Kipi bora kushuhudia kifo cha mzazi wako, anaeumwa au kuambiwa kafariki?

Kipi bora kushuhudia kifo cha mzazi wako, anaeumwa au kuambiwa kafariki?

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
16,583
Reaction score
42,992
Wakulungwa naomba mnisaidie hivi kipi bora kuwa karibu na death bed ya mzazi wako anaeumwa au kuja wakati ameshakata kauli.

Binafsi nadhani nibora ningekuwepo kushuhudia the last moments of my beloved dady probably he would have something to tell me. Naumia sana kwamba mzee wangu alifariki nikiwa sipo, nilimkuta tu amelala kwenye kitanda chake akiwa amefunikwa shuka. Oooh dady!

RIP MY DADY, NAJIKAZA KUTOA MACHOZI HATA HAPA OFISINI THOU NI MIAKA MIWILI SASA.
 
Ulinganisho wako hauna maana kwa sababu umeweka maneno "kipi bora" kana kwamba ni jambo zuri.

Kuna mambo sio ya kulinganisha.
 
Yaani kiukweli habari za kifo hakuna anayetaka hasa hasa kwa mzazi,so siwezi kuchagua, yeye alivyo panga iwe basi na iwe hakuna wakumpinga.
 
Kushuhudia na kusikia ni vitu viwili tofauti kabisa kwa hisia za Binadamu,
Kushuhudia jambo kunasisimua zaidi kuliko kulisikia,ndio maana kuna watu wanapoona jambo la hatari likifanyika hufumba macho mpaka jambo lile lipite (Inaweza kua jambo hilo la hatari linafanyika kiuhalisia au kwenye movies)

So,kwangu mimi kusikia ni nafuu kiasi kuliko kushuhudia japo matokeo ya kilichofanyika hua ni yale yale (Kifo)

Tujitahidi kua na mawasiliano na wazazi wetu kwa wale wanaoishi nao mbali kwa sababu mbalimbali za kimaisha,kama huna mawasiliano ya mara kwa mara na mzazi wako na ukaja ukasikia kua amefariki hiyo inauma zaidi kwa aliyefiwa na aliyefariki,imagine mzazi mpaka anaaga Dunia huku ukiwa hujawasiliana nawe kwa muda mrefu,hapo lazima atakufa huku akiwa na masikitiko juu yako,

Dunia isitushughulishe sana tukasahau Wazazi au ndugu,maisha ni kua karibu/kua na mawasiliano na watu wako wa karibu,

If you're giving others more priority than ur own family,then you need to understand that you're heading the wrong way.
 
Kupoteza mpendwa wako ni maumivu, na kupewa taarifa hayupo tena inauma zaidi... unatamani ungekuepo umwone mara ya mwisho. Lakini kumwona akiwa anaondoka huku ukiwa huna msaada ni maumivu makubwa sana tena zaidi. Yaani kifo ni kifo tuu hakina afadhali

Pole kwa kumpoteza baba yako, roho yake ipumzike kwa amani
 
Ni kweli mkuu,tena nilichoumia zaidi bado alikuwa hajaanza kula matunda yangu yaani ile nimeanza kufanya kazi nianze kuandaa mazingira ya kujenga ili nimlete mjini ile naanza tu kujenga amefariki
Pole sana mkuu mimi nilimuuguza mwaka na nusu na nilifanikiwa kuwapatanisha na Mama mzazi baada ya miaka 40 ya kutengana kwao na Mama akawa ndio mpishi wa mzee mpaka umauti unamkuta. Mungu awarehemu wazazi wetu Roho zao zipate pumziko la milele wapumzike kwa amani Amina.
 
Back
Top Bottom