Kipato changu kwa mwezi ni 150,000/- nipeni mbinu ya ku-save nami niondokane na umasikini wa kipato

Kipato changu kwa mwezi ni 150,000/- nipeni mbinu ya ku-save nami niondokane na umasikini wa kipato

Unahisi mimi nakaa Mkoani kigoma kule nyamuhunge si ndio?

Au unahisi mimi nilianza maisha kwa kupewa mtaji na wazazi/ndugu

Au unahisi mimi ni wale wakaa maofisini watunga story na kuziuza

Au unahisi hata kama nipo dar basi nimekuja mwaka jana si ndio?

Kijana acha nikwambie kitu,maisha hayataki watu wenye mindset kama yako

eti anatafuta kitonga! unajua maana ya kitonga wewe? kwanini nisingemshauri

akauze TIGO aongeze kipato kama shida ni kitonga? chekecha ubongo huo maisha sio marahisi hivyo

uliza walioanza maisha bila kuwa na nyumba za kuishi walikua wakilala wapi,unahisi kila

unaemuona mjini kapanga room si ndio? Unajua gharama za kupanga wewe? au unahisi kupanga ni KODI tu?

Akili yako inawaza kuwa apange room alipe kodi tu, si ndio? Una utofauti gani na wale wazazi wanazaa watoto

wakiamini mahitaji ya mtoto ni Nguo/malazi na Elimu... Fungua akili hiyo maisha ni Fumbo,si kila mtu anaweza lifumbua.

Mkuu huyo tayari anauhakika wa 150k kwa mwezi Tena yupo single ,unajua maana ya "uhuru binafsi "

Yaani akishatoka hapo na kuaanza kujiunga na kundi la wanywa pombe ,walevi ,wavuta sigara ,huku akitegemea hifadhi yao ni kujipotezea hata kipato alichokuwa anapata 150k kwa mwezi ....!

Hayo mazingira unayomwambia akaishi Mimi watu wa aina hiyo nawajua ,acha kujifanya mujuaji hayo maisha yatamzalishia majanga + ,maisha ya makundi na kukaa na masela kwa dsm Mimi nayajua na nimeishi Sana ...!

Hapa cha kumshauru mtoa maada kama anafanya kazi mchana kupata 150k atafute kazi extra hata usiku apige kuongeza kipato ......

Siri ya ushindi siku zote ni kushambulia hakuna haja ya kujilinda na kujiwekea mipaka kwa kulazimisha kuendelea kuishi kwenye 150k mwezi ....!

Ungetoa ushauri JINSI ya kuongeza kipata sio kukabidhi room ....

Unajua faida ya kuwa na chumba chako mwenyewe bila makundi ?hasa kwa hapa mjini ....?

Bro nimeishi Sana maisha hayo ya kisela na Wana ,nayajua in and out kusema kweli Kuna hasara nyingi kuliko faida ,ndio maana wengi wanaoishi hivyo wanapambana kutafuta hata room ya Giza kuishi pekee yao ...!

Kuhusu life nimelopitia nikisema nisimulie hapa ,hakuna wa kiwezea kuhimiki mapito yangu mkuu ,nishapigikaaa hasa ,kulala njaa Sana ,kulala nje kwenye mabox sanaa,hakuna rangi ya shida ambayo sijawahi ona ....

Zaidi ya yote kuwa na kwako ndio hatua ya kwanza ya kuwa na maendeleo trust me ,kutafuta chumba na kupanga hapa mjini ni kama msingi kwenye mbio za maendeleao hata kama kwa mwezi unapata 50k ila upo kwenye na sehemu inayo kustiri .....

Acha kuandika motivation story n kudhani kuwa zinaweza kufanta kazi kwenye real life ...mtu atakayesoma ataona it's simple but in real hio inabaki kuwa story kama story nyingine tu .....

Huku field Kuna kila aina ya changamoto ndio maana vilimo vingi vya wasomi vya kwenye madafutari hakuna alishawahi kufauru ,wanakujaga na hoja na mipango mirahisi mirahisi kama wewe bila kujua mtaa ni mgumu kweli kweli ....
 
Personal Fınance,
Hili ni somo muhimu sana ambalo kila mwanadamu angeweza kuliishi basi tungekua tumefanikiwa kuwa na uhuru wa kifedha kwa asilimia kubwa sana.

