Kipa na Beki Kagera Sugar wasimamishwa kwa tuhuma ya kuhujumu dhidi Yanga SC

Kipa na Beki Kagera Sugar wasimamishwa kwa tuhuma ya kuhujumu dhidi Yanga SC

Wakuu kama mnavyokumbuka timu ya Kagera Sugar ilifungwa na Yanga ya Dar jumla ya Goli 6 kwa 2. Na kama mnavyokumbuka Yanga imekuwa ikishutumiwa kununua ama timu nzima au baadhi ya wachezaji ili kurahisha mazingira ya ushindi wa kimbunga.
======================

Uongozi wa Kagera Sugar umewasimamisha wachezaji wake wawili golikipa Hussein Sharif ‘Casillas’ na beki Erick Kyaruzi kwa tuhuma za kuihujumu timu wakati wa mchezo wa liopoteza kwa kufungwa magoli 6-2.

Katibu Mkuu wa klabu hiyo Hamisi Madaki amethibisha kuwasimamisha wachezaji hao kwa muda usiojulikana kwa ajili ya kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zinazowakabili.

“Tunaendelea na uchunguzi kwasababu kunaonekana kulikuwa na hujuma katika mechi yetu na Yanga kwahiyo tumeona tuendelee na uchunguzi na tumeona wakae kando wakati tunaendelea na uchunguzi huo.”

“Aina ya magoli tuliyofungwa kila mtu aliyaona na yanatia wasiwasi mkubwa. Suala sio idadi ya magoli suala ni aina ya amagoli mtu aliayofungwa, hata kama ni goli moja lakini kama linatia wasiwasi lazima tuchukue hatua.”

“Makosa ya namna ile hatukuridhika nayo ndiyo maana tunafanya uchunguzi. Hata beki goli alilofungisha unaona dhahiri kwamba halikupashwa kuwa goli ndiyo maana tunafanya uchunguzi.”

“ nikiwa kama Mtendaji mkuu wa klabu, hiyo taarifa sina sisi tumewasimamisha na hata barua tulizowaandikia tumesema tumewasimamisha . Suala la kuwaondoa kabisa hilo siwezi kulisemea, taarifa nilitoa mbele ya wachezaji na benchi la ufundi baada ya kukaa viongozi na benchi la ufundi tulikubaliana kuwasimamisha.”

“Tumewasimamisha kwa muda usiojulikana mpaka tukamilishe uchunguzi, hii si mara ya kwanza watu wanasahau historia, tumeshawahi kusimamisha wachezaji na kuwafukuza kabisa hapo kabla.”

Katika mchezo huo, Hussein Sharif alifungwa magoli matatu kipindi cha kwanza kabla ya kufanyiwa mabadiliko kumpisha David Burhani ambaye pia alifungwa magoli matatu.

Kyaruzi yeye alirudisha pasi fupi kwa golikipa wake ambapo Donald Ngoma aliuwahi mpia huo na kufunga bao.

TAKUKURU fanyika kazi hii timu inatia aibu Taifa.
c.c Makoye Matale na sembo
Kocha anajihami kibarua chake, hana lolote. Hawajazoea capet
 
Mkuu mashabiki wengi wa simba ni shida huwa wanaamini simba ndo inapaswa kushinda game tu, ikishinda yanga kahonga.... Simba anaongoza lingi sasa umesikia shabiki wa yanga akipiga kelele simba ananunua mechi au anapendelewa!?
Kama Yanga wananua mechi, basi watuonyeshe risiti ya EFD original maana ni kosa kununua bidhaa na ukashindwa kutoa risiti. Simba waanze kuonyesha risiti kwa mechi mbili za msimu uliopita kwa kuwa mechi zao walituuzia.[emoji12]
 
mbona kama leo pia goli la pili na tatu kuna kauzembe watafukuza nani sasa??

final result Kagera 2 Azam 3 pale pale kaitaba
 
Haya na leo wamefungwa wafukuzane tena
Kagera hawajui ule uwanja wao kwa sasa ni mzuri, na nyasi za plastic zikiwa kwenye baridi utazifurahia mwenyewe kwa hiyo kwa timu za kimataifa kama yanga na Azam zitawapiga sana tuu
 
1. Toto African 0 - Yanga SC 2.

2. Kagera Sugar 2 - Yanga SC 6

3. Yanga SC 4 - JKT Ruvu 0.

Takukuru wafanyie kazi pia na mechi iliyofuatia ya JKT ruvu, huenda yanga pia walitoa rushwa wakashinda goli 4 mtungi. Huenda YANGA hawana uwezo wa kushinda goli 10 ndani ya mechi 2
 
Haya na leo wamefungwa wafukuzane tena
Kagera hawajui ule uwanja wao kwa sasa ni mzuri, na nyasi za plastic zikiwa kwenye baridi utazifurahia mwenyewe kwa hiyo kwa timu za kimataifa kama yanga na Azam zitawapiga sana tuu
Daima mbele nyuma mwiko:
marudiano na Kagera tunashinda goli8 ili tuwathibitishie watani zetu kwamba hakuna figisu bali ni uwezo tu mkubwa wa kimataifa
 
uploadfromtaptalk1477681081816.jpg

Mashabiki hawamtaki kocha
 
mi sijawahi kuona mechi ya kijinga kama hiyo. kipa anamtemea forward mpira zaidi ya mara mbili. hao wanastahili kufungiwa .
 
Back
Top Bottom