Kipi bora: Kuoga Usiku au Asubuhi?

Tafiti zinasema hakuna athari zozote za mtu kuishi bila kuoga.
Huku Tz ni joto kali, hivyo tunaoga ili kuupa mwili hali ya utulivu. Lkn Tz hii hii sehemu kama MAKETE kuoga sio ishu ya maana kwa kuwa hakuna madhara ya kimwili yapatikanayo kutokana na kutokuoga.
 
Mbeya kuna muda nilikuwa nakaa bila kuoga hadi nasahau mara ya mwisho kuoga ilikuwa lini
 
Du wewe kweli mhehe ukiwa mfifu [emoji23][emoji23]
 
Dar ukipanda daladala unakutana na wanaume wananuka uvundo, sijui ndo fangasi na meaoga siku hiyo.
 
unaeza ukaoga usikuu ukajiona umatakata...ukaoga na asubuhi ... ukijifuta na taulo jeupe peee utajichekaa kwa jinsi linavyochafukaaa

anyway ngozi inatoa uchafu na seli zingine zafwaaa cha muhimu usafi wa mwiliii
 
Usiku tu inatosha, na inategemea na hali ya hewa
 
Kwangu swala kuoga, halina ni kila mwili unapohitaji.
mfano: Nimeoga alfajiri, nikaenda kufanya mazoezi nikirudi naoga. Nikirudi nyumbani toka kwenye shuguri za kiuchumi, nitaoga, yaani kuoga kwangu hakuna ratiba.
Safi
 
Umetisha sana Mkurugenzi, umenikumbusha nilivyokuwa Boarding Uganda, Kuna mTz mwenzetu huyo jamaa alikaa mwezi mzima hajagusa Maji, Ukiachana na baridi la kule kuwa kali kipindi hicho lakn pia Maji yalikuwa ni yakuyapangia foleni

Sasa jamaa alikuwa anashangaa watu eti baridi hili lote Bado nipoteze muda kupanga foleni ndefu kuchota Maji? Akaona haiwezekani, Sasa bhana utamaduni wa kule ukienda chooni unaenda na tissue paper.

Sasa kuna kademu kalikokuwa kanakaa nae dawati moja darasani akaenda kumshtaki kwa dada zetu wa Tz walikuwa Form 6, kikao kikaitishwa Watanzania wote tukutane nyuma ya kanteen, tukaanza kusemwa "jamani eeh mjitahidi kuoga mnatoa harufu mbaya watu wanalalamika hasa wewe H"

Mwamba H toka siku Ile hakuna siku alimisi kuoga, mm niliendelea na utaratibu wangu, nikioga Leo kesho siogi Hadi kesho kutwa hvyo hvyo
 
Huyu ni mm kabisa
 
Katika vitu siwezi kuvumilia ni harufu mbaya halafu niko very sensitive yaan hata iweje nitaisikia tu,
Mtu ananuka Mdomo,
Mtu ananuka Makwapa,
Mtu ananuka Miguu,
Mtu anatoa Pumzi yenye harufu mbaya,

Siweziiii lazima nikwambie tu, ukichukia shauri yako, kikubwa ujumbe umefika na ukae mbali na mimi kama huwezi kurekebisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…