Pain killer
JF-Expert Member
- Aug 15, 2017
- 14,361
- 21,680
Unahisi mimi nakaa Mkoani kigoma kule nyamuhunge si ndio?
Au unahisi mimi nilianza maisha kwa kupewa mtaji na wazazi/ndugu
Au unahisi mimi ni wale wakaa maofisini watunga story na kuziuza
Au unahisi hata kama nipo dar basi nimekuja mwaka jana si ndio?
Kijana acha nikwambie kitu,maisha hayataki watu wenye mindset kama yako
eti anatafuta kitonga! unajua maana ya kitonga wewe? kwanini nisingemshauri
akauze TIGO aongeze kipato kama shida ni kitonga? chekecha ubongo huo maisha sio marahisi hivyo
uliza walioanza maisha bila kuwa na nyumba za kuishi walikua wakilala wapi,unahisi kila
unaemuona mjini kapanga room si ndio? Unajua gharama za kupanga wewe? au unahisi kupanga ni KODI tu?
Akili yako inawaza kuwa apange room alipe kodi tu, si ndio? Una utofauti gani na wale wazazi wanazaa watoto
wakiamini mahitaji ya mtoto ni Nguo/malazi na Elimu... Fungua akili hiyo maisha ni Fumbo,si kila mtu anaweza lifumbua.
Mkuu huyo tayari anauhakika wa 150k kwa mwezi Tena yupo single ,unajua maana ya "uhuru binafsi "
Yaani akishatoka hapo na kuaanza kujiunga na kundi la wanywa pombe ,walevi ,wavuta sigara ,huku akitegemea hifadhi yao ni kujipotezea hata kipato alichokuwa anapata 150k kwa mwezi ....!
Hayo mazingira unayomwambia akaishi Mimi watu wa aina hiyo nawajua ,acha kujifanya mujuaji hayo maisha yatamzalishia majanga + ,maisha ya makundi na kukaa na masela kwa dsm Mimi nayajua na nimeishi Sana ...!
Hapa cha kumshauru mtoa maada kama anafanya kazi mchana kupata 150k atafute kazi extra hata usiku apige kuongeza kipato ......
Siri ya ushindi siku zote ni kushambulia hakuna haja ya kujilinda na kujiwekea mipaka kwa kulazimisha kuendelea kuishi kwenye 150k mwezi ....!
Ungetoa ushauri JINSI ya kuongeza kipata sio kukabidhi room ....
Unajua faida ya kuwa na chumba chako mwenyewe bila makundi ?hasa kwa hapa mjini ....?
Bro nimeishi Sana maisha hayo ya kisela na Wana ,nayajua in and out kusema kweli Kuna hasara nyingi kuliko faida ,ndio maana wengi wanaoishi hivyo wanapambana kutafuta hata room ya Giza kuishi pekee yao ...!
Kuhusu life nimelopitia nikisema nisimulie hapa ,hakuna wa kiwezea kuhimiki mapito yangu mkuu ,nishapigikaaa hasa ,kulala njaa Sana ,kulala nje kwenye mabox sanaa,hakuna rangi ya shida ambayo sijawahi ona ....
Zaidi ya yote kuwa na kwako ndio hatua ya kwanza ya kuwa na maendeleo trust me ,kutafuta chumba na kupanga hapa mjini ni kama msingi kwenye mbio za maendeleao hata kama kwa mwezi unapata 50k ila upo kwenye na sehemu inayo kustiri .....
Acha kuandika motivation story n kudhani kuwa zinaweza kufanta kazi kwenye real life ...mtu atakayesoma ataona it's simple but in real hio inabaki kuwa story kama story nyingine tu .....
Huku field Kuna kila aina ya changamoto ndio maana vilimo vingi vya wasomi vya kwenye madafutari hakuna alishawahi kufauru ,wanakujaga na hoja na mipango mirahisi mirahisi kama wewe bila kujua mtaa ni mgumu kweli kweli ....