Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni Mkwe wangu kabisa huyu kwani Kazaa Mtoto mmoja na Mwanangu (Mtoto wa Marehemu Kaka John) aitwae Buzo aishie Kibamba Dar es Salaam.Wakati watani wa jadi wa soka la Bongo, Simba na Yanga, wakitarajiwa kushuka dimbani katika dabi inayonadiwa kwa kaulimbiu ya HAINA KIPENGELE, kuna taarifa mbaya na ya huzuni kwa nyota wa zamani wa timu hizo mbili. Huyu ni Mabruki Doyi Moke, kipa wa zamani wa Simba na Yanga aliyeishi kwenye mitaa ya Kariakoo kuanzia 1999 hadi 2003.
Moke, raia wa DRC kutoka Bukavu ameripotiwa kuuawa asubuhi ya Machi 6, mwaka huu huko kwao Bukavu.
Sababu za kifo chake zinatajwa ni kuchomwa moto na wananchi waliojichukulia sheria mkokoni wakidhani ni mhalifu. Katika siku za hivi karibuni matukio ya wananchi kujichukulia sheria mkononi huko Bukavu nchini DRC yamekuwa mengi sana.
Sababu kubwa inatajwa kuwa ni kupambana na wimbi la uhalifu kufuatia wafungwa wote kutolewa jela na waasi wa M23 baada ya kuliteka eneo hilo.
Wafungwa hao sasa wamegeuka kuwa wahalifu mitaani na wananchi hawana namna zaidi ya kuwakamata na kuwachoma moto.
Kwa hiyo wananchi walimkamata Doyi Moke kimakosa wakidhani mhalifu na kumchoma moto. Hii ni habari ya kuhunisha sana.
View attachment 3262316
daah hili kosi kitambo sana golini doy anacheza kafunga usongo wake kichwani kitasa anamaliza mayai tembele chibe chibindu kule pembeni pale kati mwanamtwa kihwelo na mahadhi wanakimbiza winga zinazibitiwa na vibelenge lunyalunya na saidi maulid senta fowadi mnyamwezi mwenyewe idi moshi.Golikipa wa zamani wa timu za Majimaji ya Songea, Simba Sc na Yanga Sc, Doyi Moke raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amefariki Dunia baada ya kuchomwa moto na Wananchi wenye hasira kali
Inaelezwa asubuhi ya Machi 6, 2025 Doyi ambaye alikuwa tayari amepatwa na matatizo ya akili na amekuwa akitembea barabarani kama ‘chizi’ alitoka kwake akielekea nyumbani kwa mwanaye ambapo mahali alipoenda huko Bukavu kuna wafungwa ambao walitoka gerezani na walishakuwa na tabia ya kuwaingilia watu ndani na kuwaibia vitu.
Kwa hiyo Wananchi waliamua kujichukulia Sheria mkononi kutokana na kitendo cha wafungwa hao kufanya vitendo hivyo ambapo inaelezwa kuwa Wananchi walikutana na Doyi ambaye alikuwa anatoka kwa mwanaye na kumjumuisha miongoni mwa wahalifu hao.
Wananchi hao walimfunga minyororo sambamba na watu wengine watatu na kumchoma moto kama inavyoonekana pichani.