Kipa na Beki Kagera Sugar wasimamishwa kwa tuhuma ya kuhujumu dhidi Yanga SC

Kipa na Beki Kagera Sugar wasimamishwa kwa tuhuma ya kuhujumu dhidi Yanga SC

Umetisha mkuu kuna watu humu kila yanga ikishinda basi imehonga, mkia akishinda basi kwa uwezo wake.... Sasa sijui yanga ina muhimu gani kununua wachezaji wa ghali na kulipa mishahara mikubwa ikiwa inaweza kununua mechi
Yanga nao wachunguzwe walihongwa na Stand United Chama la Wana, wakafungwa 1-0. Hii haikubaliki!!!!
 
Hizi huwa ni story tu kiongozi hakuna mtu aliyewahi kuthibitisha kuhongwa lazima tuwe wa kweli team ya yanga nayo ipo vizuri kiuchezaji, wanawachezaji mahiri kabisa, tujaribu kuwa wa kweli katika kukubari matokeo

wangekuwa wazuri wasingeshindwa kufunga goli kama hizo au zaidi ya hizo timu iliyopungukiwa mchezaji tokea kipindi cha kwanza,hawa ni wabakaji wa soka letu,mara nyingi sana hutuhumiwa lakini tuhuma hupotezewa
 
Chaneta FC wao walichozowea ni Ubingwa Wa Kununua tu!! Fine! Nyie Wakimataifa au Wakimanunuzi???
Sasa Napata Picha Ya Kwanini Manji Anawadai Chaneta FC bilioni 11 ambazo Kashindwa Kusema anawadai Kwa Njia gani...!!!

Kumbe Hasemi anawadai Kivipi Kwasababu Zilitumika Kuhonga Makipa na Mabeki.
 
Hv kule IPIELO Maniyu wamemsimamisha nani Kweli wakuu wangu??? baada ya kale kakipigo kadogo toka Cheisiii!!! ni Baily au Blind??? au De gea
Mkuu smalling kasimamishwa na barua kaandikiwa kabisa mpaka uchunguzi utakapokamilika hahaaaa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Rais wa timu ya kubwa ya Marseilles aliwahi kufungwa jela na timu hiyo kushushwa daraja.
Tafadhali, kama tunalitakia taifa mema tuhakikishe waliojihusisha na dhambi hii wanaadhibiwa pia.
 
Simba haijawahi hawa kuwaziwa kununua mechi, lakini kwa nini Yanga tu. Kagera sugar sio wajinga kusimamisha wachezaji
Mkuu kama huna data ni afadhali utulie. Hata hivyo, mti wenye matunda ndio hupondwa mawe!

Nanukuu:

'KIUNGO wa Simba, Ulimboka Mwakingwe, juzi alipandishwa kizimbani mkoani Morogoro ikiwa ni baada ya kuhojiwa na maofisa wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru).

Ulimboka anatuhumiwa kujaribu kumhonga aliyekuwa kipa wa Mtibwa Sugar, Shaaban Kado, miezi kadhaa iliyopita ili aisaidie Simba kupata ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina na timu hizo uliochezwa mjini Morogoro. Hii ni mara ya pili kuhojiwa na Takukuru.
'

Source: http://www.dullonet.com/sports/2011/12/24/ulimboka-mwakingwe-apandishwa-kizimbani/
 
mkuu mleta mada acha hizo bana ur one of the respected members wa jf hii sio level yako
 
mkuu mleta mada acha hizo bana ur one of the respected members wa jf hii sio level yako
Mikia fc wametangulia kwa baiskeli ya miti, wameshakaribia mlima huku nyuma wakiona treni la mwendokasi linakuja ni lazima waweweseke.
 
Penye uzia penyeza rupia.
Ndio soka la bongo hili.
 
Simba haijawahi hawa kuwaziwa kununua mechi, lakini kwa nini Yanga tu. Kagera sugar sio wajinga kusimamisha wachezaji
unakumbuka kesi ya Ulimboka alivyo kamatwa kule morogoro akitaka kumpa hela Shabani kado.?
 
