Kipi kimemfanya Geofrey Mwambe aliyekuwa Mkurugenzi (Director) wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuteuliwa kuwa Waziri wa Biashara na Viwanda?

Alifanya pia NIDA kwa muda mfupi. Na mabomu yake yakalipuka🤣🤣🤣😂😂😂😂
Arekebishe na BOT na TRA kwenye akina masamaki wengi mno, akiweza huko hakika ataisaidia Nchi kupiga hatua kimaendeleo kwa kasi kubwa mno
 
Mkuu nakubaliana na wewe. Tuweke personal differences pembeni na tumwangalie Mwambe kama mtu mwenye uthubutu, ari na uweledi unaotakiwa kwa nafasi kama hiyo. Ninamfahamu vizuri huyu mteule wa rais. Wengi wanahoji exposure yake kwa kuangalia nafasi ya ukuu wa Wilaya ila hawasemi kuwa alifanya kazi BoT kama mchumi mwandamizi idara ya international economics kwa zaidi ya miaka kumi, alikuwa mkurugenzi wa uwekezaji Wizara ya Afrika Mashariki kwa zaidi ya miaka mitatu kipindi cha JK na baadae alielekea kwy ubunge 2015. Baada ya kura kutotosha alipewa ukuu wa Wilaya na baadae Mkurugenzi TIC. Alikuwa mkurugenzi wa bodi BoT zaidi ya miaka 3 akiwa kwenye kamati nyeti kama ya sera za uchumi (monetary policy committee) na kamati ya usimamizi wa mabenki. Pia alikuwa mkurugenzi wa bodi ya TRA. Hivi tunataka exposure gani zaidi? Anaelewa vizuri sana changamoto za uchumi na uwekezaji Tanzania. Tumpe nafasi awatumikie Watanzania
 
Arekebishe na BOT na TRA kwenye akina masamaki wengi mno, akiweza huko hakika ataisaidia Nchi kupiga hatua kimaendeleo kwa kasi kubwa mno
Atafanya vizuri mkuu. Ni mzoefu katika kuchimbua mabomu na kuyalipua
 
Kabla ya kuwa DC alikuwa mkurugenzi wizara ya Africa mashariki kipindi Cha JK ,baada wizara kuunganishwa hakuwq na nafasi ya ukurugenzi ndio maana akapelekwa manyoni
 
Atafanya vizuri mkuu. Ni mzoefu katika kuchimbua mabomu na kuyalipua
Kama elimu uliyopata imekufanya kuwa mshabiki wa kiwango hiki..basi huko ulikopitia kusoma wamefeli mno, si lengo la elimu kumfanya muelimishwaji awe mshabiki wa mambo bila hata kupima ushabiki wenyewe una substance..
 
Ukiaminiwa kutumikia umma nafasi yoyote inayokupa nafasi ya kufanya maamuzi weka alama basi..ili hata ukitoka hapo alama zitabaki na zitasema wewe ulikuwepo hapo muda fulani..Mwambe amekaa TIC miaka 3 hivi kuna alama gani itakayoonyesha alikuwepo TIC km DG..? maelezo meeengi bila evidence, elimu ya makaratasi haina future kwa sasa, ONYESHA, weka alama kwamba umeelimika na una exposure..nchi hii kila mahali umachinga tu..sisi tukoje lakini, haya mambo ni magumu sana kuyaelewa kupima km mtu anafaa au keeper tu!
 
E
Xposure kaipata manyoni?
 
Na zaidi amefanya kazi Ujerumani miaka 5 kwenye kampuni kubwa sana, na anazungumza kijerumani. Pia amefanya kazi REPOA kwa ufupi. Amefanya kazi binafasi nyingi na organisation kubwa kama consultant. Watz ifike wakati tuache kujifanya wajuvi kumbe hatuna tulijualo. Ni busara kukaa kimya kwa jambo usilolijua. Uko sahihi!
 
Breathe and relax ndugu. Kisha take your time kuangalia michango yangu ya nyuma humu uone kama unalosema ni la kweli au la. Maana ni rahisi najua sina haja ya kukuelekeza namna ya kutazama kwenye profile yangu. Ukishindwa basi utakua ni sehemu ya watu wavivu kufanya research. Ungelikua mwerevu ungechukua muda wako kuitazama michango yangu kuona kama ni pro-govt au la!
 
Wewe ni mbumbumbu wa namna serikali inavyofanya kazi.

Hoja zako kuhusu uteuzi wa waziri hazina mashiko. Exposure haina umuhimu wowote katika vigezo vya kuteua mawaziri. Mtu yeyote ana historia yake, hata wewe kabla ya kuandika utumbo wako ulikuwa somewhere. Hivyo Mwambe kutokea kwenye udc sio hoja. Nyerere alitokea wapi? Castro alitokea wapi? Abeid Karume alitokea wapi? Wote hao wamefanya mambo makubwa sana kwa maendeleo ya nchi zao.
 
Diaspora wapo, yule ndejembi si amekaa nje yule?? Ila Huyu Mwambe na Dorothy Gwajima ni akili kubwa

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Kinachoangaliwa ni undugu, udini, ukanda na ukabila
 
Uongozi ni elimu au uwezo wa mtu?
 
Angalia ulivyo mpumbavu usiye na akili wala uelewa hata wa mambo madogo!!

Nimekuuliza huyo Julieth Kairuki niliyesema alikuwa ni perfect choice aliteuliwa kuwa waziri?!

Nimekuuliza, suala la kuvutia FDI lipo kwa waziri?

Halafu ulivyo mpumbavu, hadi aya ya mwisho nimezungumzia TIC... sasa TIC ni wizara hadi ung'ang'anie suala la uwaziri?

Unanitajia habari za akina Nyerere wakati suala la TIC sio la uongozi wa kisiasa!!

VERY STUPID!!
 
Alifeli kiajee? Mwambe hadharani alikua anatetea wawekezaji haswa watanzania. Na inawezekana pia alikuwa mwazi KWA mkuu na ndo maana TIC inasimamiwa na ikulu Sasa. Na hapa Tanzania Kuna fitna ajabu,, nadhani Mwambe watu wanamchafua kifitna tu. Angekua hajafanya vizuri pale TIC asingepewa uwaziri wa viwanda. Nina imani kubwa Sana nae

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Chige ,huyo sukule achana naye.
Umeandika mambo ya msingi sana kuhusu exposure kwa mtu wa TIC.
G. Mwambe namfahamu kiasi. Niliwahi kumwandikia barua kuhusu vikwazo tuvipatavyo sisi wawekezaji wa ndani. Issue yenyewe ilikuwa kulazimishwa kwa wenye viwanda kuchangia shughuli fulani.
Alichojibu ni kuwa atalifanyia kazi. Juzi tena huko Mkoa wa Pwani,wenye viwanda tumeitwa tena ili ku pledge kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na madawati,kwani msimu wa masomo unakaribia kuanza huku kukiwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa na madawati.
Nilipopata taarifa ya uteuzi wake,nikijumlisha na tukio la hilo la kuchangia ujenzi,nikapata jibu kuwa jamaa hakuwa na msaada kwa wawekezaji,na kuwa hata hapo wizarani hatakuwa na maajabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…