Kipi kiliwahi kukutokea ukajikuta unaanza kuongea peke yako?

Binafsi sioni tatizo kama mhusika hatoongea mwenyewe mbele ya watu,
Au atanyamaza baada ya kukutana na watu, kama ingekua ni tatizo la Afya ya akili....basi hata wanaojiangalia sana kwenye kioo na kujipiga sana picha kila wakati nao wamo kwenye hilo tatizo.
 
Duh
 
Jaman hii ipo na ni moja kati ya aina ya communication inaitwa "intra-personal communication" kwaiyo hakuna Cha ajabu hapo na hii hali inamtokea Kila binadamu mwenye uhai kama unabisha jiulize nafsi yako toka umezaliwa ujawahi ongea mwenyewe hii ipo na inatambulika duniani na katika ngazi za elimu na ndo maana inafundishwa katika Kila taasisi za elimu
 
Mimi huongea kimoyomoyo! Nikiwa, na hasira, mawazo mazito hutembea kichwani kwangu!
 
Faida zipo Sana, mm nmeweza kujifunza lugha ya kijerumani kwa kuongea peke yangu na wajerumani wanashangaa nmejifunzaje Mana Niko fluent Kama vile nmeishi huko Munich.

Sent from my TECNO KD7 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…