Personal Finance ni uwezo wa mwanadamu kutenga pesa kwaajili ya matumizi yake ya sasa na ya baadae.

Tunashauri mtu afate njia ya 50%, 30% 20%
Inamaanisha kipato chako unachokipata either ni kwenye biashara au mshahara ukigawe kufata hizo asilimia.
50% ya kipato ni ya kufanyia matumizi muhimu kama kulipa kodi ya nyumba, kodi ya jengo la biashara, nauli ya kukufikisha kazini au sehemu ya biashara nk

30% hii ni kama emergency fund ambayo utatumia mfano imetokea harusi ama msiba utahitajika kuchangia, laptop yako imeharibika, simu imepotea, umeamua kuji zawadia kwa zawadi nzuri, umeamua kuhonga nk

20% hii ndio unayotakiwa kuitunza, usahau kama hii pesa ni yako, sasa kwa waTanzania wengi hii sehemu ni ngumu.
ni ngumu kujisahaulisha kama una pesa na unajua unayo, ni ngumu upatwe na changamoto na usiiguse.
ushauri:
20%
1.fungua fixed account iweke huko kuanzia mwaka mzima na zaidi,
2.Fungua account ya UTT Amis au nenda DSE ulizia ni kampuni gani inafanya vizuri wekeza huko.
3.Nunua line ya simu ambayo unaweza ukampa mtu mwengine akushikie unayemuamini, weka pesa huko tunza kwenye m koba kibubu, au airtel money kibubu, au tig pesa kibubu utafaidika na gawio.
4. Kanunue ardhi (shamba ama kiwanja)

mimi nashauri 50% 20% 20% 10%
ambayo asilimia 50 inaendana na hio hapo juu,
20% iendane na 30%
20% nyengine iendane na 20%
alafu 10% ya mwisho ni mpya..
hii iwe ile pesa ambayo upo teari ku take risk nayo,
namaanisha hii iweke kwenye biashara.
kama genge, kuuza maji officini, kuuza juice, kuuza ma T shirt , wallet nk
biashara ambayo haigharimu mtaji mkubwa.
 

Attachments

  • IMG_0214.jpg
    IMG_0214.jpg
    19.2 KB · Views: 14
Mtoa mada ondoa dhana ya kusave mapesa mengi kwa muda mfupi.

Tumia formula ya kusave 10% ya kila pesa unayopata.

Yaani katika laki moja unusu wewe weka 15000 tu pembeni kila unapopata hiyo pesa.

Jitahidi kusave kiasi hiko tu.

Lazima ujifunze kusave kidogo na kutumia kingi,hautakiwi kusave kingi na kutumia kidogo.

Kwa sababu utasave pesa nyingii kuna mahitaji ya msingi utajinyima,ipo siku yataibuka yatakuwa makubwa na utamaliza mpaka hiyo akiba yako.

Ila ukifanya matumizi yako kwa usawa kila kitu ukaweka mahala pake inakuwa poa sana.

Kuna jamaa alikuwa anasave tu pesa hata hawezi pesa ya kuwatumia wazee kidogo,wazee wake walikuwa wanakopa tuu huko kwa sababu ya shida,mwisho wa siku wazee deni likawa kubwa sana,yule jamaa akapigiwa simu kwamba wazee wake wanadaiwa ikabidi atoe akiba yote akalipe deni,karudi nyuumaa.

Ukishindwa save hata 10000 tu kwa mwezi inatosha,hakuna akiba ndogo mzee.

Achana na upuuzi wa kwenda kulala kwenye vibanda.

Haya maisha mkuu hatujui tunakufa lini,bali siku zote tuna uhakika tuu kwamba tunaishi,hivyo weka akiba kidogo tu kwa sababu hata ukifa sasa unakuwa umefaidi maisha angalau.

Nakupa task we jaribu kusave 10000 tu kila mwezi kwa miezi sita,alafu ukiweza ndio uanze kusave zaidi ya hiyo.

Kwenye kusave kinachomata ni nidhamu na sio kiwango.
 
Watu wanamshauri mwezao jinsi ya kufa.

Kula mara moja? Kwa wiki?

Mwingine anasema kula isizidi elfu mbili kwa siku.

