Kipeperushi kinachotangaza Maandamano Agosti 8, 2026 chaonekana mtandaoni

Kipeperushi kinachotangaza Maandamano Agosti 8, 2026 chaonekana mtandaoni

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Wananchi wanawatag Polisi kuwajulisha dhamira yao ya kuandamana kwa amani Agosti, 8, 2026 maarufu kama 8/8

Tangazo hili linaonesha sababu za maandano ni
  • Kupinga Utekaji
  • Kudai kuheshimiwa kwa haki za binadamu na utawala wa sheria
  • Kutoa Wito wa mchakato wa katiba mpya
  • Kudai Uchaguzi huru na Haki

Screenshot 2026-07-17 at 21-24-10 Instagram.png
Pia soma: TAARIFA RASMI: Maandamano ya Amani kwa Wasafirishaji wote Nchini, Sambaza ujumbe huu Kila Jukwaa na kila mtandao

Ikumbukwe kuwa maandamano kama haya yaliitishwa ili kufanyika kwenye 7/7 Mwaka huu wa 2026 ambapo baada ya kuonekana kwa Vipeperushi hivyo kulionekana kuongezeka kwa ulinzi mkali barabarani na maeneo mengine.

Ulinzi huo uliibua maswali na hofu kubwa miongozi mwa wananchi hali iliyoathiri haa watu kujitokeza kwenye viwana vya maoneshoa mbapo kwa mujibu wa TANTRADE kwa Mwaka 2026 Tsh. Bilioni 3.9 ndio yalikuwa mauzo kwenye maonesho hayo hali inayoonesha poromoko kubwa kulinganisha na Mwaka 2025 ambapo yalikuwa Tsh. Bilioni 7.06

Soma: Mauzo ya Sabasaba yashuka kutoka Tsh. Bilioni 7.06 mwaka 2025 hadi Tsh. Bilioni 3.9 mwaka 2026

Kwa hali hiyo maandamano hayo yalidhibitiwa kwa nguvu kubwa ya hasara kwa Taifa hili.
 
Ibara ya 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Ibara hiyo inasema:

"Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani..."

Hii ndiyo ibara inayotambuliwa kama msingi wa kikatiba wa uhuru wa kukusanyika na kuandamana kwa amani nchini Tanzania.
 
Nina wasiwasi haya maandamano ya kwenye mtandao ni mradi wa watu kupiga hela za maadalizi ya kuyadhibiti, posho ya kushinda barabarani kwenye siku zote zilizoainishwa, nk

Kwa nini polisi hawaruhusu yafanyike kwa amani?
Nishawahi kuwaza hili pia, kwanini viongozi bado wanalifurahia hili kwa kujitokeza mtaani kila inapotangazwa, si ndo wanaendeleza upigaji kwa kujitengea mabilioni ya udhibiti?
 
Back
Top Bottom