Kipi kikubwa au kikuu kati ya kitambulisho cha Taifa(NIDA) na passport?

Serikali ya Tanzania inavyofanya kazi ni kwa ku assume kila mtu ni mwizi na muongo.

Hivyo kila process wanakuhakiki upya.

Yani hata kama NIDA ni kitambulisho kinachoonesha wewe ni raia, ukienda kuomba passport na NIDA yako, wanakuhakiki upya kama wewe ni raia.

Hiyo ni nafasi kwao kupata rushwa pia, wakifanya mambo rahisi watakuwa wanajizibia mianya ya rushwa.

Nchi kama Marekani passport unaenda kuomba Ofisi ya Posta ya mtaani kwako tu, na ndani ya mwezi tu wanakutumia. Unachotakiwa kufanya ni kuomba wiki sita kabla ya safari yako tu. A painless process.

Pasipoti ni haki ya kiraia, kikatiba na kibinadamu.
 
Sasa hv tunaambiwa mifumo ya bodi ya mikopo ya wanafunzi itasomana na nida pamoja na passport, labla hii ndio kitu watakachokiweza tuu.
Never, vitisho visivyo na sababu

Bodi wanamtambia mdaiwa kwa Index no ya form four...
Huko NIDA na Rita hawajui hata document wanampa nani....
Ni story tu na tushazizoea...

Wangapi walikopa hata kwenye wadaiwa hawapo?
Sasaivi kuna Samia scholarship.. ni fedha za nani na zitalipwaje?

Kwanini kulikuwa na exclusion ya waliosoma Bure kabla ya 1994, hiyo special privilege kwa pesa za umma wanatoa wapi.... Kama sio kutunga sheria kwa kuangaliana usoni.

Wakati mwingine tukubali tupo Dunia ya tatu na mambo yanaenda taratibu.
 
Mapato!
 
Tanzania yetu bila NIDA hupati passport, hufungui kampuni BRELA, hupati leseni ya biashara, haupati usajili wa line ya simu.

Na kuna mabenki, bila NIDA hufungui account.

Passport ni kama kifaranga litokanalo na yai (NIDA)
 
Tanzania yetu bila NIDA hupati passport, hufungui kampuni BRELA, hupati leseni ya biashara, haupati usajili wa line ya simu.

Na kuna mabenki, bila NIDA hufungui account.

Passport ni kama kifaranga litokanalo na yai (NIDA)
Sasa kwa nini mtu mwenye NIDA anayeomba passport anatakiwa kupitia mchakato ule ule aliopitia kupata NIDA??
 
Rushwa tu
Nyingine ngonjera tupu
Wageni kibao wanapata NIDA na passport,tena ndani ya muda mfupi tu tofauti na mtanzania asie na hela.
Hakuna cha madhara Wala nini, nchi ya hovyo
 
Rushwa tu
Nyingine ngonjera tupu
Wageni kibao wanapata NIDA na passport,tena ndani ya muda mfupi tu tofauti na mtanzania asie na hela.
Hakuna cha madhara Wala nini, nchi ya hovyo
Lakini nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara zinafanana hii tabia ya rushwa. Hapo Kenya wasomali kibao wanajichukulia tu NIDA za huko. Hata baadhi ya watanzania wanajizolea NIDA za nchi jirani hadi passport.
 
Kupata pata passport wannidai cheti cha kuzaliwa cha mzazi.
Mzazi wangu hana cheti cha kuzaliwa , kazaliwa kitambo kidogo.
Hii inakuwaje wajuvi
 
Passport ndio utambulisho muhimu kuliko vitambulisho vyako vyote. Passport ndiyo inakutambulisha duniani.
Unaposafiri nje ya nchi vitambulisho vyako vingine vyote ni kama takataka tuu. NIDa, cha Kura, Cha kazini vyote havina kazi unapoenda nje ya nchi. Ila NIDA ni lazima uwe nayo unapotafuta passport
 
Huo utaratibu unawasaidia kupata ya "maji"
 
Utofauti mwingine ni kwamba unaweza kupata passport bila kuwa raia wa Tanzania(kwa maamuzi ya kisiasa) ila huwezi kupata NIDA kama wewe sio raia wa Tanzania.
Kama ndivyo, NIDA ni kubwa kuzidi PASSPORT, hivyo ilipaswa kuwa rahisi zaidi kupata passport kuzidi NIDA!
 
Usumbufu wote huo ni kwa sababu ya kula kwa urefu wa kamba.
 
Its all about making money wala kulikuwa hakuna haja ya kuwa na majengo ya NIDA kila wilaya issue hio kingekuwepo kiofisi pale UHAMIAJI au RITA ila ndio hivyo mchakato wa kupata passport nao ni chanzo cha mapato kwa nchi na Rushwa kwa wafanyakazi..., Mambo mengi duniani ni Usanii tu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…