Hapo bado hujaambiwa mshahara wote ukabet sure odd moja
 
Kabla ya yote unatakiwa uwe na malengo yako, unataka kusave kwa muda gani? je ni miezi 6 au mwaka au miaka?

Fahamu sababu zinazokufanya u save pesa,je unataka ufungue biashara,au unataka ununue chombo cha usafiri?

Ukishafahamu target yako (labda target n 1 year) hapo sasa piga kazi ndani ya mwezi ukipokea pesa,kaa ndani tuliza akili..

Mkononi una 150k.. Jiulize matumizi yako makubwa n nini? najua kubwa n Malazi(kodi) na msosi.. Afya n muhimu ila kwenye mwanzo mgumu wa namna hii afya Muachie Allah....

Ukishajua matumizi yako makubwa n kodi na chakula,jiulize Unaweza kuondoa kipi kati ya hivyo viwili ili kibaki kimoja?

Jibu chakuondoa n Kodi,sasa utaishi wapi? Hapa sasa ndio ule msemo wa Maana halisi ya maisha unatokea eneo hili, Hapo Rudisha room ya watu..

Kama ulikua na vitu Uza vyotee bakiza nguo zako na begi tu kama mwana apolo,vitu utanunua huko mbeleni saivi havina maana yeyote maana hata kama una hotpot huna uwezo wakupka hata wali nusu uweke so hapa Ondoa mzigo uliokuganda.

Ukishauza kila kitu ukabaki mweupe n wewe begi lako na nguo zako ndani,sasa Rudsha chumba cha watu, Chukua siku 1 anza kuzunguka huko kwa vijana wanaopga kazi either wabeba tofali au au zege au mizigo ilmrad wawe vijana wapga kazi kweli unawaona.

mfate mmoja wao au waite wote waambie ndugu zangu mimi n mwanaume mwenzenu,nmekuja Mjini sina pa kuishi ila nmekuja kufanya kazi na nimepata kazi sehemu naomba mnifadhili pakulala tu walau mwezi huu tu,nkipata kodi nitahamia kwangu nikapange..

Amini nakwambia ktk lile kundi hatokosekana mmoja mwenye imani maana umeshawambia ukweli kuwa umekuja kutafuta maisha na unaomba pakulala tu.

Utakubaliwa nina uhakika uspokubaliwa zunguka sehemu nyngine na nyngine hadi utakapokutana na yule mtu ataekuelewa,Yupo Mkuu Yupo nina uhakika 100% ujue tu namna yakujieleza na uwe mstarabu.

Ukipata pakulala sasa kipengele ktabaki kwenye msosi, eneo hili nalo si la kucheza nalo linapoteza hela haswa,sasa hakikisha marafiki zako n kina mama ntlie na usijifanye much know kuwa mkweli ukienda kwa kna mama ntlie nunua ukoko ule mzuri utauziwa,siku moja moja ule vizuri ili usipoteze afya ule vtu vya kukupa afya TU.

ishi kwa malengo naamini kwa mwezi mzima utaweza save walau 100k kama kweli utakua na akili zile za mtafutaji wa maisha,aibu acha,ukipewa chakula maswala ya kuzuga umeshiba eti unasema Asante Acha ukipata chance ya kufukia free fukia hadi cha kesho kutwa.

Mkuu miezi yako 6 tu inakutosha kupata 600k na kuanza biashara yako,ukjikaza to 1year utakua na 1.2m Mkuu maisha n safari ndefu na ili ulijue hilo ingiza utendaji ktk hii post,maisha yako unayoyaptia leo Kesho yatakua simulizi za kuchekesha,kuliza na hata kufundisha.

Pambana Mkuu,wenzako tulianza na mishahara ya 2000 per day mapito tuliyoptia ukiyaskia utajiona wewe kumbe n lakinare unamiliki milaki kwa mwezi tena uhakika...

wakat hyo 2000 nlokua nkipewa kuna siku boss anavurugwa anakuja anagomba anasema mna kazi ya kula tu hapa kazini kwangu kazi hamfanyi mnanipa hasara tu,anachukua mauzo yote anatuacha weupe... Mkuuu maisha n safari hebu ianze yako kuna utamu wake kuanza maisha kwa style yako TRUST me utanielewa siku 1 ukivuka hiki kipindi kigumu.

YES YOU CAN.
Upo vizuri sana mkuu, kongole kwako.
 
Back
Top Bottom