Kwa mahitaji ya nchi yanayozingirwa na mabadiliko mengi kidunia hasa katika medani za teknolojia, uchumi na siasa...process ya uteuzi inapaswa ifanyiwe marekebisho, sikweli kabisa kuamini kuwa TISS ndio wanajua kila kitu cha nchi hii na wao wanastahili kudrive process za uteuzi, huko ni kujidanganya, pili, ni vyema sasa wanaopendekezwa uteuzi wapitie usaili wa namna moja au nyingine kuthibitisha uwezo wao, uelewa, elimu, maarifa, tabia, mahusiano na mambo gani mapya kama anayafahamu yanaweza ifaa nchi..tatu, nchi zote zenye mkakati imara wa maendeleo wanatumia sana uwepo wa diaspora kubuni na kuweka mikakati ya maendeleo inayotumia teknolojia na kusaili ushindani wa mataifa kwenye maendeleo uliopo, huwezi kuwa na Baraza la mawaziri 23 halafu hakuna diaspora hata mmoja!!!! tarajia total failure, wapo watanzania wengi wenye uwezo mkubwa sana kushape ajenda yetu ya maendeleo kwa sasa, ishu si kununua ndege, kuuza korosho, kukusanya mapato nk..NOOOO! tusiwe km bado tuko dunia ya mwaka 1980..mambo yale yale, traditions!kwamba kwenye baraza la mawaziri lazima iwepo wizara ya biashara na viwanda..bila hata kujiuliza hapa kwetu biashara tulizo nazo ni za aina gani, kubwa ndio nyingi au za kati na za chini ndio nyingi, viwanda gani tunahitaji na vijengwe wapi na wapi na kwa wakati gani...anyway ngoja tuone, sikutarajia mtu km Profesa Matambalya, mtanzania aliyefanya kazi UNIDO na kusimamia vizuri reform ajenda ya Industrialization kwa nchi za Africa, safari hii tena asiwemo kwenye cabinet kuisadia nchi yetu..nadhani pia nafasi ya chief secretary inahitaji mtu mpana sana na mjuzi mwenye maarifa mengi juu ya dunia ya sasa...sifa ya kuwa ulifanya vizuri ulipokuwa katibu mkuu wizara fulani hivyo unafaa kuwa chief secretary ni dhaifu sana..kwa kiwango kikubwa matokeo ya utendaji wa serikali kwa ujumla yanategemea sana uwezo wa mtu wa nafasi hii...haya mambo ya tumbua teua, tumbua teua ni kielelezo cha udhaifu wa mtu anayeshika nafasi hii..tukiwa wakweli kwa dhamira zetu na mbele ya mwenyezi Mungu km kweli tuna nia ya maendeleo kwa watanzania, nafasi hii inahitaji mtu wa kaliba ya Dr. Slaa..
kila la heri kwa wateuliwa!