Kipi bora kununua Hiace mpya kwa 30M ama kuchukua Tata Marcopolo kwa mkopo

Unajitosa ila muda huo huo unapolichukua tokea kwa MTU ni lazima uwe una uwezo kujua uzima Gari ni zima ama sio zima
Tunaponunua gari huwa hatukurupuki kununua Kama unavyonunua suruali Bali Ni lazima lichunguzwe na mafundi wako na ikiwezekana unaipigisha safari moja Dar to Singida na kurudi Kama ni mbovu mafundi wataijua tu.
 
Salute kwako ndugu
 
Usimdanganye kuwa akimaliza deni anaanza kula faida kumbuka kuna pesa ambayo aliitanguliza kwa Mhindi zaidi ya M 25, so baada ya kumaliza deni, anatakiwa aanze kukusanya pesa aliyojikopesha ambayo ni M 25, ambayo ataikusanya zaidi ya miezi 6. so faida ataanza kuipata baada ya miezi 15.
 
Umeongea ukweli mtupu bila kupepesa macho. Ukweli Ndio huo uwezi kuwa na 30M ukae kwy ukonda utakufa na stress
 
Hiyo ni kila kitu usajili na TRA ile gharama zao umeshalipa mana kuna muda ushuru Wa serikali unazidi gharama ya Gari japan
Mkuu naona watu wanaongea wasiyoyajua kila mtu ni Mjuaji tuu lakini ukweli wa mambo hawayajui

Mie naomba nikupe experience yangu, nilichukua mwezi wa tatu Tata 105M. Unalipa 30% ambayo ni kama 30.15M. Bima kubwa 10.6M. Wanakukopesa 73.5 interest in 23% Jumla inakuja 92M kwa mwezi unarejesha 3.8M. Sasa mie niliipeleka mkoani inapiga route mkoa to mkoa baada ya kutoa matumizi yotee mafuta na posho inalaza 150k mpaka 250k siku hazilingani. inatembea masaa 8 mpaka tisa kwa siku gari haichoki tofauti na Dar inatembea zaidi ya masaa 15. Kwa mwezi unauhakika wa kulaza 4.5M mpaka 6M

Gari ikiwa bado mpya service ni oil tuu kila baada ya wiki inategemeana na urefu wa safari yako Max service Km ni 7000, Tairi na break baada ya muda kwa sababu inatembea kila siku.

Kila biashara ina changamoto watu wasikutishee kwani wanaoifanya wanawezaje. Tafuta dereva Mzuri konda weka ndugu yako unaemwamini utatembea kifua mbele. Baada ya miezi 24 unamaliza mkopo wako unaendelea kula maisha au uanweza kuuza hata 40M unarudisha hela yako. Gari ukiitunza vizuri inaweza kufanya kazi hata miaka zaidi ya 10.

Angalizo hii biashara hela ya hesabu usiende kulia bata inatakiwe uiwekee kwenye account na hyo account usiizoee fanya kama hauijuii kabisa maana gari muda wowote inaweza taka hela afu we hela ushalia bata ndo hapo unaposikia mtu amepaki gari. Siku zote hela za biashara usiziingize kwenye matumizi yako binafsi au ya nyumbani acha biashara ijiiendeshe yenyewe huku matumizi yako unayatoa sehemu nyinyinge

Ukihitaji Contact za Tata karibu. All the Best
 
Hiyo ni kila kitu usajili na TRA ile gharama zao umeshalipa mana kuna muda ushuru Wa serikali unazidi gharama ya Gari japan
Milioni 40 unapata Coaster na ushalipia kila kitu. Kama unataka kufanya hii business hata kwa ubishi anza na Coaster lako bila mkopo.
 
keisangora Chukua TATA , tafuta route nzuri na management nzuri , usimamizi wa maintenance,fuel na drivers ni muhimu na ndo changamoto kubwa otherwise hamna biashara yenye 0 challenges, ukishindwa kabisa fanya outsourcing zipo kampuni ninafanya usimamizi wa mabasi kwa makubaliano maalumu wewe yako ni hesabu ya siku tu , the rest wanadeal nayo wenyewe,mfano routes,drivers, maintenance, insurance, nk
 
Nimesoma coment zote mwanzo mwisho
wadau wametoa ushauri mzuri tena wakitaalamu na kiuzoefut

kulingana na mawazo yaliyotolewa humu, ni vema ukaufuatilia na kutekeleza ushauri wa kufungua hardware

 
Nenda Tata saivi wanauza kama 120M ivi ila unalipa 30% na Bima comprehessive 10M. gharama zingine ni TRA , Sumatra kama laki tano ivii. Gari ikiwa Mpya na ukipata dereva mzuri service ni oil tuu mpaka miezi sita
Achana na kitu ya kiindi au kichina, kama una uwezo nunua coster used au hata tipa la mkononi kuliko izo vitu za bara asia. Unaweza jikuta kabla ya kurudisha nusu ya mkopo unaanza tafuta engine na giabox za canter bure
 
Harware minimum mtaji shingap
Minimun nashauri iwe 10million japokua pungufu yahapo pía unaweza kufanya, 10-15m unaweza kuchukua mzigo kwa supplier mmoja a ukapewa mzigo wa 20-30m, sio vitu vyote kwenye hardware vinalipiwa cash, mfano baadhi ya mabati rangi nabaadhi yavitu vingine unaweza kuvipata bila kulipia kwajumla inategemea namakubaliano yako nasupplier. Kitu ambacho huwezi kukopeshwa ni gypsum, cement nabaadhi yavitu vingine
 
Una uzoefu mkuu..hongera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…