Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Serikali ya Tanzania inavyofanya kazi ni kwa ku assume kila mtu ni mwizi na muongo.Wakati mtu unaomba passport katika idara ya uhamiaji unahitajika kuwa na kitambulisho cha taifa(NIDA) lakini pia unapaswa tena kufuata mchakato ule ule uliotumia kupata kitambulisho cha NIDA, sasa nini maana kuwa na kitambulisho cha Taifa!
Kipi ni kikubwa, kikuu au cha muhimu zaidi kati ya kitambulisho cha taifa na passport ya kusafiria?
Mimi nilifikiri ukishakuwa na kitambulisho cha taifa(NIDA) unapofika uhamiaji kuchukua passport ilikuwa ni kitendo cha kulipia na wao kuchukua tu biometrics zako za alama za vidole(fingerprints) na macho kisha wakuchapishie passport yako hapo hapo. Sielewei kwa nini inahitajika tena kufuata utaratibu ule ule wa kupata NIDA.
Hivyo kila process wanakuhakiki upya.
Yani hata kama NIDA ni kitambulisho kinachoonesha wewe ni raia, ukienda kuomba passport na NIDA yako, wanakuhakiki upya kama wewe ni raia.
Hiyo ni nafasi kwao kupata rushwa pia, wakifanya mambo rahisi watakuwa wanajizibia mianya ya rushwa.
Nchi kama Marekani passport unaenda kuomba Ofisi ya Posta ya mtaani kwako tu, na ndani ya mwezi tu wanakutumia. Unachotakiwa kufanya ni kuomba wiki sita kabla ya safari yako tu. A painless process.
Pasipoti ni haki ya kiraia, kikatiba na kibinadamu.