Kipi kinaanza Mema / Wema au Imani / Mungu

Najiuliza kwa mukstakabari wa Afya ya Jamii na Amani kipi kinatakiwa kiwe Kipimo cha Matendo ya Wanajamii kuyafanya Imani yao inavyowatuma (bila kuangalia matokeo) au Matokeo (yaani wanachofanya kuhakikisha hakiumizi yoyote) hata kama kinaendana tofauti na Imani yao ?

Hata Kama Imani hio ni ya wengi je inamaanisha hata wale wachache wanaobaki waumie ili hao wengi waridhishe Mungu / Imani yao ?

After all Kama Simba Wawili na Binadamu mmoja wakisema wapige Kura ya Chakula cha Kula, Binadamu lazima ndio atakuwa Kitoweo....
Mkuu kumbuka nia ya mtu ndio imebeba mema au uovu. Naweza kufanya jambo ukaliona halikuumizi ukaliona ni jema lakini nimelenga nikumalize.

Itaanza imani ila itategemea kama hiyo imani imejengwa juu ya upendo.
 
Sidhani kama matendo yote yanasukumwa na Imani mengine yanasukumwa na facts ukiumwa nikikupa dawa nataka nikuponye nikikupa sumu nataka nikuue

Tukija kwenye motive yako kama jamii who cares kama umepanga kumuumiza mtu ukamwagia maji ila kumbe ana kiu akanywa yale maji ni vema kuliko anayepanga kumpa maji ya kuondoa kiu kumbe hayajachemshwa hence kupata madhara...
 
Sidhani kama matendo yote yanasukumwa na Imani mengine yanasukumwa na facts ukiumwa nikikupa dawa nataka nikuponye nikikupa sumu nataka nikuponyeshe.....

Mkuu kwanza imani ni fact, hakuna imani bila fact.

Imani bila fact tunaita ni kuamini(believing) lakini imani(faith) inakuja kwa kuwa na uhakika kama huna uhakika hiyo sio imani ni kuamini, ILA tuna imani na yale tunayoyajua tu tofauti na hapo ni kuamini.

Mfano uliotoa ni proof tosha pia maana huwezi kunywa maji bila kuwa na imani kuwa hayo maji yatakata kiu yako.
 
Can there be two sets of facts ? Kama wewe unaamini au dunia nzima inaamini dunia ni tambalale haibadilishi dunia ikawa tambalale kweli...,

Umaanisha nini napokunywa maji wala ninajua kwamba yatakata kiu, nothing to do with faith..., lakini naweza kuamini kwamba nikimuomba Muumba kiu changu kitayeyuka na kisipoyeyuka takuwa sijaomba vya kutosha...., one is faith which has nothing to do with facts and the other is factual which has been proven again and again
 
Mungu yupi ? Sababu tukiangalia kwa haraka haraka kuna Mungu tofauti kulingana na Imani za watu tofauti..., Mimi hapa naweza kuwa nina Mungu wangu ambaye anataka nitoe kafara watumwa au watoto wanaozaliwa na kilema..., sasa hapo ni bora nimpendeze huyo Mungu ? (As far as Kilema is concerned jibu ni hapana)

Kwa kujibu swali lako ni kwamba binafsi naona kwa jamii yenye afya tunapaswa kutomtendea mwanadamu yoyote jambo ambalo linaweza kumuumiza hatuwezi kuishi kwa kupendezana sababu kinachokupendeza wewe huenda kikawa ni sumu kwa mwingine (Ukifanya mema kwa kila anayekuzunguka ni bora hata ukiwa mpagani kuliko yule anayeamini Imani fulani inayopelekea kuniletea mimi Shida)
Jambo ambalo haliwezi kukuumiza= ni sawa na kumpendeza mtu.
"Kwa kujibu swali lako ni kwamba binafsi naona kwa jamii yenye afya tunapaswa kutokumtendea mwanadamu yoyote jambo ambali linaweza kumuumiza" hahahahah huwezi kufanya jambo bila kutokumumiza mwanadamu kwa sababu kiasili binadamu ni mbinafsi(ndio maana natumia neno kumpendeza wanadamu )😁😁
AMIN AMIN NAKWAMBIA "UBAYA USIODHURU NI SAWA NA WEMA USIYO NA FAIDA"
 
Okay kwahio unakubali kwamba kuna imani ambazo zinaleta matendo mabaya (be it ni Imani Potofu or Otherwise) na sababu ni Imani huenda wewe ukadhani upo sawa kumbe umepotoka (its all good to each their own)..., ila kupotoka kwako kunaweza kukawa ni hasara na hatari kwa jamii...

Hivyo conclusion ni kwamba ni bora kitu ambacho tuna uhakika nacho ambacho ni wema tukaendelea nacho kuliko kile ambacho hatuna uhakika na kinaweza kuleta madhara
Nimekuelewa ila wewe hujanielewa
Kwenye conclusion yako unasema"ni bora kitu ambacho tuna uhakika nacho ni wema"ni kweli kabisa ila hukunielewa.
Ili utende wema au ubaya imani inahitajika eidha imani nzuri ama imani mbaya.
"Ukitenda huo wema wako utakua hauna faida na hauna tofauti na ubaya usiodhuru"
 
Conclusion ni kwamba jambo lolote kukilitenda bila imani ni dhambi( na kwa wasio amini juu ya dhambi basi ni kosa).
 
