Kwa kuwa unataka ushauri wa magari ngoja tukushauri kwenye magari ambao tumeshatoka huko.
1. Kwa lengo la mzunguko wa pesa ya chap chap na pressure juu, chukua TATA kwa sababu zifuatazo.
a. Vipuri vyake ni bei juu, na ufundi wake ni gharama, pindi kile cha upya kimeisha.
b. Ngoma ikichoka huwezi iuza mapema ukilinganisha na hiace utakayonunua.
C. Ukikomaa mlangoni ni vyema, ila kwa sababu wewe ni mgeni kwenye game, watakupgisha mswaki mwanzo mwisho, na jioni dereva anajua posho yake ipo, hivyo huna la kubisha maana hela ulikuwa unachukua wewe.
Mfano, kama wangekuwa wenyewe wangepanga foleni na kujaza level seat na wanaenda mdogo mdogo ila ukiwa nao wanakwambia foleni ndefu tuanze mbele huko wanakimbizana mwisho wa route unaenda mswaki na kurudi mswaki.. ( bora uwaache wenyewe wakuletee hesabu usiweke mpambe).
Hapa kama unaweza omba hata deiwaka kwanza kwenye magari kwa miezi kadhaa then ndo uwe na chombo yako uzuge nimepewa na uncle. Faida yake utajua konda/derva yupi chenga na yupi mzuri.
D. Mabao kwa costa na hiace hayatofautiana sana, ila costa/tata inaongoza,
E. Riba ya mkopo against na running expenses unatakiwa uliangalie haswa baada ya miezi 6-8 kuisha.
2. Chukua hiace/costa.( agiza japani)
Kwani hela yake ni 50 hadi 100k ni yako na ukiipata huwazi marejesho.
Wewe ni service na benk.
2. Ikichooka ni rahisi kufanyiwa matengenezo ikarudi karibia na upya kwa bei nafuu ukilinganisha tata.
3. Unaweza ukapata tenda ya kubeba wanafunzi wa shule na ikakulipa kwa rahisi kwa ruti za asubuhi na mchana.
Kingine u cane manage seven kuendesha mwenyewe.
Ushauri mwingine mbadala wa hayo magari/ iron businesses.
1. Cjui upo wapi ila fuga mbuzi wa nyama, fuga mbuzi tafuta eneo hiko singida kodi( hata heka 10.) Kashinde huko ununie mbuzi uwe na mbuzi 50 kwa kuanzia nakuapia baada ya mwaka na nusu. Hutaki tena hiace au tata.
2.ushauri mwingine usifanye haraka kwenye jambo lolote anza mdogo mdogo na usiwekeze mzigo wote kwenye 1 running business.
Nakutakia mafanikio mema, ukafanikiwe mwana jf