Simba haijawahi hawa kuwaziwa kununua mechi, lakini kwa nini Yanga tu. Kagera sugar sio wajinga kusimamisha wachezaji
Hajawahi vipi, kessy akiwa mtibwa mlimpa nini??? Acheni kujisahaulisha
 
Hiv unampeleka yanga kwenye nyasi bandia then unategemea ufungwe moja?? Kipindi kile ilikuwa taabu coz uwanja ulikuwa kama shamba. Mchawi wenu kagera sugar ni uwanja wenu. Ngoja simba nao waje hapo wakupe tano tuone
 
hili nalo litapita kama lilivyopita la upangaji matokeo kupanda ligi kuu la geita na wale wenzao.................tz ya viwanda
 
Mkuu kama huna data ni afadhali utulie. Hata hivyo, mti wenye matunda ndio hupondwa mawe!

Nanukuu:

'KIUNGO wa Simba, Ulimboka Mwakingwe, juzi alipandishwa kizimbani mkoani Morogoro ikiwa ni baada ya kuhojiwa na maofisa wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru).

Ulimboka anatuhumiwa kujaribu kumhonga aliyekuwa kipa wa Mtibwa Sugar, Shaaban Kado, miezi kadhaa iliyopita ili aisaidie Simba kupata ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina na timu hizo uliochezwa mjini Morogoro. Hii ni mara ya pili kuhojiwa na Takukuru.
'

Source: http://www.dullonet.com/sports/2011/12/24/ulimboka-mwakingwe-apandishwa-kizimbani/
hahaha jamaa alikua anajitoa ufahamu.
 
hahaha jamaa alikua anajitoa ufahamu.
Mkuu JF naiheshimu sana, huwa siandiki mambo makubwa kama haya bila ushahidi. Jamaa kwa makusudi alimua kutokumbuka. Yapo na mengine mengi, nimelitoa hili moja tu ili akae kimya.
 
Wakuu kama mnavyokumbuka timu ya Kagera Sugar ilifungwa na Yanga ya Dar jumla ya Goli 6 kwa 2. Na kama mnavyokumbuka Yanga imekuwa ikishutumiwa kununua ama timu nzima au baadhi ya wachezaji ili kurahisha mazingira ya ushindi wa kimbunga.
======================

Uongozi wa Kagera Sugar umewasimamisha wachezaji wake wawili golikipa Hussein Sharif ‘Casillas’ na beki Erick Kyaruzi kwa tuhuma za kuihujumu timu wakati wa mchezo wa liopoteza kwa kufungwa magoli 6-2.

Katibu Mkuu wa klabu hiyo Hamisi Madaki amethibisha kuwasimamisha wachezaji hao kwa muda usiojulikana kwa ajili ya kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zinazowakabili.

“Tunaendelea na uchunguzi kwasababu kunaonekana kulikuwa na hujuma katika mechi yetu na Yanga kwahiyo tumeona tuendelee na uchunguzi na tumeona wakae kando wakati tunaendelea na uchunguzi huo.”

“Aina ya magoli tuliyofungwa kila mtu aliyaona na yanatia wasiwasi mkubwa. Suala sio idadi ya magoli suala ni aina ya amagoli mtu aliayofungwa, hata kama ni goli moja lakini kama linatia wasiwasi lazima tuchukue hatua.”

“Makosa ya namna ile hatukuridhika nayo ndiyo maana tunafanya uchunguzi. Hata beki goli alilofungisha unaona dhahiri kwamba halikupashwa kuwa goli ndiyo maana tunafanya uchunguzi.”

“ nikiwa kama Mtendaji mkuu wa klabu, hiyo taarifa sina sisi tumewasimamisha na hata barua tulizowaandikia tumesema tumewasimamisha . Suala la kuwaondoa kabisa hilo siwezi kulisemea, taarifa nilitoa mbele ya wachezaji na benchi la ufundi baada ya kukaa viongozi na benchi la ufundi tulikubaliana kuwasimamisha.”

“Tumewasimamisha kwa muda usiojulikana mpaka tukamilishe uchunguzi, hii si mara ya kwanza watu wanasahau historia, tumeshawahi kusimamisha wachezaji na kuwafukuza kabisa hapo kabla.”

Katika mchezo huo, Hussein Sharif alifungwa magoli matatu kipindi cha kwanza kabla ya kufanyiwa mabadiliko kumpisha David Burhani ambaye pia alifungwa magoli matatu.

Kyaruzi yeye alirudisha pasi fupi kwa golikipa wake ambapo Donald Ngoma aliuwahi mpia huo na kufunga bao.

TAKUKURU fanyika kazi hii timu inatia aibu Taifa.
c.c Makoye Matale na sembo

TAKUKURU tia ndani wakora hao!!
 
Back
Top Bottom