Sidhani kama matendo yote yanasukumwa na Imani mengine yanasukumwa na facts ukiumwa nikikupa dawa nataka nikuponye nikikupa sumu nataka nikuponyeshe.....

Tukija kwenye motive yako kama jamii who cares kama umepanga kumuumiza mtu ukamwagia maji ila kumbe ana kiu akanywa yale maji ni vema kuliko anayepanga kumpa maji ya kuondoa kiu kumbe hayajachemshwa hence kupata madhara...
Sijaelewa apo ukimpa sumu unataka kumponyeshe???
 
I meant kuna matendo ni factual ukiumwa nikikupa dawa nataka nikuponyeshe nikikupa sumu nataka nikuue hio ni fact and has nothing to do with faith
 
Conclusion ni kwamba jambo lolote kukilitenda bila imani ni dhambi( na kwa wasio amini juu ya dhambi basi ni kosa).
Imani ni nini (kwa mtizamo wako)labda tuanzie hapo kwanza
 
Jambo ambalo haliwezi kukuumiza= ni sawa na kumpendeza mtu.
"Kwa kujibu swali lako ni kwamba binafsi naona kwa jamii yenye afya tunapaswa kutokumtendea mwanadamu yoyote jambo ambali linaweza kumuumiza" hahahahah huwezi kufanya jambo bila kutokumumiza mwanadamu kwa sababu kiasili binadamu ni mbinafsi(ndio maana natumia neno kumpendeza wanadamu )😁😁
AMIN AMIN NAKWAMBIA "UBAYA USIODHURU NI SAWA NA WEMA USIYO NA FAIDA"
Mkuu kwenye point yako hapo juu kwenye bold nadhani hata wewe haujaifikiria kwa umakini..., Kama kila tendo linaumiza na kila tendo linatokana na Imani na Matendo ni Mapenzi ya Mungu (atleast yale mazuri) na unasema kila tendo linaumiza watu indirectly unasema Mungu anaumiza watu (Sidhani wewe kama muumini wa imani yako unaamini hayo)

Pili matendo mengi tu unaweza kuyafanya ambayo hayana athari..., kumpa mtu maji au chakula mwenye njaa unamuumiza vipi huyo uliyempa ? (Kama unaongelea third party huko mwenye wivu hayo ni matatizo yake sababu wewe kwa wakati huo unadeal na huyu mwenye njaa

Ngoja nikupe hii qoute kutoka House MD

House
: You gonna base your whole life on who you got stuck in a room with?

Eve: I'm gonna base this moment on who I'm stuck in a room with. That's what life is. It's a series of rooms. And who we get stuck in those rooms with adds up to what our lives are.
 
Can there be two sets of facts ? Kama wewe unaamini au dunia nzima inaamini dunia ni tambalale haibadilishi dunia ikawa tambalale kweli...,
Maana yangu ni kwamba: we use faith to discover facts. INGAWAJE, fact still exists in absent of faith. Kwa sababu ili iwe fact lazima ithibitike.

LAKINI, Absolutely truth is a statement that is true at all times and in all place. Something that is always true no matter the circumstance. That can not be changed. It is a fact that con not be changed.

Hivyo basi fact ni truth iliyokuwa proven lakini truth inaweza isiwe proven na hiyo haiondoi uhalali wa kuwa kweli. So imani inatusaidia kugundua kweli(truth).
 
Imani inatufanya tusiquestion sababu tunadhani / tunaamini tunachokijua ndio cha kweli..., ila kina Tomaso ambao wana question everything ndio wanatusaidia kugundua ukweli.., Imani (especially through indoctrination) unapokea mambo kama yalivyo bila kuhoji
 
kupokea bila kuhoji ni kuamini ila imani lazima upime katika ufahamu ndipo uamue.

Tatizo ni pale kuamini kunapotangulia kabla ya imani. Mwenye imani hapotoshwi ila muumini anapotoshwa. Mwenye imani anatumia akili kupambanua mambo na ana uwezo wa kuhoji tofauti na mwenye kuamini bila kuwa na imani.

Neno IMANI unalitumia isivyo, jaribu kutofautisha na kuamini.
 
Unaweza ukawa na Imani Potofu ?
 
Unaweza ukawa na Imani Potofu ?
Imani inayolenga maslahi binafsi na ile inayokuja baada ya kushawishika hiyo ni ya uharibifu ndo tunaita imani potofu ILA imani inayolenga maslahi ya wote (yaani wewe na jirani yako) ndio imani sahihi yaani Upendo.
 
Kwahio ili kutenga Imani potofu tunaweza tukasema Wema / Upendo ndio mpango mzima ni bora mpagani anayejali watu na kuwatendea watu mema kuliko mlokole mwenye husuda na judgmental...

Au kuliko ku-base maisha yako kwenye assumptions ni bora ukawa mdadisi kwenye kujua kwamba hujui hence kujifunza kila kitu kuliko kukubali kwamba kila usichokijua ni divinity....
 
Yeah sahihi kabisaa.
 
Back
Top Bottom