

Uongozi wa Kagera Sugar umewasimamisha wachezaji wake wawili golikipa Hussein Sharif ‘Casillas’ na beki Erick Kyaruzi kwa tuhuma za kuihujumu timu wakati wa mchezo wa liopoteza kwa kufungwa magoli 6-2.

Katibu Mkuu wa klabu hiyo Hamisi Madaki amethibisha kuwasimamisha wachezaji hao kwa muda usiojulikana kwa ajili ya kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zinazowakabili.

“Tunaendelea na uchunguzi kwasababu kunaonekana kulikuwa na hujuma katika mechi yetu na Yanga kwahiyo tumeona tuendelee na uchunguzi na tumeona wakae kando wakati tunaendelea na uchunguzi huo.”

“Aina ya magoli tuliyofungwa kila mtu aliyaona na yanatia wasiwasi mkubwa. Suala sio idadi ya magoli suala ni aina ya amagoli mtu aliayofungwa, hata kama ni goli moja lakini kama linatia wasiwasi lazima tuchukue hatua.”

“Makosa ya namna ile hatukuridhika nayo ndiyo maana tunafanya uchunguzi. Hata beki goli alilofungisha unaona dhahiri kwamba halikupashwa kuwa goli ndiyo maana tunafanya uchunguzi.”

“ nikiwa kama Mtendaji mkuu wa klabu, hiyo taarifa sina sisi tumewasimamisha na hata barua tulizowaandikia tumesema tumewasimamisha . Suala la kuwaondoa kabisa hilo siwezi kulisemea, taarifa nilitoa mbele ya wachezaji na benchi la ufundi baada ya kukaa viongozi na benchi la ufundi tulikubaliana kuwasimamisha.”

“Tumewasimamisha kwa muda usiojulikana mpaka tukamilishe uchunguzi, hii si mara ya kwanza watu wanasahau historia, tumeshawahi kusimamisha wachezaji na kuwafukuza kabisa hapo kabla.”

Katika mchezo huo, Hussein Sharif alifungwa magoli matatu kipindi cha kwanza kabla ya kufanyiwa mabadiliko kumpisha David Burhani ambaye pia alifungwa magoli matatu.

Kyaruzi yeye alirudisha pasi fupi kwa golikipa wake ambapo Donald Ngoma aliuwahi mpia huo na kufunga bao.

TAKUKURU fanyika kazi hii timu inatia aibu Taifa.
c.c Makoye Matale na sembo
Timu zote zilizofungwa na Yanga magoli mengi (kuanzia 2-0) since 2015/2016 league zichunguzwe na TAKUKURU, maana kuna mazingira ya Rushwa!!!
 
Back
Top Bottom