Mando_
New Member
- Sep 24, 2023
- 1
- 0
Binafsi sioni tatizo kama mhusika hatoongea mwenyewe mbele ya watu,Jana nimekutana na mwamba mmoja kavaa fresh tu na ukimtazamaunajua huyu anaelekea katika ofisi flani yenye hadhi au labda ni mtu mwenye mishe zake za kuelewekwa, lakini ajabu nikaona anaongea peke yake.
Awali wakati namkaribua sikutilia shaka sana hilo niliamini labda kuna kitu kaaa sikioni, si unajua tena siku hizi teknologia ipo juu, lakini haikuwa hivyo, alikuwa hajavaa kifaa chochote na tulipokaribiana nikiwa nimemtolea macho kwa ukaribu, akajishtukia akaacha kuongea.
Ni kama vile mwaba alikuwa kwenu kikao cha kwake mwenyewe kichwani.
Hii sio mara ya kwanza kutokea hali hiyo, hata mimi huwa inanitokea, hivi ni changamoto ya Afya ya Akili au maisha tu yanatupeleka puta.
Au atanyamaza baada ya kukutana na watu, kama ingekua ni tatizo la Afya ya akili....basi hata wanaojiangalia sana kwenye kioo na kujipiga sana picha kila wakati nao wamo kwenye hilo tatizo.