Kipi kikubwa au kikuu kati ya kitambulisho cha Taifa(NIDA) na passport?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Wakati mtu unaomba passport katika idara ya uhamiaji unahitajika kuwa na kitambulisho cha taifa(NIDA) lakini pia unapaswa tena kufuata mchakato ule ule uliotumia kupata kitambulisho cha NIDA, sasa nini maana kuwa na kitambulisho cha Taifa!

Kipi ni kikubwa, kikuu au cha muhimu zaidi kati ya kitambulisho cha taifa na passport ya kusafiria?

Mimi nilifikiri ukishakuwa na kitambulisho cha taifa(NIDA) unapofika uhamiaji kuchukua passport ilikuwa ni kitendo cha kulipia na wao kuchukua tu biometrics zako za alama za vidole(fingerprints) na macho kisha wakuchapishie passport yako hapo hapo. Sielewei kwa nini inahitajika tena kufuata utaratibu ule ule wa kupata NIDA.
 
Wakati mtu unaomba passport katika idara ya uhamiaji unahitajika kuwa na kitambulisho cha taifa(NIDA) lakini pia unapaswa tena kufuata mchakato ule ule uliotumia kupata kitambulisho cha NIDA, sasa nini maana kuwa na kitambulisho cha taifa!

Kipi ni kikubwa, kikuu au cha muhimu zaidi kati ya kitambulisho cha taifa na passport ya kusafiria?

Mimi nilifikiri ukishakuwa na kitambulisho cha taifa(NIDA) unapofika uhamiaji kuchukua passport ilikuwa ni kitendo cha kulipia na wao kuchukua tu biometrics zako za alama za vidole(fingerprints) na macho kisha wakuchapishie passport yako hapo hapo. Sielewei kwa nini inahitajika tena kufuata utaratibu ule ule wa kupata NIDA.
Kuna duplication ya kazi hapa, kweli tena unaanza upya wanataka cheti cha kuzaliwa tena na vya wazazi wako hawaminiani
 
Kwa mtu mzima (18+) NIDA ndio kuu/kubwa ila sasa suala la umuhimu inategemea na matumizi au malengo yako tu.

Kwa sasa bila NIDA ni ngumu kwa mtu mzima kupata Passport ila mtoto ataipata vizuri tu.

Bila passport huwezi kusafiri kwa amani kwenda mataifa ya mbali.

Ila sio kweli kuwa mchakato wa kupata passport ni sawa na ule wa kupata NIDA. Fomu ya uhamiaji kuombea passport ni tofauti na fomu yakuombea NIDA.

Ni muhimu kuwa na hii michakato sababu ikitokea mtu asiye sahihi akaipata moja ya hizo nyaraka madhara yake ni makubwa tofauti na inavyoweza dhamiwa.
 
Ni kitu gani cha tofauti kikubwa kati ya fomu ya uhamiaji na ile ya NIDA?
 
Kitambulisho cha Taifa (NIDA) na passport ni nyaraka muhimu, lakini zina matumizi tofauti:

Kitambulisho cha Taifa (NIDA).

- Malengo:
Ni nyaraka ya utambulisho wa ndani inayotumika kuthibitisha raia na kupata huduma mbalimbali za serikali.
- Matumizi:
Mara nyingi hutumika katika shughuli za kila siku kama kujiandikisha kwenye uchaguzi, kupata huduma za afya, na shughuli za kifedha.
- Usalama:
Kawaida hutoa ulinzi wa kibinafsi na haki za raia ndani ya nchi.

Passport.

- Malengo:
Ni nyaraka inayotumika kwa ajili ya kusafiri kimataifa na kuthibitisha utambulisho wa mtu katika mipaka ya nchi.
- Matumizi:
Inahitajika unapokuwa unataka kusafiri nje ya nchi, na inatumika pia katika shughuli kama kupata visa.
- Usalama:
Inatoa ulinzi wa kisheria na haki za raia unapokuwa nje ya nchi.

Hitimisho
Kila moja ina umuhimu wake kulingana na muktadha. Kitambulisho cha Taifa ni muhimu kwa shughuli za ndani, wakati passport ni muhimu kwa kusafiri kimataifa.
 
Kwa mtu mzima (18+) NIDA ndio kuu/kubwa ila sasa suala la umuhimu inategemea na matumizi au malengo yako tu.
Lengo la NIDA ni kukutambulisha kwamba wewe ni raia wa nchi(Tanzania), lengo la passport ni nchi kukudhamini uweze kusafiri katika nchi nyingine ukiwa kama raia wa nchi yake au mtu mwenye maslahi na nchi husika.
 
