KMC jana aliyeharibu ni Beki namba mbili 2. Kikosi kilikuwa vizuri tu. Na huyo No. Mbili kacheza hadi mwisho.
Ile Sub, ya kipindi cha pili iliyowatoa wachezaji watatu wa KMC ilikuwa ya mipango.
Uwesu Uwesu na wale wawili waliupiga mwingi sana mi walivyo tolewa tu nikacheka na kuwaambia jirani zangu kuwa Yanga ishashinda.
Mmoja ya waliotolewa alikuwa anatikisa kichwa kwa kushangaa kwanini anatoka.
Ndio maana yule msemaji wa KMC anayeropoka kwa jazba wakicheza na Simba jana alikuwa Kimyaaaa.
Nawaambieni Yanga mtakuwa mnachukua makombe yote ya ndani kwa muda huu. Ila mkienda kimataifa mtachapika hadi mkome.
Hao Watunisia watawakaanga hapahapa kwa mkapa kwakuwa refa sio mtanzania.
Imefikia mahali Yanga inabebwa na karibu nchi nzima.
Ni ajabu na kweli.