Wakati mtu unaomba passport katika idara ya uhamiaji unahitajika kuwa na kitambulisho cha taifa(NIDA) lakini pia unapaswa tena kufuata mchakato ule ule uliotumia kupata kitambulisho cha NIDA, sasa nini maana kuwa na kitambulisho cha Taifa!

Kipi ni kikubwa, kikuu au cha muhimu zaidi kati ya kitambulisho cha taifa na passport ya kusafiria?

Mimi nilifikiri ukishakuwa na kitambulisho cha taifa(NIDA) unapofika uhamiaji kuchukua passport ilikuwa ni kitendo cha kulipia na wao kuchukua tu biometrics zako za alama za vidole(fingerprints) na macho kisha wakuchapishie passport yako hapo hapo. Sielewei kwa nini inahitajika tena kufuata utaratibu ule ule wa kupata NIDA.
Mifumo serikalini haisomani
 
Kitambulisho cha Taifa (NIDA) na passport ni nyaraka muhimu, lakini zina matumizi tofauti:

Kitambulisho cha Taifa (NIDA).

- Malengo:
Ni nyaraka ya utambulisho wa ndani inayotumika kuthibitisha raia na kupata huduma mbalimbali za serikali.
- Matumizi:
Mara nyingi hutumika katika shughuli za kila siku kama kujiandikisha kwenye uchaguzi, kupata huduma za afya, na shughuli za kifedha.
- Usalama:
Kawaida hutoa ulinzi wa kibinafsi na haki za raia ndani ya nchi.

Passport.

- Malengo:
Ni nyaraka inayotumika kwa ajili ya kusafiri kimataifa na kuthibitisha utambulisho wa mtu katika mipaka ya nchi.
- Matumizi:
Inahitajika unapokuwa unataka kusafiri nje ya nchi, na inatumika pia katika shughuli kama kupata visa.
- Usalama:
Inatoa ulinzi wa kisheria na haki za raia unapokuwa nje ya nchi.

Hitimisho
Kila moja ina umuhimu wake kulingana na muktadha. Kitambulisho cha Taifa ni muhimu kwa shughuli za ndani, wakati passport ni muhimu kwa kusafiri kimataifa.
Utofauti mwingine ni kwamba unaweza kupata passport bila kuwa raia wa Tanzania(kwa maamuzi ya kisiasa) ila huwezi kupata NIDA kama wewe sio raia wa Tanzania.
 
Uliona wapi taasisi za serikali wakitumia akili
Wana uji kichwani,nilifata process zote za passport enzi za vitabu.
Tuma maombi enzi hizo napigwa hadithi tu mara filé limepotea.
Badae naondoka kuna dogo kaka hapa inatakiwa laki 1 tu tumalize jambo lako.
Nilitamani nimkabe anipeleke liliko file.
Nikalipa laki nikapewa pass na ni hapo mjini dar ofisi ya uhamiaji.
 
Hoja za mifumo kusomana ilikuwa changamsha genge😂

Vitambulisho kibao, havijuani na bado service hupati...

Nadhani hata hiyo NIDA ipo linked na taasisi chache sana....

Still your government doesn't know you... Of all the IDs.😄
Sasa hv tunaambiwa mifumo ya bodi ya mikopo ya wanafunzi itasomana na nida pamoja na passport, labla hii ndio kitu watakachokiweza tuu.
 
Wakati mtu unaomba passport katika idara ya uhamiaji unahitajika kuwa na kitambulisho cha taifa(NIDA) lakini pia unapaswa tena kufuata mchakato ule ule uliotumia kupata kitambulisho cha NIDA, sasa nini maana kuwa na kitambulisho cha Taifa!

Kipi ni kikubwa, kikuu au cha muhimu zaidi kati ya kitambulisho cha taifa na passport ya kusafiria?

Mimi nilifikiri ukishakuwa na kitambulisho cha taifa(NIDA) unapofika uhamiaji kuchukua passport ilikuwa ni kitendo cha kulipia na wao kuchukua tu biometrics zako za alama za vidole(fingerprints) na macho kisha wakuchapishie passport yako hapo hapo. Sielewei kwa nini inahitajika tena kufuata utaratibu ule ule wa kupata NIDA.

Hakika.

Halafu NIDA inatumika kukopea simu while Passport kusafiri kwenda kutafuta Maisha mbefele.
 
Back
Top Bottom